Maumivu ya Moyo yanaweza sababishwa na kitu chochote kinacho weza kukufanya upate maumivu.
Rose ni binti anayeishi na wazazi wake katika Mkoa wa Iringa mji mdogo wa Mafinga Kinyanambo. Walipokuwa wakila chakula alipokea simu na haikujulikana ya nani na nini kilitokea Leo tunaendelea.....
Baada ya Rose Kuzinduka aliendelea kulia mama yake alipo uliza kunani
Rose alijibu kwa husuni Joel, mama aliposikia hivyo alishituka pia. Joel
ni kijana anayeishi mjini Dar-es-salaam ni mchumba wa rose ambaye
walipanga kuoana siku chache zijazo pia walishakua wamemaliza hatua zote
za kufanya ajulikane ni mumewe mtalajiwa. Mama aliendelea kuuliza ili
apate kujua ukiundani zaisi.
"Mama Joel yupo kituo cha polisi na inaonekana hana hali nzuri kwani
amepata ajali, kinachoniliza zaidi inasemekana alikua akisafilisha
madawa ya kulevya kuelekea South Africa ndipo wakapata ajali na
kupelekwa kitu cha polisi" Alisimulia Rose huku akili kwa uchungu mama
alijitahidi kumbembeleza Rose lakini hakuelewa.
Siku ilipita kesho yake Rose aliamua kusafiri kuelekea Dar-es-salaam
kujua vyema mambo yaliyotokea. Aliwasili mnamo saa 10 jioni hakutaka
kupumzika na kwenda moja kwa moja katika kituo cha police alicho elezwa.
Alipofika akajieleza na polisi wakamruhusu aingie kumwona mtuhumiwa
ambaye alidaiwa kuwa ni mchumba wake. Alipofika ndani alishitushwa
kumkuta mtu anaye oneshwa si yeye. Rose alishangaa na kuwaeleza polisi
kuwa huyo siye lakini polisi walimuhakikishia kuwa mwenye simu ile ndiye
huyo. Baada ya Maelezo hayo yule mtuhumiwa alijaribu kusema ukweli kuwa
simu hiyo si yake kuna gari walilogongana nalo ndio simu hiyo ilitoka
nae kwakua na shida akaichukua na kuifanya yake na hakua anamfaham
mwenye simu. Rose alizidi kuchanganyikiwa kusikia hivyo kwani alihisi
kabisa Joel amefariki dunia. Alikimbia hospitali ya Muhimbili na kumkuta
Joel katika wodi ya watu mahututi akiwa hawezi kuongea na akipumlia
mipira uso wake ukiwa hautamaniki kwa dam na uvimbe. Rose aliwapigia
simu ndugu na jamaa wa karibu wakiwemo wazazi wake na kuwaeleza ukweli
wa mambo ulivyo. Alienda kuonana na Dacktari wa mifupa akaambiwa mgonjwa
wake amepata shida kubwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji na kutolewa figo
1. hapo Rose alizidi kuhisi maisha ya Joel yanaishia hapo. Madaktari
walipanga kumwingiza kwenye chumba cha upasuaji saa 3 asubuhi ya siku
inayofuata.
Masaa alisogea hatimaye kukakucha. Joel aliandaliwa kwa ajili ya kuingia
chumba cha upasuaji (Machinjioni). Rose alisali kila dakika kumwomba
Mungu amponye mpedwa wake. Mda ulifika hatimaye Joel akaingizwa chumba
cha upasuaji. Rose akiwa nnje ya chumba aliendelea kusali masaa yalizidi
kusonga mbele masaa mawili aliisha bila mtu yeyote kutoka nnje wala
kuingia ndani ya chumba hicho. Baada ya dakika kadhaa alitoka Muuguzi
mmoja akionekana kuwa na haraka sana na kukimbia kama mtu anayefuata
kitu au anaye mkimbilia mtu furani. Rose alijalibu kumsimamisha lakini
hakumsikiliza. Baada ya muda kidogo yule muuguzi alirudi tena na Rose
alipo msimamisha alijalibu kumsikiliza lakini akiwa anatembea kwa kasi
sana.
"Dada samahani mgonjwa wangu vipi?"
"Samahanani anaonekana katokwa sana na damu nyingi sana tumwombe Mungu kwa bado madaktari wanaendelea na upasuaji"
Rose alikaa chini taratibu huku akimtaja mungu wake. Mala dactari
alitoka na kuonekana kama mtu aliye kata tamaa vile. Rose hakuweza hata
kumsogelea kwani hakuwa na nguvu tena .... Je Joel yupo katika hali gani
na Dactari ana kipi cha kumweleza Rose. Tutaendelea keshoooooooo. Na
Mayness Chapote
No comments:
Post a Comment