Thursday, November 27, 2014

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO: MASWALI KWA WAZIRI MKUU


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
KIKAO cha Bunge leo kimeanza kwa maswali kwa Waziri Mkuu ambapo aliyekuwa wa kwanza kuuliza alikuwa ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
Alianza Mbowe: 
“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa…

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

KIKAO cha Bunge leo kimeanza kwa maswali kwa Waziri Mkuu ambapo aliyekuwa wa kwanza kuuliza alikuwa ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
Alianza Mbowe: 
“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungeni, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“
Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Akaunti ya Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Nguvu za Wanaume kuwatesa wanawake



1.       Mwanaume ana nguvu ya kumpenda mwanamke katika njia yoyote ambayo hajawahi kupendwa na lakini kumuumiza katika njia ile ile


2.       Mwanaume ana nguvu kumjali mwanamke kama marikia kisha kumgeuza nyuma na kumfanya ajihisi kama angekua hajazaliwa
3.       Mwanaume ana nguvu ya kumfanya mwanamke akalia kwa furaha na pia kumgeuza nyuma na kumfanya akalia kwa maumivu na hasira
4.       Mwanaume ananguvu ya kumfanya mwanamke kujiona huru na pia kumfanya kuchukia na kujiona asiye faa.
5.       Mwanaume ananguvu ya kumwangalia mwamke usoni na kumwambia anampenda lakini wakati huo huo anageuka na kulala na rafiki wa karibu wa mwanamke huyo
6.       Mwanaume ananguvu yakumfanya mwanamke akampenda ndani ya siku moja na kumfanya mwanamke amchukie ndani ya dakika moja

Kwa nini wanaume wananguvu hizo?
1.       Wananguvu nyingi kwasababu tunawapa nguvu hizo Mfano: Asilimia kubwa ya wanawake wanapoingia kwenye mahusiano huwaza mbali (Kuoana) Lakini wanaume wao hujaribu tu.
2.       Nguvu za mwanaume si chochote bila mwanamke ingawa wengi wao hujiona wao wako sahihi kuliko.
3.       Kwahiyo ndugu zangu kama unawakati mgumu kati yako na mwanaume wako na umetambua anakutendea vibaya kumbuka kuwa anafanya kile ambacho umekiruhusu

Lakini katika yote tunatakiwa kukumbuka tu Mwenyezi Mungu ameshatuandalia watu sahihi wakuishi nao hivyo tunatakiwa kuwa makini na kujipa moyo kwani mtu sahihi yupo na huja kwa wakati. Hakuna kuumia sana katika hili tunachotakiwa kufanya ni kuyakabidhi mahusiano yetu kwa Mungu.

Thursday, October 23, 2014

SABABU ZINAZOPELEKEA WATU KUWA WALEVI, NJIA ZA KUACHA ULEVI NA MADHARA YATOKANAYO NA ULEVI

Asilimia kubwa ya watu hasa vijana tunafikiri pombe ni kiburudisho cha kutufanya tusahau matatizo yetu. Watu wengi huita pombe mfariji kwani akishapata kilevi hujiona kama kila kitu kwake ni rahisi na kujiona yeye anaweza kila kitu na husahau mambo na shida zake kwa muda mfupi kabla Pombe zake hazijaisha kichwani. Leo nimependa kuzungumzia kidogo maswala ya ulevi kifupi labda yanaweza kutusaidi mimi  na wewe pia.


SABABU ZINAZOPELEKEA WATU KUJIUNGA KATIKA ULEVI/KUWA WALEVI
Kama tunavyo fahamu asilimia kubwa ya watu wanajifunza kunywa pombe ukubwani kutokana na mambo ambayo yamewakuta katika kipindi hicho. Ninaamini hakuna mtu aliyezaliwa na pombe. Leo nitaeleza sababu chache zinazowafanya watu wengi kujiingiza katika maswala ya ulevi/kutumia vileo
  1. Mapenzi - Hili ni swala kubwa lakini kiufupi mapenzi yakienda kombo huwa yana athiri sana Saikorojia ya mtu na kumsababishia mtu kujiingiza katika maswala yasiyofaa kama vile ulevi. 
  2. Umaskini/Hali ya kukosa mahitaji yake ya kila siku - Mtu wa aina hii anaweza kushawishika kutumia vilevi kutokana na ugumu wa maisha yake na kukata tamaa na kujiona hana thamani tena zaidi kushinda akiwa amelewa kila siku.
  3. Urafiki na watu walevi - Marafiki ni watu wakubwa katika maisha yetu na siku zote huwa chanzo cha kubadili maisha yetu eitha kuyaharibu au kuyajenga, inategemeana upo na rafiki wa dizaini gani na mnashauliana vipi. Huwezi kila siku kuambatana na mlevi kama wewe si mlevi.
  4. Matatizo ya kifamilia/Matatizo katika ndoa - Hii inaweza kuwa sababu ya watu kujiingiza katika kilevi mfano mtu anaweza kuwa ameoa/kaolewa na mtu ambaye hakuwa chaguo lake au alilazimisha mahusiano mwisho wa siku anajikuta mtu wa kujuta kila siku. Tunaamini ndoa ni Paradiso ndogo kama tu tutafanya matwakwa yake na kujua nini maana ya ndoa. Lakini endapo ndoa yako itakua na doa utajikuta huna furaha na kuona Pombe yaweza kuwa faraja yako. Nimeshuhudia watu wengi wakijiingiza katika ulevi hata watoto wadogo ukiuliza sababu anakwambia kuwa nyumbani wazee wanazingua mfano anasoma akifeli kidogo mzazi/mlezi anakosa busara za kuongea nae katika hali nzuri anakua akimfokea na kumsemea maneno mabaya ndipo mtoto huyo anafikili pombe yaweza kuwa mfariji wake.
  5. Msongo wa Mawazo - Kipindi kilichopita nimeshaelezea sana msongo wa mawazo hii pia inachangia kwa nafasi mtu akiwa hana furaha hana amani mawazo kila kukicha anajikuta anatamani aingie katika ulevi ili asahau shida zake

NJIA ZA KUACHANA NA ULEVI
TAFUTA KITU CHA KUKUWEKA BUSY MUDA ULIOKUWA UNAFIKILI KWENDA KULEWA 
Watu wengi wanafikiri na kuhisi kuwa ni ngumu kuacha pombe la hasha si kweli endapo utatafuta kitu mbada cha kufanya kwa kipindi kile ulichokua unafikiria kwenda kunywa pombe utaacha kabisa, kama kucheza mpira, kufanya mazoezi, kusoma vitabu vya hadidhi mbalimbali, kuangalia moves hata kusikiliza mziki. Au jaribu kufikiri kitu gani unapenda sana kufanya ukifanya hivyo itakusaidia.

EPUKA MARAFIKI WALEVI
Sina maana usiwe na marafiki hapana unaweza kuwa hata na rafiki mlevi lakini wewe ukawa hutumii kilevi chochote. Tengeneza mazingira mazuri na marafiki zako ili tu wasijekushawishi ukaingia katika ulevi. Epuka kwenda nao sehemu za vilevi kwani wanauwezo mkubwa wakukushawishi nawe ukajikuta umeingia kwenye dimbwi hilo.

USIKAE NA MAMBO YANAYO KUUMIZA KICHWA 
Hapa ninamaanisha hushahiri kukaa na kufikiri matatizo ambayo unaweza kuyatatua kivyovyote. Kuna wakati mwingine mtu anaweza kuwa kakosana na mmoja wa familia yake hafikiri kukaa chini wakazungumza ili tu kupata suruhu yeye anaanza kuweka mambo kichwa na kuumia sana hii haitakiwi hata kidogo kwani inaweza ikakufanya urudi ulikotoka.

EPUKA MITOKO ISIYO YA LAZIMA
Unaweza kualikwa na watu kwenda mazingira ambayo yanavilevi na wao wakiwa watumiaji ni bora kuahirisha kutoka nao ili usije kushawishika

MADHARA YATOKANAYO NA ULEVI 
Madhara ya Ulevi ni mengi lakini kwa leo ntajaribu kuandika machache tu bila shaka yatakusaidia katika maisha yako na utajifunza kitu.
  1. Akili inalala kwani hutaweza kufikiri na akili itakua imeathirika ki Saikologia
  2. Vidonda vya tumbo.
  3. Kansa ya utumbo.
  4. Kansa ya Ini.
  5. Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni.
  6. Kisukari. 
  7. pungufu wa nguvu za kiume.
  8. Kukosa hamu ya kula.
  9. Magonjwa ya moyo.
  10. Heshima kushuka kwa watu wanao kuzunguka.
  11. Unapoteza kujiamini
HAYA NI BAADHI TU YA MAMBO YA ULEVI. ANGALIZO KWA WOTE POMBE SI CHAKULA KWAMBA UKIACHA UTAKUFA NJAA. KAMA BADO UNAPENDA KUENDELEA KUISHI NA UNATAKIWA KUCHUKUA HATUA POMBE SI NZURI KWA AFYA ACHA KABISA.

Tuesday, October 21, 2014

Mahusiano ni jambo ambalo linachukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku. Ukiwa na mahusiano mazuri na mwenzi wako unajiweka katika mazingira mazuri ya kufanya shughuli zako mbalimbali. Leo ninapenda kuzungumzia mambo machache katika mahusiano ikiwa ni pamoja na Jinsi ya kudumisha mahusiano ya mbali, Nini Mwanaume/Mwanamke anapenda kufanyiwa, Mambo yanayopelekea watu kuvunja mahusiano na Heri kuvunja uhusiano ukigundua haya.



JINSI YA KUDUMISHA UHUSIANO WA MBALI.
Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa.
Hata hivyo, mapenzi ya mbali huwa ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na wakati mwingine mmoja wapo anaweza kutafuta nafasi na kwenda kumsabahi mwenzi wake japo kwa siku chache, au  kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama anakofanyia kazi laazizi na mwandani wake
Pamoja na hayo yote bado umbali hauwezi kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na mpenzi wako. Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo
utafanya haya:-

1. MAWASILIANO MARA KWA MARA.
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Jitahidi kila unapo amka asubuhi kumjulia hali umpendae, kuna baadhi ya watu hasa sisi kina dada tunasubili mpaka tutafutwe sisi na si sisi kuanza kuwajulia hali wenzi wetu, hapo tunakosea sana kwani katika mahusiano kila mmoja anajukum la kuhakikisha anamfanya mwenzi wake awe na furaha na kuzidisha upendo hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.
Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe. Maana ukikaa kimya unampa wakati mgumu na inaweza kuwa chanzo cha malumbano.

2. HESHIMU HISIA ZAKO:
Heshima ni kitu cha bure na heshima humfanya mtu akaheshimika zaidi. Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.
Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake lakini sio ule wakubomoa! Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.

Mambo hayo machache yanaweza kukufanya ukadumisha mapenzi yako na mpenzi aliyeko mbali na hatimaye kufikia malengo yenu.

MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAMKE HUPENDA KUFANYIWA NA MWENZI WAKE
  1. Jamani ukweli ni nguzo tosha ya mahusiano. Hakuna mwanamke anayependa kudanganywa nikiwa mmoja wapo. Ingawa naume wengi wanadai wasipotudanganya inakua ngumu kutupata ila wanakosea sana.
  2. Wanawake wengi tunapenda kuwa na wapenzi wetu muda mwingi kuliko hata marafiki zetu.
  3. Mwanamke hupenda mwanaume anaejali zaidi kuliko mbabaishaji 
  4. Wanawake tunapenda kusifiwa. Msifie mwenzi wako pale anapokua kapendeza sio mpaka akuulize "Eti baby nimependeza" Ukifanya hivyo atahamia kwa wale wanaomjali na kumsifia
  5. Mwanamke anapenda kuthaminiwa na mpenzi wake, hata ukiwa na watu wengi, onyesha unajali kuwa nae karibu, hujiona wa pekee
  6. Mwanamke hupenda kusikilizwa japokuwa wanaume hujifanya vichwa na kutuona hatuna la kuongea lakini sio kweli ni fikra zenu tu. Msikilize mpenzi wako uone kama na wewe hatokusikiliza.
  7. Mwanamke anapenda mpenzi wake akumbuke mambo muhimu ambayo amemwambia mfano tarehe ya kuzaliwa. Binafsi hapa naweza kuwa zaidi nafurahi sana mwenzi wangu anapokumbuka tarehe yangu ya kuzaliwa na kukumbuka japo kuniimbia najisikia burudani starehe. Ingawa hata sisi pia tunatakiwa kukumbuka tarehe ya kuzaliwa na mambo muhimu tunayoambiwa na wenzi wetu
  8. Mwanamke huthamini sana msg za mpenzi wake kuliko simu apigiwayo na mwenza wake, maana kuona faraja zaidi pindi asomapo msg hizo zaidi ya kupoteza muda kusubiri apigiwe au akupigie.
  9. Mwanamke hapendi kukalipiwa hata kama kakosea. Jitahidi umwite kwa upole umwambie kama amekosea na umrekebishe sio kuanza kumropokea hata mbele za watu.
  10. Mkumbuke kila wakati hata mara 2 kwa siku hata kama umetigwa jitahidi walau asubuhi ukiwa hujaanza shughuri zako na jioni pia ukimaliza shughuri zako.
  11. Punguza jeuri na kauli chafu kwa mwenzi wako.
Hayo yakizingatiwa utaona kama mwanamke anaweza kukufanyia lolote baya. Wanaume wengi wanapenda kuwachezea akili wanawake hasa pale watakapojua kuwa mwanamke huyo anampenda kutoka moyoni. Jitahidi kuwa na mapenzi ya dhati hasa kwa mwanamke anayeonesha kukujali.

MAMBO AMBAYO MWANAUME ANAPENDA KUFANYIWA
  1. Heshima, mwaume anapenda sana mwanamke amweshimu hapo anaona kama amefika mbingu ya pili. Wewe mwanamke unayekaa hata ujawahi kuitika vizuri kwa mpenzi wako utampoteza wenzio wakamdake mana kuna wanawake wengine hata wakiitwa utasikia anaitika "Nini" au "Unasemaje". Hizo sio kauli nzuri hebu jitahidi kumweshimu mwenzi wako kwa kila kitu.
  2. Jamani wanawake wenzangu mwanaume ni kama mtoto mdogo anapenda ahudumiwe vizuri na kujaliwa pia. Lakini msizidi sana mana wanaume wengine wakisikia hivyo sasa wanataka hadi mikono wanawishwe sina maana hiyo lakini tunatakiwa kuwajali na kuwatunza vyema pale panapobidi
  3. Wanaume wengi hawapendi kufuatiliwa katika maisha yao ingawa sio wote lakini kuna baadhi. Wanawake nasi mda mwingine tunakua na gubuza mala kidogo uko wapi na nani unafanya nini wanaume wengi hawapendi mambo hayo
  4. Pekupeku kwa simu zao. Wanaume wengi hawapendi wapenzi wao wawe wanapekua pekua simu zao za mkononi japo kuwa wao ndo kwanza kimbelembele kupekua simu zetu. Mi humo simo.
 MAMBO YANAYOPELEKEA WATU KUVUNJA MAHUSIANO
Kuna mambo mengi sana yanayopelekea mahusiano kuvunjika, endapo tu wampenzi watashindwa kujizuia na kuyakwepa  katika mahusiano yao
  • Uongo ulio kithili. Hatukatai kwenye mapenzi kunakudanganyana lakini uongo ukizidi mahusiano mengi huvunjika.
  • Wivu, kunawatu wanawivu jamani mpaka basi akimkuta mwenzi wake amesimama na mtu au hata kaenda kutembelewa nyumbani ye tatizo. Mi ninaamini mtu mwenye wivu sikuzote hajiamini kwanini usijiamini kama upo pekeako kwa mpenzi wako? Wivu unachangia sana watu kuvunja mahusiano.
  • Ku cheat, Kutobaki njia kuu kunasababisha sana mahusiano mengi kuvunjiaka mana mmoja wa wapenzi akigundua mwenzake anatoka hawezi kuvumilia kuendelea kuwa nae katika mahusiano.
  • Matumizi mabaya ya simu za mikononi na Mitandao ya kijamii vinachangia sana kuvunja mahusiano. unaweza kukuta mtu yupo na mpenzi wake lakini simu haiishi kuingia sms au kupigiwa na watu wasio na mana. Na kunawakati mwingine mwingine yupo na mpenzi wake lakini simu ndo kaikumbatia anachati mda wote sijui Whatsapp, Twitter,  Facebook na mitandao mingine ya kijamii. Hapo lazima umboe uliye naye hata ningekua mimi.
  • Marumbano na Migogolo ya mala kwa mala kugombana kwa wapenzi mala kwa mala kunakatisha sana tamaa ya kuendelea na mahusiano.
  • Kuzungumzia mahusiano yaliyopita. Jamani kunawatu wanakela ukikaa nae ye ndo kumwaga sifa tu za mpenzi wake wa zamani. Utasikia tulipendana mala alikua ananifanyia hivi hee jamani ye sio yeye kila mmoja anayake huwezi kufanyiwa kama alivyokua anakufanyia aliyepita. Kwani hadi mkaanza mahusiano si mlishasimuliana sasa kila siku gubu hilo hilo jamani inakera sana kusikia sifa za yule tu kila siku mie utanisifia lini. Au kuongelea mabaya ya aliyepita kila siku inakera jamani
Nimeandika baadhi tu ya mambo kwani hata mimi ni binadamu ninasahau pia lakini ukijitahidi kuyakwepa hayo utadumu na mwenzi wako milele


 UKIGUNDUA MAMBO HAYA NI BORA KUVUNJA MAHUSIANO
Kuna wakati tunakua kwenye mahusiano na watu ambao si sahihi kwetu: Hapa nakutajia mambo machache ambayo ukigundua ni bora kuvunja mahusiano kabisa.
1. Kama umefanya uchaguzi usio sahihi. Kunawakati tunakurupuka kuingia kwenye mahusiano eitha baada ya uachana na wapenzi wetu, au tukiwa tayari kwenye msongo wa mawazo.
2. Dini zetu, kama upo kwenye mahusiano na mtu wa Dini tofauti na wewe na mkashindwa kufika muafaka wa nini kifanyike ni bora kusitisha mahusiano yenu.
3. Kukosa Uaminifu (Ku cheat) ni bora kuvunja mahusiano iwapo utagundua mwenzi wako anatoka nje ya mahusiano yenu.
4. Kuwa na tamaa ya maisha makubwa tofauti na uwezo hii hasa inatugusa sisi wanawake kwani wengi hawana mapenzi na wanapenda mali hivyo ukiona upo katika mahusiano hayo ni bora kusitisha mapema kabla hamjafikia maamuzi magumu ya kuishi pamoja.
5. Uchumba wa mda mrefu, kuwa na mchumba kwa muda mrefu bila ndoa ni bora kuvunja mahusiano kwani Mungu atakua hakupanga ninyi muishi pamoja.

Vijana wenzangu ambao bado hamjaoa wala kuolewa twapaswa Kujitambua kwanza kabla hatujaamua kufanya maamuzi ya kutafuta wenza wa kuishi nao. Haya ni baadhi ya mambo tu lakini kila kitu bila kumshirikisha Mwenyezi Mungu haziendi kwahiyo kwa kila tunachokifanya hata tunapofikilia kuanzisha mahusiano mapya tumshirikishe Mungu kwanza mambo mengine yatafuata kwani kwake hakuna linalo shindikana. Twayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.

Wednesday, September 24, 2014

Mwanamziki Chipukizi Tel Omaino arecord wimbo wake wa kwanza wa video unaoitwa BADO NIPO NAYE


Mwana Mziki chipukizi Tel Omaino mkazi wa Tunduru - Songea, Amerecord wimbo wake wa kwanza wa video unaoenda kwa jina la "BADO NIPO NAYE" amemshirikisha Mwanamziki Kauye wimbo huo unatarajiwa kutoka hivi karibu. 

Alipoongea na chanzo chetu alijaribu kueleza historia yake kwa ufupi, Tel Omaino amesoma secondary Lutengano iliyopo jijini Mbeya na kwasasa ni mwanafunzi wa chuo Mtwara. alianza kufanya muziki tangu akiwa secondary, hii ndio nyimbo yake ya kwanza  kuifanyia video. Hata hivyo hakua tayari kutaja umri wake.

Video hiyo Imefanyika katika Studio za 29 Records na Producer Suly, na Video director ni Timmy San jijini Dar es Salaam. Hivyo anawaomba wadau wa mziki kumpa support kubwa mala tu atakapo zindua wimbo wake huo wa kwanza.

 Mwana Musiki chipukizi Tel Omaino katika Poz


 Baadhi ya Vipande katika Video hiyo


  Tel Omaino (Kushoto) na Kauye (Kulia) katika baadhi ya kipande katika video hiyo

  Tel Omaino (Kushoto) na Kauye (Kulia)

 Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

Tel Omaino na Kauye wakipeana salam katika video hiyo

 Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

 Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

 Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande katika Video 

  Baadhi ya Vipande

  Kauye aliyeshirikishwa katika video hii

  Baadhi ya Vipande 

  Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande katika Video hiyo

  Baadhi ya Vipande


Kauye akiimba katika kipande chake


Friday, August 29, 2014

Patrick Ole Sosopi Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA (Baraza la Vijana Chadema) awaomba watu wampigie kura

Patrick Ole Sosopi ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA (Baraza la Vijana Chadema). Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi mbalimbali vya maisha yake. Historia yake ya uongozi ni kuanzia akiwa Elimu ya Sekondari mpaka Chuo Kikuu.

Patrick Ole Sosopi. Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani. Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). 

Ni mpenda maendeleo na amekua mstari wa mbele kutetea ukombozi wa Taifa letu. Akielezea historia yake kwa ufupi Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na watu wote kwa ujumla na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.


Patrick Ole Sosopi ni mojawapo wa waanzilishi wa Chadema Students Organizati (CHASO) mkoani Iringa,  Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja na Mbeya. Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara. Hivyo anaomba kula zako wewe Mtanzania ili kuleta mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu. Uchaguzi unategemewa kufanyika tarehe 10/9/2014 Dar es salaam Makao makuu ya Chama.



 Partick Ole Sosopi akihutubia Wananchi wa Iringa Mjini




 Alipokuwa kwenye uchaguzi wa Kalenga Mwanzoni mwa mwaka huu

 Akihutubia wananchi wa Wilaya ya Kilolo
 Akiwa katika Jimbo lake la Isamani kama Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo hilo.


 Akiwa Pawaga na wadau wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

 

Monday, August 18, 2014

Man U yaanza ligi kwa kichapo


Wachezajii wa Manchester United wakitoka kwa huzuni baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka Swansea
Manchester United imeanza vibaya katika msimu huu wa ligi kuu ya England baada ya kukubali kichapo cha magoli 2 - 1 dhidi ya Swansea.
Swansea ndio waliokuwa kwanza kuandika bao katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza bao lilofungwa na Ki Sung Yueng.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Manchester United walikuwa nyuma kwa bao 1 - 0.
Baada ya kutoka mapunziko Man U walionekana kuja kwa kasi ambapo walilishambulia lango la Swansea mara mara na ndipo katika dakika ya 53 Nahodha mpya wa timu hiyo Wayne Rooney akafanikiwa kusawazisha goli kwa kuunganisha mpira wa kona.
Hata hivyo kama vile waswahili wasemavyo siku ya kufa nyani miti yote huteleza, dakika ya 72 Gyfi Sigurdsson wa Swansea baada ya walinzi wa Manchester United kujichanganya alipigilia msumari wa moto kwenye kidonda na kuandika bao la ushindi kwa Swansea na hivyo kufanya hadi mechi inamalizika Manchester United ikawa imefungwa 2 - 1.

Chanzo  BBC Swahili

MKE WA MTU AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO, KISA NI MUME WA MTU


Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
My God! Mke wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.
 Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa…
Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
My God! Mke wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.


Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini hapa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.


Mama mdogo wa Mwajuma Prima akimuuguza mwanaye.
“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?
“Mabishano yalishika kasi na mwishowe walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa, akaingia jikoni na kuipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka na kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.


 Mume wa Mwajuma Prima akiwa na mama mdogo wa mwajuma.
Akizungumza na gazeti hili, mama mdogo wa Mwajuma alisema: “Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana.
“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia jikoni akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia mwanangu mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”

Soma magazeti ya leo Jumatatu ya tarehe 18 Agosti 2014. DIAMOND, WEMA MWISHO UMEFIKA

Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya
Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Suala la…
Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya
Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala la Wema kukashifiwa liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Wema wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa Instagram kwamba ni kwa nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno jukwaani (hivi karibuni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya kumfungulia biashara ya maana?
“Tujaribuni kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu Diamond. Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno namna ile kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye ni mfuasi wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa kumshauri ‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonesha Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata mauno jukwaani kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.
WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau hao walimtaka Wema kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy Sumari (2005), Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi kwa jinsi wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza kuendesha maisha yao bila kudhalilishwa majukwaani.
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata mauno.
DIAMOND AWAJIBU
Baada ya wadau hao kumshauri Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo walidai yanamdhalilisha, kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond alishindwa kuvumilia ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka wake unaodaiwa kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond alieleza kwamba yeye kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu kama mpenzi wake na suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.
WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri ningewaona kweli mna akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu (Wema) kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe, mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. “Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo anatakiwa aamue kunywa maji!
Aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda.
“Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu, nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”
WAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya waraka huo, mashabiki na wadau waliopo kwenye mtandao huo walimgeukia Diamond kwa kumlaumu kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona amemfungulia dada yake Esma Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa akimtumia tu bila faida yoyote?
MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana na waraka huo, aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika wa kwake na kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.
MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada ya meneja huyo kubwanga manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na penzi hilo la mwanaye ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha hivyo anaacha ‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.
Mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu
“Jamani sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao wazungushane wee mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo imemchanganya.
TUJIKUMBUSHE
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.