Monday, September 3, 2012

Haya sasa Siasa imekua gumzo kila kona. Nani alaumiwe kwa hili jamani? Niserikali iliyoko madarakani au ni nani? Nashindwa kuelewa ndugu zanguni tumempotezea mwana habari wetu kisa Siasa. Jamani kwanini hatu badiliki? Hebu ona ameshabadili jina tunamwita Marehemu Daudi Mwangosi tutakukumbuka sana ndugu yetu. Rest in Peace Daudi
Nampenda sana twiga nafurahia kuwa na nchi yenye wanyama wazuri kama huyu jamani Twiga ni mnyama anaye vutia mwenye sifa za kila aina ana mwendo wa maringo jamani Twiga anavutia. Najivunia sana kuwa Mtanzania naipenda sana nchi yangu.
Maisha ni mazuri kama ukijikubali mwenyewe, pia maisha humwendea mtu vibaya pale ambapo yeye huya kosea. Maisha ni kujipanga usisubili kupangiwa. Ona watu tunafurahia maisha na tunasahau shida zote za hapo nyuma aah maisha ni raha jamani. Karibuni tufurahi sote.