ANGALIA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA WAKATI WA MAHOJIANO NA GPL.
Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na
kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo
Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.…
ANGALIA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA WAKATI WA MAHOJIANO NA GPL.
Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na
kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo
Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.
Denti anayedai kubakwa na Prof Kapuya akiongea na GPL.
Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya
sheria vitazungumza lakini gazeti hili limejiridhisha pasipo shaka
yoyote kuwa denti husika ni tapeli na anacheza rafu ili kumharibia
Kapuya kwa maslahi yake.
Gazeti hili, liliamua kumchunguza denti
husika ili kumjua kiundani katika kutimiza ahadi ambayo Global
Publishers Ltd, ilishaitoa kwenye Gazeti la Risasi, nakala ya Jumamosi
iliyopita kuwa waandishi wake watafuatilia kinagaubaga na kuanika kila
kitu kupitia magazeti yake, utekelezaji unaendelea.
Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya.
HUU NDIYO WASIFU WA DENTI MWENYEWE
Baada
ya jana kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuzungumza na Kapuya ambaye
alifunguka kila kitu, gazeti hili linaendelea kwa kumchambua denti
husika, wasifu wake na maisha yake yote ya kitapeli.
ANA MAJINA MENGI
Denti
huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima
Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina
ambalo alimuingia nalo Kapuya ili kumtapeli ni Halima Hamad, upande
mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Denti akiwa busy na simu yake wakati wa mahojiano na GPL.
MSHANGAO KUHUSU DENTI HUYO
Mwezi
mmoja kabla ya sakata la Kapuya halijapamba moto, Felista alizungumza
na waandishi wetu wawili kwa nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na
mheshimiwa huyo ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista alimweleza mwandishi wa kwanza
ambaye ni mwanamke: “Nina stori kuhusu Kapuya, yule ni mtu wangu, ila
subiri kidogo nitakupa stori kamili.”
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata
mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza,
ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.”
Hata hivyo, waandishi wetu
hawakuingia kwenye mtego huo kwa sababu mbili. Mosi; si kawaida ya
Global Publishers kuandika habari zenye sura ya upande mmoja kwa maslahi
ya mtu, isipokuwa husimamia zaidi weledi na mizani.
Pili; Felista
siyo mgeni kwa waandishi wetu kwa sababu ana rekodi nyingi za matukio
yenye sura ya utapeli, kwa hiyo hakuweza kufua dafu kuiingiza mkenge
Global Publishers.
Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano.
ENDELEA KUMSHANGAA DENTI HUYO
Baada
ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, kasi na ari, waandishi wetu
walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje akalifikisha suala mbali
zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati siyo kweli?
Felista
alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka hizo habari ni Leylat.
Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu nilishiriki vikao vya usuluhishi
kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana vizuri. Mimi kama shahidi
nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Mwandishi wa pili alipomuuliza, alijibu:
“Jamani siyo mimi, yule ni Leila. Yule mtoto sijui kafikishaje hayo
mambo huko, ila mimi najua kila kitu.”
Baadaye Felista alimpigia simu
yule mwandishi wa kiume, akamwambia: “Kama utanihakikishia pesa ya
usafiri nakuja, nitaeleza kila kitu kwa sababu mimi ndiye shahidi
muhimu.”
Denti huyo akiondoka katika ofisi za GPL baada ya mahojiano.
Mwandishi wetu akambana Felista: “Mimi bado nahisi huyo Leylat unayemtaja ndiye wewe mwenyewe ila unaficha.”
Felista akajibu: “Siyo mimi, halafu sasa hivi sijui mahali alipo ila najua yote kuhusu Leylat na Kapuya.”
Mazungumzo
hayo yalifika mwisho, huku Felista akiahidi kufika ofisi za Global
Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge lakini baada ya kukata simu, dakika tatu
baadaye alimpigia simu mwandishi wetu, safari hii akiwa na maelezo haya:
“Nimeongea na Leylat. Amefichwa Maili Moja,
Kibaha, Pwani, hakuna watu wanaoruhusiwa kumuona zaidi ya wanaharakati
ambao wamejitolea kumsaidia kisheria.”
Felista alipotakiwa na
mwandishi wetu atoe namba ya Leylat, alijibu: “Namba hapana ila mkitaka
nitawapeleka mkamuone. Yule mtoto anasikitisha sana, unajua sasa hivi
anatumia dawa.”
AKAZUA SEKESEKE OFISINI GLOBAL PUBLISHERS
Jumamosi
iliyopita, Gazeti la Risasi likiwa lina uhakika wa asilimia zaidi ya 95
kwamba Felista ndiye anayecheza sinema yote ya Kapuya, akibadilisha
majina na kujiita mwanafunzi, lilitoa picha yake kisha likaiziba ili
kumtega kisha likamtambulisha kama shahidi muhimu kama alivyojiita.
...Akiwa nje ya ofisi za Global.
Asubuhi mapema siku hiyo, Felista alimpigia
simu mwandishi wetu akilalamika: “Mmeniharibia, Kapuya amenipigia simu
anatishia kuniua kwa sababu anasema mimi nimejifanya kiherehere kwamba
najua kila kitu.”
MWANDISHI: Wewe ungekuja ofisini tuongee vizuri.
FELISTA: Sawa nakuja ila lazima muangalie jinsi ya kunilinda, maisha yangu yapo hatarini.
Baada ya takriban saa moja, Felista alifika
Global Publishers na kusema: “Yaani hatari kweli, Kapuya amekuja
nyumbani kwangu, akiwa ameongozana na Leylat. Amesema ataniua kwa sababu
mimi ndiye kiherehere nataka kumharibia.”
MWANDISHI: Kapuya amekuja nyumbani kwako kivipi? Tena akiwa ameongozana na Leylat, mbona unatuchanganya.
FELISTA: Amekuja ndiyo, tena inavyoonekana Leylat mwenyewe sasa hivi yupo pamoja na Kapuya. Ugomvi wao umeisha.
Kapuya anafungua kesi kwa magazeti na mitandao iliyomchafua, Leylat yupo upande wake, mimi nikipingana na Kapuya si nitakufa?
MWANDISHI:
Hebu Felista usiongee sana, wewe asubuhi uliniambia Kapuya alikupigia
simu, sasa hivi unasema alikuja kwako, tukueleweje?
FELISTA: Kapuya hakupiga simu, alikuja na Leylat.
MWANDISHI: Inawezekana Kapuya akawa mtoto kiasi hicho? Na kwako alipajuaje?
FELISTA: Mimi sijui, ila pale nyumbani aliletwa na Leylat.
MWANDISHI: Haya tuambie wewe unatakaje?
FELISTA: Nataka pesa ya kodi, nikapange nyumba sehemu nyingine, pale hapanifai tena, nitauawa. Leoleo nataka kuhama.
UWAZI LIKAENDA MBELE ZAIDI
Gazeti
hili, lilimuweka ‘pending’ Felista na madai yake kisha likaingia kazini
kumtafuta Kapuya, aweze kueleza wasifu wa denti husika.
“Ni mfupi, mwembamba, mweusi, ana macho
makubwa, pua kama ya Kitutsi, kichwa kirefu,” alisema Kapuya baada ya
kukiri kumtambua msichana huyo anayejiita mwanafunzi.
Kwa kuchambua
maelezo hayo, jawabu moja kwa moja lilikwenda kwa Felista kwa sababu
sifa ambazo zimetajwa zinashabihiana naye kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Anaitwa nani?
KAPUYA: Halima Hamad.
MWANDISHI: Mmejuana kwa muda gani?
KAPUYA: Tangu mwaka 2011.
MWANDISHI: Katika kipindi hicho, ulikutana naye mara ngapi?
KAPUYA: Kama mara nne, alikuja kuomba
msaada akalipe ada Tumaini University. Nilimpa shilingi 3,000,000. Awamu
ya kwanza nilimpa shilingi 2,300,000, mara ya pili shilingi 700,000.
Nilimsaidia akasome, sikujua kama ni tapeli.
(Rejea maelezo ya
Felista kwamba alipewa shilingi 3,000,000 kwa awamu mbili. Zilianza
shilingi 2,300,000, baadaye zikafuata shilingi 700,000).
MWANDISHI: Ulijuaje kama ni tapeli?
KAPUYA: Kwanza niligundua hasomi na kuna
watu alikuwa anashirikiana nao kunizunguka ili wanitapeli. Nikagundua
pia kumbe hata Mkurugenzi wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alimtapeli kwa
njia hizohizo.
MWANDISHI: Alikwambia anaishi wapi?
KAPUYA: Yule
mtoto muongomuongo, kuna kipindi aliniambia anaishi Mbagala, baadaye
akasema Gongo la Mboto, hapa juzujuzi, alisema amehamia jirani na
Shoppers Plaza.
(Felista aliwaeleza waandishi wetu kuwa anaishi Gongo la Mboto).
MWANDISHI: Namba yake ya simu ni ipi?
KAPUYA: 0713 7...20…0 (tarakimu mbili zimefichwa).
Lengo la kuuliza namba ni kutaka kujua namba aliyonayo Kapuya ili kuifananisha na ile ya Felista ambayo ipo kwa waandishi wetu.
Namba hiyo ndiyo hasa ya Felista, hivyo kuzidi kujidhihirisha kuwa ndiye anayecheza sinema yote.
MWANDISHI: Pamoja na utapeli wake, vipi kuhusu tuhuma za kumbaka na kumuambukiza Ukimwi?
KAPUYA:
Jamani sijawahi kubaka katika maisha yangu yote. Sina Ukimwi. Huyo
mtoto anatumiwa na watu kunichafua, maana kuna SMS alinitumia akaniambia
atahakikisha sipati cheo chochote.
TUKARUDI KWA FELISTA
MWANDISHI: Kapuya ameshatufungua na tunajua wewe ndiye mhusika,
FELISTA: Siyo kweli, Kapuya anataka tu kutengeneza mambo ili ajisafishe.
MWANDISHI: Kapuya ametaja namba yako kuwa wewe ndiye mhusika. Na kwa nini ataje namba yako?
FELISTA: Labda kapata namba yangu kupitia kwa Leylat.
MWANDISHI: Kapuya amesema wewe unaitwa Halima Hamad na ndivyo ulivyojitambulisha kwake.
FELISTA: Siyo kweli, mimi naitwa Felista. Hilo jina la Halima silitambui.
(Papo
hapo, mwandishi wetu aliiangalia namba hiyo usajili wake wa laini na
Tigopesa na kubaini kwamba jina lililosajiliwa ni Halima Hamad).
MWANDISHI:
Mbona simu yako, laini na Tigopesa, imesajiliwa kwa jina la Halima
Hamad ambalo limetajwa na mheshimiwa? Halima ni nani sasa?
FELISTA: Turudi kwenye madai ya msingi, msitake kunibadilishia mada?
MWANDISHI: Wewe ndiye Halima, ndiye Felista, ndiye Leylat na Leila. Wewe ndiye unamchezea Kapuya, siyo mwanafunzi, ni tapeli.
FELISTA: Najua mnataka kunichezea mchezo. Mimi siyo Halima.
MWANDISHI: Mbona namba yako umesajili Halima?
FELISTA: Nimesema mimi siyo Halima.
KAMA HUMJUI FELISTA
Felista
wa Kapuya ndiye yule binti aliyewahi kumtapeli mke wa Rais Jakaya
Kikwete, Mama Salma kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama).
Msichana
huyo, alidai yeye ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia
mkenge na kumpa kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana,
alishtakiwa kwa utapeli, akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea,
Dar es Salaam.
Felista alikiri kuwekwa Segerea kisha akajitetea: “Kuna watu walitaka kunigombanisha na Mama Salma lakini mbona nilitoka?”
Felista,
alishawahi kumuibia marehemu Steven Kanumba kamera, alipokwenda ofisini
kwake, akijidai ni yatima na ana kipaji cha kuigiza, alipopata mwanya
tu, alimliza supastaa huyo ambaye alifariki dunia, Aprili 7, mwaka jana.
Ukiachana
na hilo la Kimei ambalo limetajwa na Kapuya, yapo matukio mengine
ambayo Felista alishayafanya, ikiwemo kudanganya anasoma alipiwe ada,
vitabu, madaftari na sare za shule, kumbe ni ‘gia’ yake ya kupata fedha
kwa njia ya udanganyifu.
SIYO MTOTO KABISA
Uchunguzi
wa gazeti hili unalo jawabu kuwa kama kuna uongo ambao jamii haipaswi
kubisa kukubaliana nao ni huu kwamba Felista ana umri wa miaka 16 na
anasoma sekondari.
Gazeti hili limebaini kuwa Felista ni mama wa
mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina
umri wa miaka 21.”
Waandishi wetu walifika mpaka Shule ya
Sekondari Turiani, Magomeni ambako alidai anasoma, huko kila mwalimu
aliyeulizwa alisema: “Hakuna mwanafunzi kama huyo anayesoma hapa labda
kama mmechanganya shule.”