Wednesday, November 20, 2013

Unyama uliopitiliza Mume amcharanga mapanga mkewe na kumkata mguu


Stori: Imelda Mtema

WAKATI mwingine unakosa maneno ya kuelezea ukatilia uliopitiliza unaofanywa na baadhi ya watu hapa duniani dhidi ya binadamu wenzao. Tukio lililompata binti Gati Chacha, mkazi wa Kijiji cha Kinyantila, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara

tena alilofanyiwa na mumewe Bw. Chacha Mwita, linahuzunisha na kusikitisha kama siyo kustaajabisha. Uwazi limekinasa kisa kizima.
Binti Chacha amepewa kilema cha maisha baada ya kukatwa mguu wa kuume na mumewe, sababu ikiwa ni kuchelewa tu kumfungulia mlango aliporejea nyumbani usiku saa tatu, unaweza usikubaliane na sababu hiyo, lakini hivyo ndivyo inavyoelezwa kwa mshangao wa kila mtu!
Simulizi kutoka kinywani kwa mwanamke huyo inadai kuwa, siku ya tukio asubuhi mumewe alimuaga anakwenda kutafuta mboga ya familia lakini…
Stori: Imelda Mtema
WAKATI mwingine unakosa maneno ya kuelezea ukatilia uliopitiliza unaofanywa na baadhi ya watu hapa duniani dhidi ya binadamu wenzao. Tukio lililompata binti Gati Chacha, mkazi wa Kijiji cha Kinyantila, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara
tena alilofanyiwa na mumewe Bw. Chacha Mwita, linahuzunisha na kusikitisha kama siyo kustaajabisha. Uwazi limekinasa kisa kizima.
Binti Chacha amepewa kilema cha maisha baada ya kukatwa mguu wa kuume na mumewe, sababu ikiwa ni kuchelewa tu kumfungulia mlango aliporejea nyumbani usiku saa tatu, unaweza usikubaliane na sababu hiyo, lakini hivyo ndivyo inavyoelezwa kwa mshangao wa kila mtu!
Simulizi kutoka kinywani kwa mwanamke huyo inadai kuwa, siku ya tukio asubuhi mumewe alimuaga anakwenda kutafuta mboga ya familia lakini hakurudi mpaka saa tatu usiku.
Alisema: “Aliporudi hiyo saa tatu alibisha hodi, mimi kwa sababu nilishalala nikachelewa kusikia, lakini niliposikia nilikwenda kumfungulia mlango, lakini akaja juu akitaka kujua ni kwa nini nilichelewa kumfungulia mlango.
“Nilimuomba msamaha, nikamwambia nilishapitiwa na usingizi, hata watoto walishalala, hakunisikiliza, akachukua  panga na kunikata miguu yote.
“Huu mguu wa kulia aliukata kabisa, ukatengana na sehemu yake, huu wa kushoto hakuumalizia, ukawa unaning’inia, nikawahishwa Hosptali ya Wilaya Tarime kushonwa ndiyo ikawa salama yangu kubaki na mguu mmoja kama hivi.” (akalia).
“Inauma sana jamani! Ni kwa nini mume wangu alinikata miguu kwa panga kama anayekata pingili za mua?
“Siamini hata sasa kama ni akili zake kwani mimi ni mke wake nimemzalia watoto wawili, ni adhabu gani hii aliyonipa?” alihoji mwanamke huyo huku machozi yakiendelea kumchuruzika.
Akaendelea: “Kutoka moyoni nasema kuwa, baada ya tukio lile nilitaka sana kurudi nyumbani kwa wazazi nikauguze vidonda, lakini  tatizo ni kwamba kwa vile nililipiwa mahari siwezi kurudi wala mama hawezi kunikubalia nirudi mpaka baba aje kutoa ruhusa.” (matatizo ya mila na desturi na ukatili dhidi ya mwanamke).
Naye mama mzazi wa mwanamke huyo (hakutaja jina lake) maarufu kama mama Gati akilia kwa uchungu mkubwa alisema kwamba amekuwa akimwaga machozi kila siku tangu kutokea kwa tukio hilo la mwanaye kukatwa mguu na mumewe.
“Mimi nalia tu jamani! Nalia kila siku, nakumbuka siku nilipomzaa huyu mwanangu furaha niliyokuwa nayo na siku alipokatwa huu mguu uchungu nilioupata, lakini nimemwachia Mungu,” alisema mama huyo huku akilia.
Aliongeza: “Kwa utamaduni wetu huku, baba wa mtoto aliyekatwa mguu yaani mume wangu ndiye mwenye mamlaka ya kuamua binti yetu arudi nyumbani au aendelee kubaki kwa mume wake kwa hiyo nashindwa kuamua chochote.”
Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime-Rorya lilimtia mbaroni  mtuhumiwa huyo na kumfikisha  mahakamani.
Kwa kumalizia, Gati alimewaomba Watanzania watakaoguswa na tatizo lake wamsaidie ili aweze kurudi nyumbani kwa wazazi wake na kuachana na mila zinazomzuia kwa sababu baba mkwe wake (hakumtaja jina) amekuwa akimkejeli kwamba yeye (Gati) anaona raha kulala kitandani wakati mtoto wake (mtuhumiwa) analala chini jela.
“Hii kauli ya baba mkwe wangu inaniweka hatarini mimi. Naomba nisaidiwe nirudi nyumbani kwa wazazi wangu,” alisema Gati.
Hata hivyo, mama mzazi wa Gati alisema hana uwezo wa kumsaidia mwanaye huyo atakaporudi nyumbani akiwa katika hali hiyo kwa kuwa maisha yao ni duni.
Akaomba kwa yeyote atakayeguswa na tatizo la binti yake Gati awasaidie msaada wowote wa kibinadamu kwa kutumia namba 0713 612533 na Mungu atawabariki.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kikatili. Mguu wa Gati unaoonekana pichani umehifadhiwa chumba cha baridi katika hospitali hiyo.
Usikose kuangalia Kipindi cha  Wanawake Live cha Joyce Kiria kitakachorushwa leo usiku na Runinga ya EATV ili uupate mkasa huu ‘laivu’.

Soma kiundani magazeti ya Jumanne ya tarehe 19/11/2013 hapa... ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA HUYU HAPA



ANGALIA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA WAKATI WA MAHOJIANO NA GPL.
Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.…
ANGALIA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA WAKATI WA MAHOJIANO NA GPL.
Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.
Denti anayedai kubakwa na Prof Kapuya akiongea na GPL.
Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya sheria vitazungumza lakini gazeti hili limejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa denti husika ni tapeli na anacheza rafu ili kumharibia Kapuya kwa maslahi yake.
Gazeti hili, liliamua kumchunguza denti husika ili kumjua kiundani katika kutimiza ahadi ambayo Global Publishers Ltd, ilishaitoa kwenye Gazeti la Risasi, nakala ya Jumamosi iliyopita kuwa waandishi wake watafuatilia kinagaubaga na kuanika kila kitu kupitia magazeti yake, utekelezaji unaendelea.
Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya.
HUU NDIYO WASIFU WA DENTI MWENYEWE
Baada ya jana kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuzungumza na Kapuya ambaye alifunguka kila kitu, gazeti hili linaendelea kwa kumchambua denti husika, wasifu wake na maisha yake yote ya kitapeli.
ANA MAJINA MENGI
Denti huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina ambalo alimuingia nalo Kapuya ili kumtapeli ni Halima Hamad, upande mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Denti akiwa busy na simu yake wakati wa mahojiano na GPL.
MSHANGAO KUHUSU DENTI HUYO
Mwezi mmoja kabla ya sakata la Kapuya halijapamba moto, Felista alizungumza na waandishi wetu wawili kwa nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na mheshimiwa huyo ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista alimweleza mwandishi wa kwanza ambaye ni mwanamke: “Nina stori kuhusu Kapuya, yule ni mtu wangu, ila subiri kidogo nitakupa stori kamili.”
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza, ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.”
Hata hivyo, waandishi wetu hawakuingia kwenye mtego huo kwa sababu mbili. Mosi; si kawaida ya Global Publishers kuandika habari zenye sura ya upande mmoja kwa maslahi ya mtu, isipokuwa husimamia zaidi weledi na mizani.
Pili; Felista siyo mgeni kwa waandishi wetu kwa sababu ana rekodi nyingi za matukio yenye sura ya utapeli, kwa hiyo hakuweza kufua dafu kuiingiza mkenge Global Publishers.
Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano.
ENDELEA KUMSHANGAA DENTI HUYO
Baada ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, kasi na ari, waandishi wetu walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje akalifikisha suala mbali zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati siyo kweli?
Felista alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka hizo habari ni Leylat. Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu nilishiriki vikao vya usuluhishi kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana vizuri. Mimi kama shahidi nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Mwandishi wa pili alipomuuliza, alijibu: “Jamani siyo mimi, yule ni Leila. Yule mtoto sijui kafikishaje hayo mambo huko, ila mimi najua kila kitu.”
Baadaye Felista alimpigia simu yule mwandishi wa kiume, akamwambia: “Kama utanihakikishia pesa ya usafiri nakuja, nitaeleza kila kitu kwa sababu mimi ndiye shahidi muhimu.”
Denti huyo akiondoka katika ofisi za GPL baada ya mahojiano.
Mwandishi wetu akambana Felista: “Mimi bado nahisi huyo Leylat unayemtaja ndiye wewe mwenyewe ila unaficha.”
Felista akajibu: “Siyo mimi, halafu sasa hivi sijui mahali alipo ila najua yote kuhusu Leylat na Kapuya.”
Mazungumzo hayo yalifika mwisho, huku Felista akiahidi kufika ofisi za Global Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge lakini baada ya kukata simu, dakika tatu baadaye alimpigia simu mwandishi wetu, safari hii akiwa na maelezo haya:
“Nimeongea na Leylat. Amefichwa Maili Moja, Kibaha, Pwani, hakuna watu wanaoruhusiwa kumuona zaidi ya wanaharakati ambao wamejitolea kumsaidia kisheria.”
Felista alipotakiwa na mwandishi wetu atoe namba ya Leylat, alijibu: “Namba hapana ila mkitaka nitawapeleka mkamuone. Yule mtoto anasikitisha sana, unajua sasa hivi anatumia dawa.”
AKAZUA SEKESEKE OFISINI GLOBAL PUBLISHERS
Jumamosi iliyopita, Gazeti la Risasi likiwa lina uhakika wa asilimia zaidi ya 95 kwamba Felista ndiye anayecheza sinema yote ya Kapuya, akibadilisha majina na kujiita mwanafunzi, lilitoa picha yake kisha likaiziba ili kumtega kisha likamtambulisha kama shahidi muhimu kama alivyojiita.
...Akiwa nje ya ofisi za Global.
Asubuhi mapema siku hiyo, Felista alimpigia simu mwandishi wetu akilalamika: “Mmeniharibia, Kapuya amenipigia simu anatishia kuniua kwa sababu anasema mimi nimejifanya kiherehere kwamba najua kila kitu.”
MWANDISHI: Wewe ungekuja ofisini tuongee vizuri.
FELISTA: Sawa nakuja ila lazima muangalie jinsi ya kunilinda, maisha yangu yapo hatarini.
Baada ya takriban saa moja, Felista alifika Global Publishers na kusema: “Yaani hatari kweli, Kapuya amekuja nyumbani kwangu, akiwa ameongozana na Leylat. Amesema ataniua kwa sababu mimi ndiye kiherehere nataka kumharibia.”
MWANDISHI: Kapuya amekuja nyumbani kwako kivipi? Tena akiwa ameongozana na Leylat, mbona unatuchanganya.
FELISTA: Amekuja ndiyo, tena inavyoonekana Leylat mwenyewe sasa hivi yupo pamoja na Kapuya. Ugomvi wao umeisha.
Kapuya anafungua kesi kwa magazeti na mitandao iliyomchafua, Leylat yupo upande wake, mimi nikipingana na Kapuya si nitakufa?
MWANDISHI: Hebu Felista usiongee sana, wewe asubuhi uliniambia Kapuya alikupigia simu, sasa hivi unasema alikuja kwako, tukueleweje?
FELISTA: Kapuya hakupiga simu, alikuja na Leylat.
MWANDISHI: Inawezekana Kapuya akawa mtoto kiasi hicho? Na kwako alipajuaje?
FELISTA: Mimi sijui, ila pale nyumbani aliletwa na Leylat.
MWANDISHI: Haya tuambie wewe unatakaje?
FELISTA: Nataka pesa ya kodi, nikapange nyumba sehemu nyingine, pale hapanifai tena, nitauawa. Leoleo nataka kuhama.
UWAZI LIKAENDA MBELE ZAIDI
Gazeti hili, lilimuweka ‘pending’ Felista na madai yake kisha likaingia kazini kumtafuta Kapuya, aweze kueleza wasifu wa denti husika.
“Ni mfupi, mwembamba, mweusi, ana macho makubwa, pua kama ya Kitutsi, kichwa kirefu,” alisema Kapuya baada ya kukiri kumtambua msichana huyo anayejiita mwanafunzi.
Kwa kuchambua maelezo hayo, jawabu moja kwa moja lilikwenda kwa Felista kwa sababu sifa ambazo zimetajwa zinashabihiana naye kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Anaitwa nani?
KAPUYA: Halima Hamad.
MWANDISHI: Mmejuana kwa muda gani?
KAPUYA: Tangu mwaka 2011.
MWANDISHI: Katika kipindi hicho, ulikutana naye mara ngapi?
KAPUYA: Kama mara nne, alikuja kuomba msaada akalipe ada Tumaini University. Nilimpa shilingi 3,000,000. Awamu ya kwanza nilimpa shilingi 2,300,000, mara ya pili shilingi 700,000. Nilimsaidia akasome, sikujua kama ni tapeli.
(Rejea maelezo ya Felista kwamba alipewa shilingi 3,000,000 kwa awamu mbili. Zilianza shilingi 2,300,000, baadaye zikafuata shilingi 700,000).
MWANDISHI: Ulijuaje kama ni tapeli?
KAPUYA: Kwanza niligundua hasomi na kuna watu alikuwa anashirikiana nao kunizunguka ili wanitapeli. Nikagundua pia kumbe hata Mkurugenzi wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alimtapeli kwa njia hizohizo.
 MWANDISHI: Alikwambia anaishi wapi?
KAPUYA: Yule mtoto muongomuongo, kuna kipindi aliniambia anaishi Mbagala, baadaye akasema Gongo la Mboto, hapa juzujuzi, alisema amehamia jirani na Shoppers Plaza.
(Felista aliwaeleza waandishi wetu kuwa anaishi Gongo la Mboto).
MWANDISHI: Namba yake ya simu ni ipi?
KAPUYA: 0713 7...20…0 (tarakimu mbili zimefichwa).
Lengo la kuuliza namba ni kutaka kujua namba aliyonayo Kapuya ili kuifananisha na ile ya Felista ambayo ipo kwa waandishi wetu.
Namba hiyo ndiyo hasa ya Felista, hivyo kuzidi kujidhihirisha kuwa ndiye anayecheza sinema yote.
MWANDISHI: Pamoja na utapeli wake, vipi kuhusu tuhuma za kumbaka na kumuambukiza Ukimwi?
KAPUYA: Jamani sijawahi kubaka katika maisha yangu yote. Sina Ukimwi. Huyo mtoto anatumiwa na watu kunichafua, maana kuna SMS alinitumia akaniambia atahakikisha sipati cheo chochote.
TUKARUDI KWA FELISTA
MWANDISHI: Kapuya ameshatufungua na tunajua wewe ndiye mhusika,
FELISTA: Siyo kweli, Kapuya anataka tu kutengeneza mambo ili ajisafishe.
MWANDISHI: Kapuya ametaja namba yako kuwa wewe ndiye mhusika. Na kwa nini ataje namba yako?
FELISTA: Labda kapata namba yangu kupitia kwa Leylat.
MWANDISHI: Kapuya amesema wewe unaitwa Halima Hamad na ndivyo ulivyojitambulisha kwake.
FELISTA: Siyo kweli, mimi naitwa Felista. Hilo jina la Halima silitambui.
(Papo hapo, mwandishi wetu aliiangalia namba hiyo usajili wake wa laini na Tigopesa na kubaini kwamba jina lililosajiliwa ni Halima Hamad).
MWANDISHI: Mbona simu yako, laini na Tigopesa, imesajiliwa kwa jina la Halima Hamad ambalo limetajwa na mheshimiwa? Halima ni nani sasa?
FELISTA: Turudi kwenye madai ya msingi, msitake kunibadilishia mada?
MWANDISHI: Wewe ndiye Halima, ndiye Felista, ndiye Leylat na Leila. Wewe ndiye unamchezea Kapuya, siyo mwanafunzi, ni tapeli.
FELISTA: Najua mnataka kunichezea mchezo. Mimi siyo Halima.
MWANDISHI: Mbona namba yako umesajili Halima?
FELISTA: Nimesema mimi siyo Halima.
KAMA HUMJUI FELISTA
Felista wa Kapuya ndiye yule binti aliyewahi kumtapeli mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama).
Msichana huyo, alidai yeye ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia mkenge na kumpa kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana, alishtakiwa kwa utapeli, akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Felista alikiri kuwekwa Segerea kisha akajitetea: “Kuna watu walitaka kunigombanisha na Mama Salma lakini mbona nilitoka?”
Felista, alishawahi kumuibia marehemu Steven Kanumba kamera, alipokwenda ofisini kwake, akijidai ni yatima na ana kipaji cha kuigiza, alipopata mwanya tu, alimliza supastaa huyo ambaye alifariki dunia, Aprili 7, mwaka jana.
Ukiachana na hilo la Kimei ambalo limetajwa na Kapuya, yapo matukio mengine ambayo Felista alishayafanya, ikiwemo kudanganya anasoma alipiwe ada, vitabu, madaftari na sare za shule, kumbe ni ‘gia’ yake ya kupata fedha kwa njia ya udanganyifu.
SIYO MTOTO KABISA
Uchunguzi wa gazeti hili unalo jawabu kuwa kama kuna uongo ambao jamii haipaswi kubisa kukubaliana nao ni huu kwamba Felista ana umri wa miaka 16 na anasoma sekondari.
Gazeti hili limebaini kuwa Felista ni mama wa mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina umri wa miaka 21.”
Waandishi wetu walifika mpaka Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni ambako alidai anasoma, huko kila mwalimu aliyeulizwa alisema: “Hakuna mwanafunzi kama huyo anayesoma hapa labda kama mmechanganya shule.”

Saturday, November 9, 2013

FAINALI ZA MISS UNIVERSE 2013 KUFANYIKA LEO


                                      Miss Universe Tanzania 2013, Betty Omara.

Mashindano ya 62 ya urembo ya Miss Universe yanatarajiwa kufanyika leo usiku  katika Ukumbi wa Crocus City, Krasnogorsk, Moscow nchini Urusi . Olivia Culpo, Miss Universe 2012 kutoka Marekani atamvisha taji mrithi wake atakayeshinda katika shindano hilo litakalowashindanisha warembo kutoka nchi 86. Mwaka huu, Tanzania inawakilishwa na mrembo Betty…

                                      Miss Universe Tanzania 2013, Betty Omara.
Mashindano ya 62 ya urembo ya Miss Universe yanatarajiwa kufanyika leo usiku  katika Ukumbi wa Crocus City, Krasnogorsk, Moscow nchini Urusi . Olivia Culpo, Miss Universe 2012 kutoka Marekani atamvisha taji mrithi wake atakayeshinda katika shindano hilo litakalowashindanisha warembo kutoka nchi 86. Mwaka huu, Tanzania inawakilishwa na mrembo Betty Omara.

Mwendesha Mashtaka auawa Libya

Moja ya matukio ya milipuko ya mabomu yaliyotegwa kwenye gari nchini Libya
Mwendesha Mashtaka Mohammed al Naass ameuawa kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa bandari wa Darna mashariki mwa Libya.
Wakati huo huo polisi wawili wamepigwa risasi katika mji wa Benghazi ambapo ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linasema karibu watu hamsini wameuawa tangu mwaka 2012 katika matukio yanayohusiana na mgogoro wa kisisiasa katika miji miwili iliyopo mashariki.
Pia kumekuwa na hali machafuko katika mji kuu wa Tripoli tangu mwishoni mwa wiki wakati makundi mawili ya wapiganaji yalipopambana kwa kutumia bunduki na silaha nzito nzito na kufanya milio ya makombora kusikika katika baadhi ya maeneo ya mji huo.
Karibu watu kumi wameripotiwa kujeruhiwa katika ghasia hizo.


Taarifa na BBC Swahili

WANAFUNZI MSIKUBALI KUFELI ILA MKIFELI PIA SI TATIZO!


Posted by MPEKUZI MAYNESS on November 8, 2013 at 9:30am 0 Comments 0 Likes
AWALI ya yote ningependa kumshukuru Mungu kwa mengi mema ambayo amekuwa akinitendea katika maisha yangu ya kila siku. Kikubwa zaidi ya vyote nimshukuru kwa kunijaalia uhai, afya njema na nguvu za kutosha kiasi cha kunifanya niweze kutimiza majukumu yangu ya kila siku kama kawaida. Ndugu zangu, wiki hii imeanza vibaya sana kwangu.
Hiyo imetokana na ile taarifa ya yule kijana wa sekondari ya Sabasaba mkoani Iringa ambaye amekutwa amejinyonga kwa madai kuwa alihisi atafeli mtihani wa kidato cha nne unaoendelea nchini.
Kwa mujibu wa ujumbe aliouacha, kijana huyo amesema amekuwa akirudia kufanya mitihani kila wakati lakini anafeli na

kusababisha asifikie malengo yake. Akaenda mbele zaidi na kusema kuwa, anajua wapo watu watamshangaa lakini aliona kujinyonga ndiyo uamuzi…
Soma Zaidi....


MWANAMKE, MWANAUME WAFA WAKIWA WAMEKUMBATIANA!


NA MWANDISHI WETU,GEITA

Watu w a w i l i a m b a o hawakufahamika majina yao, wamefariki dunia papohapo wilayani Bukombe mkoani Geita baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga kisha kugongwa na gari aina ya Noah. Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, ilitokea hivi karibuni ambapo dereva wa bodaboda hiyo alikuwa amembeba mwanamke pamoja na mizigo mingi.
Shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini akisimulia zaidi alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo kilitokana na dereva wa bodaboda aliyekuwa akiendesha kwa kasi kushindwa kuimudu pikipiki yake iliyoteleza kwenye mchanga. “Wakati akipishana na gari pikipiki yake iliteleza kwenye mchanga na kuanguka katikati ya barabara ndipo gari aina ya Noah ambayo namba zake…
NA MWANDISHI WETU,GEITA
Watu w a w i l i a m b a o hawakufahamika majina yao, wamefariki dunia papohapo wilayani Bukombe mkoani Geita baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga kisha kugongwa na gari aina ya Noah. Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, ilitokea hivi karibuni ambapo dereva wa bodaboda hiyo alikuwa amembeba mwanamke pamoja na mizigo mingi.
Shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini akisimulia zaidi alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo kilitokana na dereva wa bodaboda aliyekuwa akiendesha kwa kasi kushindwa kuimudu pikipiki yake iliyoteleza kwenye mchanga. “Wakati akipishana na gari pikipiki yake iliteleza kwenye mchanga na kuanguka katikati ya barabara ndipo gari aina ya Noah ambayo namba zake hazikunaswa aliyokuwa akipishana nayo ikawapitia vichwani na kufa papohapo wakiwa wamekumbatiana,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:“Ni ajali mbaya sana kwani wote wawili wamekufa palepale, mbaya zaidi hawajafahamika ni wakazi wa eneo gani,” alisema shuhuda huyo.

MITUSI MTANDAONI YAMPA UCHIZI SHILOLE

Posted by Mayness on November 8, 2013 at 9:11am 0 Comments 0 Likes
NA IMELDA MTEMA

MMSANII Zuena Mohammed ‘Shilole” ameonekana kupata uchizi kufuatia matusi mazito aliyoporomoshewa

mtandaoni baada ya kuweka picha ya baba wa Wema Sepetu na kuandika R.I.P baada ya kutundika picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instergram akitarajia kuungwa mkono na wadau, wengi walionekana kukerwa na kitendo hicho huku wakimuita mnafiki mkubwa pamoja na maneno mengine makali.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Shilole alisema amesikitishwa sana na kutukanwa na kuonesha kuwa amepata uchizi na kudai kuwa atamshitaki Wema kwani ndiye anayeweza kuwazuia wapambe wake waache kumshambulia. Wema akizungumzia ishu hiyo alisema, anamshangaa Shilole kwani wanaomtukana wala hawajui na kama ana mpango wa kumshitaki atapoteza muda wake…
NA IMELDA MTEMA
MMSANII Zuena Mohammed ‘Shilole” ameonekana kupata uchizi kufuatia matusi mazito aliyoporomoshewa
mtandaoni baada ya kuweka picha ya baba wa Wema Sepetu na kuandika R.I.P baada ya kutundika picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instergram akitarajia kuungwa mkono na wadau, wengi walionekana kukerwa na kitendo hicho huku wakimuita mnafiki mkubwa pamoja na maneno mengine makali.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Shilole alisema amesikitishwa sana na kutukanwa na kuonesha kuwa amepata uchizi na kudai kuwa atamshitaki Wema kwani ndiye anayeweza kuwazuia wapambe wake waache kumshambulia. Wema akizungumzia ishu hiyo alisema, anamshangaa Shilole kwani wanaomtukana wala hawajui na kama ana mpango wa kumshitaki atapoteza muda wake bure.

NDOA YA MIKE, THEA YAVURUGIKA Soma kiundani....

Posted by Mayness on November 8, 2013 at 8:30am 0 Comments 0 Likes
Hamida Hassan na Gladness Mallya

NDOA ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ imevurugika baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili hao chanzo kikidaiwa ni kukosekana uaminifu.
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa, kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato) anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu tulitokea kutoelewana na si mambo…
Hamida Hassan na Gladness Mallya
NDOA ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ imevurugika baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili hao chanzo kikidaiwa ni kukosekana uaminifu.
Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao.
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa, kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato) anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.


Soma kiundani hapa MKE AKUTWA KANYONGWA CHUMBANI

Posted by Mayness on November 8, 2013 at 8:30am 0 Comments 0 Likes
Stori: Brighton Masalu Hna Jelard Lucas

HAMIDA Issa (26), amefariki dunia baada ya kuuawa chumbani kwake. Haijajulikana aliyefanya maujai hayo ila mumewe aitwaye Yahya ametoweka baada ya tukio hilo, Ijumaa lina habari kamili.
Ndugu aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Issa, alisema marehemu Hamida alikumbwa na ukatili huo Jumapili iliyopita nyumbani kwake Kibondemaji Mbagala jijini Dar, lakini mwili wake ukagundulika Jumanne kufuatia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani ya chumba chake.
Rehema alisema ndugu yake alifunga ndoa na Yahya miaka mitatu iliyopita lakini ndoa hiyo ilikuwa ikikumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
“Ugomvi mkubwa ulikuwa ni kuhusu ulevi wa mwanaume jambo ambalo lilikuwa likimkera sana mkewe,” alisema Rehema.…

Stori: Brighton Masalu Hna Jelard Lucas
HAMIDA Issa (26), amefariki dunia baada ya kuuawa chumbani kwake. Haijajulikana aliyefanya maujai hayo ila mumewe aitwaye Yahya ametoweka baada ya tukio hilo, Ijumaa lina habari kamili.
Ndugu aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Issa, alisema marehemu Hamida alikumbwa na ukatili huo Jumapili iliyopita nyumbani kwake Kibondemaji Mbagala jijini Dar, lakini mwili wake ukagundulika Jumanne kufuatia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani ya chumba chake.
Rehema alisema ndugu yake alifunga ndoa na Yahya miaka mitatu iliyopita lakini ndoa hiyo ilikuwa ikikumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
“Ugomvi mkubwa ulikuwa ni kuhusu ulevi wa mwanaume jambo ambalo lilikuwa likimkera sana mkewe,” alisema Rehema.
Ndugu huyo alisema kila alipokuwa anarudi nyumbani amelewa, mwanaume huyo alikuwa akimshushia kipigo mkewe na kumfanya marehemu kupeleka malalamiko yake akachukue vyombo vyake na    alisema mdogo mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni upande wa mwanaume lakini hakukuwa na suluhu yoyote.
“Alipoona anashindwa Hamida akaamua kubadili sehemu ya kusuluhishwa na kuanza kupeleka madai yake nyumbani kwao Tabata Kimanga jijini Dar,” alisema Rehema na kudai kwamba hata huko hawakuweza kutatua migogoro hiyo.
“Baada ya kuona hali haibadi liki, Hamida aliamua kurudi nyumbani huku akidai talaka yake kitu kilichokuwa kigumu kwa mumewe kukikubali,” aliendelea kusema Rehema.
Habari zinadai kuwa siku moja Hamida akiwa kwao, Tabata, mume alitishia kujiua na kumfanya marehemu kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kufunguliwa kumbukumbu ya jalada namba RB TBT/ RB/ 1583/ 2013 TAARIFA.
Pia Hamida alikwenda kutoa taarifa kwenye Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) ili aweze kupewa talaka yake.
“Mumewe aliandikiwa barua ya wito na Bakwata lakini hakwenda.
“Siku moja mwanaume huyo alimpigia simu mkewe na kumwambia anataka kuhamia Sinza kwa hiyo aende nyumbani kwao
vingine wagawane. “Mama yetu (Zaria Munge)alimzuia Hamida kuvifuata vitu hivyo lakini marehemu alilazimisha kwa madai kuwa mumewe akihamia sehemu nyingine itakuwa vigumu kuvipata vyombo vyake,” alisema Rehema.
Inadaiwa kwamba mwanaume huyo alikwenda nyumbani kwa wakwe zake ili akamchukue mkewe wakagawane hivyo vyombo. Kutokana na shaka, marehemu aliamua kumchukua mdo go wake ili wawe wawili.
Habari zinadai Hamida na mumewe walitembea sanjari huku mdogo mtu huyo akitangulia na kwenda kufikia kwa jirani wakati akiwasubiri.
Wawili hao walipofika, mdogo mtu huyo aliwafuata kwa lengo la kuungana nao katika zoezi la kukusanya vyombo lakini sh- emeji yake alikataa na kumtaka abaki nje kisha akafunga mlango kwa ndani.
“Nilipoona shemeji amekataa nisiingie na akafunga mlango niliamua kurudi kwa yule jirani. Mara shemeji akanipigia simu kwa namba ya dada ikisema nirudi nyumbani kwani wao bado wana shughuli maalum,”
baye jina halikupatikana mara moja.
Akiwa njiani, alipigiwa tena simu na shemeji yake huyo akimwambia kuwa muda si mrefu simu zote zitazima chaji lakini asiwe na wasiwasi wowote.
Habari zinasema kuanzia wakati huo hadi saa sita usiku Hamida hakuwa amerudi kwa mama yake, lakini mara Yahya alimpigia simu mdogo huyo wa marehemu akimuulizia kama dada yake ameshafika nyum bani hapo!
“Nikashangaa sana, inakuwaje shemeji aniulize hivyo wakati niliwaacha pamoja baada ya kunizuia kuingia ndani? Kuanzia hapo nikaingiwa na wasiwasi,” alisema.
Asubuhi ya siku ya pili, ndugu wa Hamida walikwenda Mbagala na kutoa taarifa polisi ya kupotelewa na ndugu yao huyo katika mazingira ya kutatanisha, polisi walikataa kutoa ushirikiano ikiwemo kuvunja mlango wa nyumba hiyo ili kujiridhisha ndipo waliondoka huku mioyo yao ikiwa imegu bikwa na wasiwasi.
Jumanne iliyopita mama mzazi alipokea simu kutoka kwa mjumbe wa eneo la Kwamjerumani (ilipo nyumba ya Yahya) na kumtaarifu kuwa kuna harufu kali sana kutokea kwenye nyumba ya Yahya hivyo wafike mara moja kwa ajili ya ukaguzi.
“Simu hiyo ilinishtua sana, nikawataarifu ndugu akiwemo dada wa marehemu, tukaenda,” alisema mama mzazi.
Akaendelea kusema kuwa baada ya kufika mahali hapo, walichukua uamuzi wa kuvunja mlango kwa kupewa ruhusa na mjumbe ambapo chumbani waliukuta mwili wa Hamida ukiwa kitandani.
Marehemu alikuwa ameshindiliwa nguo kinywani na kufungwa kitambaa shingoni huku mwili wake ukiwa ndani ya nailoni ikionekana kuwa unyon-gaji umefanyika.
Baada ya taratibu zote ku fanyika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi.
Marehemu Hamida alizikwa Jumatano iliyopita katika Kijiji cha Mzenga, Bagamoyo, Pwani. Ameacha mtoto wa kike aitwaye Tayana. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panaposta- hiki. Amina.


PENNY AKUBALI KUSHEA PENZI NA WEMA Soma hapa ki undani zaidi

Posted by Mayness on November 8, 2013 at 7:30am 0 Comments 0 Likes


MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
 
 Penny katika pozi na Wema.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliliambia gazeti hili maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye…

MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
 
Penny katika pozi na Wema.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliliambia gazeti hili maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.
 
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Ninampenda Diamond na sitaki kumpoteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha. Kama Diamond anaona kuna msichana mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.
Wema Sepetu 'Madam 'na Peniela Mwingilwa ‘Penny’.
Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.
Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka

MREMBO AKODI CHUMBA GESTI, AINGIZA WANAUME KWA ZAMU USIKU KUCHA


Posted by Mayness  on November 8, 2013 at 7:30am 0 Comments 0 Likes
Stori: Richard Bukos na Issa Mnally

KABANG! Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar kwa kushirikiana na Oparesheni    Fichua

Maovu (OFM) ya Global Publishers wamemnasa mrembo Zuena Mohammed anayedaiwa kukodi chumba cha gesti na kuingiza wa- naume kwa zamu usiku kucha.
Tukio hilo lilijiri chumba namba 14 ndani ya Gesti ya Mori Lodge iliyopo Sinza jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikuwa amekodi chumba hicho na kuwapanga wanaume kwa foleni kwa ajili ya kutoa huduma haramu ya ngono.
AFM Watonywa.

Awali, ‘makachero’ wa OFM walitonywa kuwepo kwa ishu hiyo na chanzo chake kilichodai kuk- erwa na tabia ya mrembo huyo ambaye amekuwa akitishia afya za wanaume wakiwemo vigogo wa serikali ambao ilidaiwa kuwa ni sehemu ya…
Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
KABANG! Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar kwa kushirikiana na Oparesheni    Fichua
Maovu (OFM) ya Global Publishers wamemnasa mrembo Zuena Mohammed anayedaiwa kukodi chumba cha gesti na kuingiza wa- naume kwa zamu usiku kucha.
Tukio hilo lilijiri chumba namba 14 ndani ya Gesti ya Mori Lodge iliyopo Sinza jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikuwa amekodi chumba hicho na kuwapanga wanaume kwa foleni kwa ajili ya kutoa huduma haramu ya ngono.
AFM Watonywa.
Awali, ‘makachero’ wa OFM walitonywa kuwepo kwa ishu hiyo na chanzo chake kilichodai kuk- erwa na tabia ya mrembo huyo ambaye amekuwa akitishia afya za wanaume wakiwemo vigogo wa serikali ambao ilidaiwa kuwa ni sehemu ya wateja wake.
Chanzo: Jamani OFM mpo ka- zini?
OFM: Tumejaa tele leta maneno.
Chanzo: Mimi naitwa (anataja jina) lakini naomba msinitaje. Kuna mrembo mmoja amekodi chumba gesti...yaani anapanga wanaume foleni anagawa dozi ya penzi.
OFM: Hatuwezi kukutaja tuna- heshimu vyanzo vyetu vya habari. Una uhakika na taarifa zako?
Chanzo: Nina uhakika asili- mia zote. Ninyi nendeni pale Mori Lodge maeneo ya Sinza, fanyeni kazi yenu mtapata mkanda kamili.
OFM kazini
Baada ya kupenyezewa ‘tipu’ hiyo, OFM iliingia kazini na ‘kuliteka’ eneo la tukio kwa uchunguzi na kubaini undani wa ufuska huo wa kutisha.
Kabla ya yote ‘memba’ wa OFM alijifanya mmoja wa wanaume waliokuwa wakihitaji huduma ya mrembo huyo hivyo kujipatia data nyingi kabla ya kubadilisha uamuzi baada ya kupata ishu kamili.
Tukio Laivu
Kilichofuata ni kwamba OFM iliwasiliana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ambalo nalo baada ya kupokea taarifa hizo bila kusita lilifika eneo la tukio na kumnasa mrembo huyo akitoa hudumu kwa mwanaume ndani ya chumba hicho.
Katika hali ya sintofahamu, mazingira ndani ya chumba hicho yalionesha kuwa mrembo huyo ni mpangaji wa kudumu ambapo kulikuwa na meza ya kujiremba (dressing table) iliyosheheni mazagazaga ya vipodozi.
Ndani ya chumba hicho kulikutwa kondom zilizotumika na zisizotumika zikiwa zimezagaa sakafuni,
jambo lililothibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo vichafu.
Wanaume Watoka Nduki
Wakati mrembo huyo akinaswa, baadhi ya wanaume waliokuwa wakisubiria huduma yake walitoka nduki huku wachache wakitiwa ko- rokoroni.
Wote    waliokamatwa    katika sekeseke hilo walipelekwa nyuma ya nondo za Mahabusi kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Maba- tini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Aingiza Sh. 200, 000
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, kutokana na jinsi mrembo huyo ‘anavyokula vichwa’ mambo yakimuendea vizuri huweza ku- kusanya hadi shilingi laki mbili (200,000) kwa siku au usiku mmoja.
Wengine Mbaroni
Mbali na mrembo huyo, wengine walionaswa wakijihusisha na bi- ashara haramu ya ngono eneo hilo ni Shakira Thabit na Christina Benard ambao nao walitiwa mbaroni pamoja na wateja wao.
OFM inalipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni na RPC wake, Camillus Wambura kwa kuitikia wito haraka wanapopata taarifa mbalimbali za uhalifu hivyo kupun- guza kasi ya uovu katika maeneo yake.

SIRI ZA KUDUMISHA PENZI LAKO LISITETEREKE! kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi.


Posted by Mayness on November 8, 2013 at 9:17am 0 Comments 0 Likes
NAKUKARIBISHA kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi. Ni imani yangu, umekuwa ukipata maarifa mapya kila siku kupitia hapa. Kaa tayari uvune kitu kipya leo.

Kwanza kabisa, napenda kuchukua  nafasi hii kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia ya simu na kunipongeza, kunikosoa na kuuliza maswali kuhusu mambo mbalimbali yanayowakabili katika uhusiano.
Kufanya kwenu hivyo kunanipa moyo kwamba, ujumbe unawafikia vilivyo. Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Nazungumzia juu ya mambo ya kuzingatia kama unahitaji kudumu katika uhusiano

ulionao.
Hapa naomba nizungumze na wanawake zaidi. Hii haina maana kwamba, wanaume hawahusiki katika mada hii.    Ni ukweli kwamba…
NAKUKARIBISHA kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi. Ni imani yangu, umekuwa ukipata maarifa mapya kila siku kupitia hapa. Kaa tayari uvune kitu kipya leo.

Kwanza kabisa, napenda kuchukua  nafasi hii kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia ya simu na kunipongeza, kunikosoa na kuuliza maswali kuhusu mambo mbalimbali yanayowakabili katika uhusiano.
Kufanya kwenu hivyo kunanipa moyo kwamba, ujumbe unawafikia vilivyo. Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Nazungumzia juu ya mambo ya kuzingatia kama unahitaji kudumu katika uhusiano
ulionao.
Hapa naomba nizungumze na wanawake zaidi. Hii haina maana kwamba, wanaume hawahusiki katika mada hii.    Ni ukweli kwamba wanawake ndiyo wanaokumbana zaidi na matatizoya kuachwa na wapenzi wao kuliko wanaume kuachwa solemba na wenzi wao. Ni sahihi kusema, wanawake ndiyo huumizwa zaidi katika mapenzi kuliko wanaume.

Hii ni kutokana na sababu kubwa mbili; kwa kawaida wao ndiyo hufuatwa na kutongozwa na wanaume, lakini lingine ni kwamba, mara nyingi wanaume ndiyo hutoa uamuzi wa kuacha au kuachana. Kwa sababu hizo, hakuna ubishi kuwa wanawake ndiyo walengwa wakubwa wa mada hii. Rafiki zangu, kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kusababisha uhusiano kuwa butu na baadaye  kuishia njiani. Hapa katika Let’s Talk About Love nitakupa dondoo za kuzingatia ili usiingie kwenye matatizo niliyoeleza hapo juu. Jambo kubwa kabisa ambalo unatakiwa kulifahamu mpenzi msomaji wangu ni kuwa, mwanaume anahitaji kuwa na mwanamke wake ambaye atakuwa kila kitu kwake. Hebu sasa twende tukaone vipengele vyenyewe.

UTAMBUZI WA THAMANI
Ili uweze kuwa bora ni lazima uanzie kwako, ujitambue kama mwa n a - mke na thamani yako kwa mwanaume wako.
Ukiijua thamani yako, lazima utakuwa makini na kila kitu. Rafiki yangu, ninaposema thamani ninamaanisha kwanza kujiamini na kujipa nafasi ya kwanza.
Uamini kwamba wewe ni mwanamke mrembo na unayevutia. Imani hiyo ikishaingia, tayari utakuwa unajali mambo
mengi ya msingi, ikiwemo usafi wako binafsi. Waswahili wanasema, mwanamke ni pambo la nyumba. Pambo haina maana  ya ua, inamaanisha ule usafi wa kila kitu.

Kwamba nyumba bila mwanamke haiwezi kukamilika, wewe kama mwanamke unatakiwa kufahamu wewe ni kila  kitu ndani ya nyumba. Umakini wako na kujitambua ndiyo vitu vitakavyokuweka katika nafasi nzuri ya kudumu katika uhusiano wako na baadaye kuingia katika ndoa.

TAMBUA THAMANI YAKE
Ukiijua thamani ya mwanaume kutoka ndani ya moyo wako ni wazi kwamba hata vipengele vifuatavyo hapa chini havitakuwa vigumu kwako kutekelezeka. Inakupasa ujue thamani ya mwanaume wako.
Hilo si tu kwa maneno, bali ni jambo ambalo litatakiwa kufanyika kwa ridhaa ya moyo wako. Ni rahisi zaidi jambo hili kufanyika ikiwa utakuwa na mapenzi ya dhati. Mpende kwa moyo wako wote na ujue kuwa maisha yako yanakamilishwa  na uwepo wake. Ndiyo! Yanakamilishwa na uwepo wake, maana una mategemeo ya kuingia katika ndoa naye. Hapo mtakuwa mwili mmoja na maisha ya kila mmoja yatamtegemea mwenzake. Bado kuna vitu vya kujifunza zaidi. Wiki ijayo tutaendelea. Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vitatu; True Love, Let’s, Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

Makubaliano na Iran kuhusu Nuklia yanukia:Waziri wa mambo ya nje wa Iran, amesema kuwa anaamini makubaliano kuhusu mpango wake wa Nuklia yataafikiwa mwishoni mwa Ijumaa.







Maungumzo kuhusu mpango wa Nuklia wa Iran mjini Geneva
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, amesema kuwa anaamini makubaliano kuhusu mpango wake wa Nuklia yataafikiwa mwishoni mwa Ijumaa.
Mohammad Zarif ameambia CNN kuwa Iran haitasitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium kabisa lakini inaweza kujizuia naa baadhi ya maswala yanayozungumziwa.
Nchi za magharibi hata hivyo hazikuzungumzia hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo mjini Geneva.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ambaye anazuru Mashariki ya Kati, anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo siku ya Ijumaa.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye msafara wa Bwana Kerry, anasema kuwa uamuzi wake kubadili mipango yake ya safari nchini Saudi Arabia na kwenda Geneva, ni dalili tosha kuwa mkataba huenda ukaafikiwa kati na Iran
Mnamo siku ya Alhamisi, Marekani ilithibitisha kuwa baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran vitalegezwa ikiwa Iran itachukua hatua muhimu na ambazo zinaweza kuthibitishwa katika mpango wake wa nuklia.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema kuwa ikiwa mkataba utafikiwa litakuwa kosa la kihistoria na kuituhumu Iran kwa kutokuwa mkweli.
Wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ujerumani , walikutana kwa mazungumzo kuhusu Iran siku ya Alhamisi mjini Geneva.
Nchi za Magharibi zinashuku kuwa mpango wa Iran wa kurutubisha madini ya Uranium ni hatua ya kutaka kujenga zana za nuklia.

Na BBC Swahili

KIPA wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ amesema kuwa ataendelea kujituma ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kwa kuwa anaamini huu ndiyo muda wake wa kujituma.


Dida: Huu ndiyo wakati wangu Yanga

Deogratius Munishi ‘Dida’.



Dida ambaye ametua Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam amefanikiwa kudaka mechi tatu za mwisho za Yanga bila kuruhusu bao kabla ya mechi za jana huku akionyesha kiwango kizuri.
“Kila mtu ana muda wake wa kuonekana kwa hiyo nadhani zamu yangu imefika sasa ya kuonekana Yanga lakini ikifika wakati wa mtu mwingine na mimi pia nitakaa benchi, anaweza (Ally Mustapha) Barthez akarudi golini au akaja mwingine akatupiku,” alisema Dida.
Dida…
Deogratius Munishi ‘Dida’.

KIPA wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ amesema kuwa ataendelea kujituma ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kwa kuwa anaamini huu ndiyo muda wake wa kujituma.
Dida ambaye ametua Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam amefanikiwa kudaka mechi tatu za mwisho za Yanga bila kuruhusu bao kabla ya mechi za jana huku akionyesha kiwango kizuri.
“Kila mtu ana muda wake wa kuonekana kwa hiyo nadhani zamu yangu imefika sasa ya kuonekana Yanga lakini ikifika wakati wa mtu mwingine na mimi pia nitakaa benchi, anaweza (Ally Mustapha) Barthez akarudi golini au akaja mwingine akatupiku,” alisema Dida.
Dida alikuwa chaguo la pili kikosini hapo, lakini mara baada ya mechi ya Simba iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3, Barthez aliyekuwa chaguo la kwanza alianza kuwekwa benchi.

Soma kiundani zaidi magazeti ya leo Ijumaa ya tarehe 8/11/2013. Bahanuzi atangaza tarehe ya kuihama Yanga. MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amesema ataendelea kujituma

 
Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi.


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amesema ataendelea kujituma katika kikosi hicho, lakini kwa mara ya kwanza akazungumzia juu ya muda ambao ataihama timu hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bahanuzi ambaye ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, alisema hana wasiwasi juu ya uwezo wake, lakini kama ataendelea kukosa nafasi, ataikimbia klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Bahanuzi ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora katika timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Kagame misimu miwili iliyopita, amesema hawezi kuvumilia kukaa nje wakati anaamini bado uwezo wa kuitumikia Yanga anao.

“Kazi yangu ni mpira, ili niendelee kutumia kipaji changu, natakiwa kucheza katika mechi, nafurahi kuwa hapa lakini sifurahii kuwa nje, naamini uwezo wangu, nitavumilia kwa kujituma zaidi mazoezini, ikitokea hali ikazidi kuendelea, nafikiri naweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu,” alisema Bahanuzi aliyetua Yanga akitokea Mtibwa Sugar.

Hapo jana. Ajali mbaya Sinza iliyo usisha Bodaboda


AJALI MBAYA SINZA


Watu wakishangaa ajali hiyo.
               Wasamaria wema wakijitolea kumpakiza kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali.

Dereva wa bodaboda akiitetea roho yake mara baada ya kugongwa na gari maeneo ya Sinza Afrikasana.

Watu wakishangaa ajali hiyo.
               Wasamaria wema wakijitolea kumpakiza kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali.
Dereva wa bodaboda akiitetea roho yake mara baada ya kugongwa na gari maeneo ya Sinza Afrikasana.

Friday, November 8, 2013

WANAFUNZI WAWILI WA CBE WAPATA AJALI MBAYA YA PIKIPIKI NA KUFARIKI MKOANI DODOMA‏

 Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
 Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani hapo.



 
 Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Dodoma.
 Asikari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.


Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara  wamepoteza  CBE wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo  yenye namba za usajili T 420 CCN  waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE  na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo  na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.