Friday, April 4, 2014

Mayness Mwanahabari wa Kujitegemea & Designer: http://gopaidweekly.com/?ref=179849

Mayness Mwanahabari wa Kujitegemea & Designer: http://gopaidweekly.com/?ref=179849: http://gopaidweekly.com/?ref=179849

Picha ya Rais Obama yazua kizaa zaa


Ortiz amekana madai ya kulipwa na kampuni ya Samsung kwa picha hiyo
Ikulu ya Whitehouse imeikashifu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu nchini Marekani David Ortiz kama tangazo la kibiashara.

Marekani
Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki.
Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia kwa mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.

Ortiz mwenyewe alisema kuwa watu zaidi ya 40,00 waliisambaza picha hiyo kupitia Twitter
Bwana Carney amesema kuwa mawakili wa White House wanashauriwa kuhusu kitendo hicho cha Samsung.
"bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,'' alisema Carney
Ortiz alimpa Rais Obama Jezzi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na kisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama 'Selfie'.
"Nilimpa Jezzi na wapiga picha wake wanatupiga picha, basi nilijhisi na mimi kujipiga naye picha'' alisema mchezaji huyo.
Alikana kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa kwa picha hio.

Na BBC Swahili

http://gopaidweekly.com/?ref=179849

http://gopaidweekly.com/?ref=179849

HATUA KUMI ZA KUCHAGUA MCHUMBA KWA PANDE ZOTE MWANAUME/MWANAMKE





Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.


Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Wanawake husema wamechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Wamekua wakiniomba ushauri. Nia yao ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Hoja ni kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.


Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo Mwanaume/Mwanamke anaweza kutumia kumpata Mwanaume/Mwanamke mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA
-Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

NAY KUMUOA SIWEMA KABLA YA KUJIFUNGUA

Nay akiwa na mpenzi wake Siwema.
Stori: MAYASA MARIWATA
MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema yupo kwenye mikakati ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Siwema baada ya kumtundika mimba.
Siwema wa Nay.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema anajivunia kukaribia kuitwa baba na kizuri ni kwamba msichana aliyempa mimba alikuwa na ndoto za…
Nay akiwa na mpenzi wake Siwema.
Stori: MAYASA MARIWATA
MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema yupo kwenye mikakati ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Siwema baada ya kumtundika mimba.
Siwema wa Nay.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema anajivunia kukaribia kuitwa baba na kizuri ni kwamba msichana aliyempa mimba alikuwa na ndoto za kumuita mke wake hivyo ndoa itafungwa kabla ya mtoto kuzaliwa.
“Kikubwa naomba Mungu mipango yangu iende kama nilivyopanga kwa sababu nataka kabla mtoto hajazaliwa tuwe ni wanandoa tunaotambulika kwa Mungu kwa kufunga pingu za maisha,” alisema Nay.
Akizungumzia kubebeshwa mimba na msanii huyo, Siwema aliliambia Ijumaa: “Najisikia furaha sana kumbebea mimba Nay, tumetoka mbali naamini ndoto yetu ya kuoana itatimia siku si nyingi.”

Soma Magazeti ya leo April 4, 2014 VAI ACHEZEA KICHAPO

Stori: Gladness Mallya
KICHAPO! Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amechezea kichapo ‘vitasa’ kutoka kwa bwana’ke aliyetajwa kwa jina la Boniface Matiku ‘Bonny’.
Vai akiugulia maumivu ya kipigo hevi kutoka kwa bwana'ke.
Kwa mujibu wa sosi wetu, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni mishale ya usiku nyumbani kwa msanii huyo maeneo ya Mwananyamala-Hospitali jijini Dar baada ya wawili hao kutofautiana.
Ilidaiwa kwamba, Vai akiwa amelala nyumbani alipigiwa simu na Bonny lakini…
Stori: Gladness Mallya
KICHAPO! Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amechezea kichapo ‘vitasa’ kutoka kwa bwana’ke aliyetajwa kwa jina la Boniface Matiku ‘Bonny’.
Vai akiugulia maumivu ya kipigo hevi kutoka kwa bwana'ke.
Kwa mujibu wa sosi wetu, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni mishale ya usiku nyumbani kwa msanii huyo maeneo ya Mwananyamala-Hospitali jijini Dar baada ya wawili hao kutofautiana.
Ilidaiwa kwamba, Vai akiwa amelala nyumbani alipigiwa simu na Bonny lakini hakupokea ndipo mwanaume huyo akahisi labda alikuwa amechepuka kutoka njia kuu na kwenda kusaliti penzi lao.
Ilielezwa kwamba jamaa huyo alipotimba nyumbani hapo, alimhoji Vai kwa nini alikuwa hapokei simu huku akikutana na meseji za WhatsApp za kumtongoza kutoka kwa mwanaume mwingine ndipo msanii huyo aliyeishi naye kwa kipindi kirefu akamjibu mbovumbovu.
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika matanuzi.
Chanzo chetu kilidai kuwa mdomo mchafu ulimponza Vai ambaye alipokea kipigo ‘hevi’ hadi akapasuka kichwani lakini haikufahamika alipigwa kwa kutumia kitu gani.
Hata hivyo, duru za kihabari zilidai kuwa timbwili hilo halikuishia ndani kwani wawili hao walitoka nje na kuendeleza mtiti hadi Vai akapoteza ile ‘smart phone’ yake.
Chanzo hicho kilitiririka kwamba baada ya kuona hali inakuwa mbaya huku Vai akitokwa damu, majirani waliwaamulia kisha kumkimbiza Vai hospitalini ambako alishonwa nyuzi kumi kichwani.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Vai ambaye alipopatikana alizungumza kwa tabu huku akilalamika maumivu makali.
Vai akiwa na bandeji kichwani baada ya kichapo.
“Ni kweli Bonny amenipiga sana sijiwezi,” alisema Vai ambaye anatarajia kusukuma sokoni filamu yake ya Beautiful Liar.
Alipoulizwa chanzo cha ugomvi na kama Bonny amechukuliwa hatua gani, Vai alisema: “Ni wivu wa mapenzi. Bonny ana wivu sana. Sijamchukulia hatua yoyote kwani nampenda sana Bonny. Pia ameniomba msamaha na ananihudumia hivyo nimemsamehe.”
Hivi karibu Vai aliripotiwa na gazeti hili baada ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndipo mgogoro na Bonny ulipoanza.

MAMA ADAI KUIBIWA MTOTO LEBA


Stori: Chande abdallah na Deogratius Mongela 
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili aliojifungua Machi 28, mwaka huu.
Mama Shakila Bakari (30), mkazi wa Mbagala jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto wake wa kwanza,lakini kukatokea hitilafu ndogo ya mwanaye huyo…
Stori: Chande abdallah na Deogratius Mongela 
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili aliojifungua Machi 28, mwaka huu.
Mama Shakila Bakari (30), mkazi wa Mbagala jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto wake wa kwanza,lakini kukatokea hitilafu ndogo ya mwanaye huyo kukatwa kidogo na mkasi uliosababisha jeraha kwenye paji la uso.
“Waliniambia walimgusa kidogo kwa bahati mbaya na mkasi, lakini wakasema hakuna tatizo, waliniwekea kifuani na damu ikawa imenivujia kidogo, baadaye nilijisikia uchungu tena, manesi wakamtoa mtoto yule kifuani kwangu ili nipate nafasi ya kujifungua tena, nilipojifungua walinionyesha motto wa kiume,” alidai mama huyo.
Shakila alidai kuwa, tofauti na matarajio yake, alikabidhiwa mtoto aliyejifungua wakati huo huku Yule wa mwanzo akipewa maelezo yasiyoeleweka. “Niliwashangaa manesi. Waliponiona sibabaiki kuhusiana na mtoto wangu ndipo wakaniletea mtoto mwingine wakidai kuwa ndiye huyo. Nilipomchunguza nilibaini kuwa alikuwa wa kiume wakati mimi nilimzaa wa kike, halafu huyu niliyeletewa hakuwa na kijereha.
”Baada ya kumkataa mtoto huyo, Shakila alidai manesi waliondoka na kichanga kile na katika hali ya kushangaza, walisimamia kauli yao ya awali kuwa hakuzaa motto mwingine zaidi ya huyo aliyekuwa naye.
Dada wa Shakila aliyejitambulisha kwa jina la Sikujua Bakari alisemawakati mdogo wake akijifungua yeye pamoja na shemeji yake (mume wa Shakila) hawakuruhusiwa kuingia ndani, lakini baada ya kujifungua walikwenda kumuona akiwa na mtoto mmoja wa kiume, walipompa pongezi walipatwa na mshangao.

PASTOR FUSKA ANASWA!


Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar baada ya kunaswa na wanawake watatu wakimchezea utupu.
OFM…
Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar baada ya kunaswa na wanawake watatu wakimchezea utupu.
OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR
Ilikuwa Jumanne ya Aprili Mosi, 2014, saa 4:14 asubuhi, chanzo cha habari kilipiga simu chumba cha habari cha Global na kuwataka makachero wa OFM ambapo alipounganishwa nao alisema:
“Jamani kama kweli hapo ni OFM nina malalamiko. Mimi nimeshtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na pastor (mchungaji) mmoja anaitwa Rubanguka.
Pasta John Paul Simon Rubanguka akijaribu kujitetea.
“Huyu pastor amempa dili dada mmoja kumtafutia wasichana wazuri watatu na kuwapeleka kwenye nyumba moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake huku wao wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo. Wasichana wameshapatikana.”
Makamanda wa Polisi wakimbananisha na kumtuliza Pasta huyo ili apunguze munkari.
MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUU
Mtoa habari huyo aliendelea kudai kuwa, pastor huyo alisema wasichana watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia usaili wa kwenda kuwauza kwenye kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye ni wakala wa kuwapelekea malaya huko.
Pastor akiwa na mmoja wa wanawake waliofumaniwa naye.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi wanawake hao kitita cha shilingi 300,000 kila mmoja kwa wale watakaofaulu kumchezea vizuri, sanjari na kuwakatia hati za kusafiria ‘passport’.
Makamanda wa OFM wakimtuliza Pasta.
OFM YAWEKA MTEGO
Baada ya kupata ishu nzima, OFM ilifanya ukachero na kugundua mahali ambapo tukio hilo lilipangwa kufanyika, ni kwenye danguro moja lililopo Kinondoni jijini Dar.
Wanawake walionaswa katika tukio hilo wakivaa viwalo vyao.
OFM ilifika kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu wake ambapo walifanikiwa kuweka mitambo yao sambamba na kulishirikisha jeshi la polisi kwa ajili ya kumnasa mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo hivyo.
Saa 8:11 mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo waliwashuhudia warembo watatu, weupe wakielekea kwenye nyumba ambayo mtoa habari wetu aliielekeza.
Kitambulisho cha Pasta.
PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE
Saa 11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka. Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa wanawake hao.
Bango lililopo Kinondoni Mkwajuni, Dar likieleza lilipo kanisa la Pasta huyo.
MCHEZO WAANZA
Saa 11:40 jioni, makachero wa OFM walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa, tayari mchezo ulishaanza ambapo waliwataarifu polisi na kuungana nao kwenda kuvamia nyumba hiyo.
Msafara wa OFM na polisi hao ulifika nje ya chumba kilichokuwa kikidaiwa kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki na wanawake waliokuwa kama wapo kwenye darasa la siri zilisikika.
Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.
PASTOR APATA MCHECHETO
Pasta John na wanawake hao walitii amri kwa kufungua mlango ambapo mchungaji huyo alikumbwa na mchecheto na kutaka kurukia juu ya dari lakini polisi walimtafadhalisha kutulia pamoja na wanawake hao kama walivyo.
OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa wakimnengulia viuno.
Baada ya kupewa kibano, warembo hao walimwanika pastor huyo kwamba ndiye aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu ili awalipe shilingi laki tatu kila mmoja, pia kuwapeleka Uarabuni kwenye kasino.
UTETEZI WA PASTOR
Kwa upande wake, Pastor John alijitetea kuwa anaomba asamehewe kwa gharama zozote ili taarifa hizo zisifike popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri yake bali shetani alimpitia.
“Jamani naomba tumalize humuhumu ndani, mnajua mimi ni Pastor wa Kanisa la Maximum Deliverance, sasa ukweli ni kwamba waumini wangu hawatanielewa, chondechonde ilindieni kazi yangu jamani,” alijitetea.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio, pastor huyo na wanawake ‘wake’ walikuwa kwenye harakati za kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zinazostahili.
KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Siku zote kazi ya OFM ni kuwajibikia matendo maovu na si kuwaonea watu  kwa lengo la kuwachafua. OFM inapopata habari huichunguza ukweli wake kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kuifanyia kazi moja kwa moja, yaani kufika kwenye eneo la tukio.
Lengo kubwa la kutoa habari za aina hii ni kuwakumbusha watu namna ya kuishi maisha yanayompendeza  Mungu. Wengi wamebadilika, sasa wanaishi vizuri wakiwa watu wapya na wanyenyekevu pia wenye kufundisha wenzao.