Friday, August 29, 2014

Patrick Ole Sosopi Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA (Baraza la Vijana Chadema) awaomba watu wampigie kura

Patrick Ole Sosopi ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA (Baraza la Vijana Chadema). Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi mbalimbali vya maisha yake. Historia yake ya uongozi ni kuanzia akiwa Elimu ya Sekondari mpaka Chuo Kikuu.

Patrick Ole Sosopi. Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani. Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). 

Ni mpenda maendeleo na amekua mstari wa mbele kutetea ukombozi wa Taifa letu. Akielezea historia yake kwa ufupi Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na watu wote kwa ujumla na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.


Patrick Ole Sosopi ni mojawapo wa waanzilishi wa Chadema Students Organizati (CHASO) mkoani Iringa,  Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja na Mbeya. Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara. Hivyo anaomba kula zako wewe Mtanzania ili kuleta mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu. Uchaguzi unategemewa kufanyika tarehe 10/9/2014 Dar es salaam Makao makuu ya Chama.



 Partick Ole Sosopi akihutubia Wananchi wa Iringa Mjini




 Alipokuwa kwenye uchaguzi wa Kalenga Mwanzoni mwa mwaka huu

 Akihutubia wananchi wa Wilaya ya Kilolo
 Akiwa katika Jimbo lake la Isamani kama Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo hilo.


 Akiwa Pawaga na wadau wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

 

Monday, August 18, 2014

Man U yaanza ligi kwa kichapo


Wachezajii wa Manchester United wakitoka kwa huzuni baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka Swansea
Manchester United imeanza vibaya katika msimu huu wa ligi kuu ya England baada ya kukubali kichapo cha magoli 2 - 1 dhidi ya Swansea.
Swansea ndio waliokuwa kwanza kuandika bao katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza bao lilofungwa na Ki Sung Yueng.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Manchester United walikuwa nyuma kwa bao 1 - 0.
Baada ya kutoka mapunziko Man U walionekana kuja kwa kasi ambapo walilishambulia lango la Swansea mara mara na ndipo katika dakika ya 53 Nahodha mpya wa timu hiyo Wayne Rooney akafanikiwa kusawazisha goli kwa kuunganisha mpira wa kona.
Hata hivyo kama vile waswahili wasemavyo siku ya kufa nyani miti yote huteleza, dakika ya 72 Gyfi Sigurdsson wa Swansea baada ya walinzi wa Manchester United kujichanganya alipigilia msumari wa moto kwenye kidonda na kuandika bao la ushindi kwa Swansea na hivyo kufanya hadi mechi inamalizika Manchester United ikawa imefungwa 2 - 1.

Chanzo  BBC Swahili

MKE WA MTU AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO, KISA NI MUME WA MTU


Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
My God! Mke wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.
 Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa…
Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
My God! Mke wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.


Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini hapa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.


Mama mdogo wa Mwajuma Prima akimuuguza mwanaye.
“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?
“Mabishano yalishika kasi na mwishowe walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa, akaingia jikoni na kuipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka na kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.


 Mume wa Mwajuma Prima akiwa na mama mdogo wa mwajuma.
Akizungumza na gazeti hili, mama mdogo wa Mwajuma alisema: “Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana.
“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia jikoni akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia mwanangu mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”

Soma magazeti ya leo Jumatatu ya tarehe 18 Agosti 2014. DIAMOND, WEMA MWISHO UMEFIKA

Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya
Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Suala la…
Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya
Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala la Wema kukashifiwa liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Wema wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa Instagram kwamba ni kwa nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno jukwaani (hivi karibuni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya kumfungulia biashara ya maana?
“Tujaribuni kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu Diamond. Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno namna ile kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye ni mfuasi wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa kumshauri ‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonesha Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata mauno jukwaani kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.
WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau hao walimtaka Wema kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy Sumari (2005), Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi kwa jinsi wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza kuendesha maisha yao bila kudhalilishwa majukwaani.
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata mauno.
DIAMOND AWAJIBU
Baada ya wadau hao kumshauri Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo walidai yanamdhalilisha, kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond alishindwa kuvumilia ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka wake unaodaiwa kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond alieleza kwamba yeye kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu kama mpenzi wake na suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.
WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri ningewaona kweli mna akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu (Wema) kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe, mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. “Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo anatakiwa aamue kunywa maji!
Aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda.
“Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu, nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”
WAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya waraka huo, mashabiki na wadau waliopo kwenye mtandao huo walimgeukia Diamond kwa kumlaumu kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona amemfungulia dada yake Esma Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa akimtumia tu bila faida yoyote?
MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana na waraka huo, aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika wa kwake na kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.
MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada ya meneja huyo kubwanga manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na penzi hilo la mwanaye ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha hivyo anaacha ‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.
Mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu
“Jamani sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao wazungushane wee mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo imemchanganya.
TUJIKUMBUSHE
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Monday, August 11, 2014

Gazeti la leo tarehe 11 Agosti Michezo ARSENAL BINGWA NGAO YA JAMII

Arsenal wakiwa na Ngao ya Jamii baada ya kuipiga Manchester City 3-0.
Santi Carzola akishangilia bao lake la kwanza kwa Arsenal.
Aaron Ramsey akifunga bao la pili kwa Arsenal.
Bao la tatu la Arsenal lililofungwa na Olivier Giroud.

Raha ya ushindi.
KLABU ya Arsenal imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Manchester City mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Wembley jijini London usiku huu. Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Cazorla 21, Ramsey 42 na Giroud 60.