Pilau ni Chakula kitam sana na chenye mvuto wa mwonekano wake hasa kikipabwa kwa vitu tofauti tofauti. Kama Karoti, Hoho, Njegere na hata Nyanya pia.
Leo tutapika Pilau la Nyama ya Ngombe kwanza unatakiwa kuandaa vitu vifuatavyo.
MAHITAJI
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Pilipili boga 1 kubwa
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Ndimu1
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Hatua:
- Chemsha nyama yako mpaka iive, uwe umeweka chumvi kiasi, hakikisha nyama ina supu ya kutosha wakati wa kuichemsha
- Osha mchele wako tayari kwa kuutumia na kisha utenge pembeni
- Weka sufuria jikoni, kisha ongeza mafuta. Yakisha pata moto weka vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kuaanga viive. Ongeza chumvi kiasi na endelea kukoroga
- Ongeza vitunguu swaumu vilivyopondwa na endelea kukoroga, koroga mpaka vitunguu vigeuke kuwa rangi ya kahawia na kuiva
- Ongeza viazi ulaya, vilivyomenywa na kukatwakatwa kwa ukubwa uupendao, endelea kukoroga ili vipate kuiva
- Supu uliyochemshia nyama itakua inaonekana hivi baada ya kuondoa nyama. Yaonekana tamu kunyweka ila usiinywe inahusika sana kwenye pishi letu
- Weka mchele wako uliokwisha kuuosha jikoni kisha endelea kuchanganya ili viungo vichanganyike vyema
- Weka supu ya ya nyama kisha endelea kuchanganya
- Weka viungo vya unga na Endelea kuchanganya kwa mda kidogo ili mchanyanyiko wa viungo uchanganyikane vizuri
- Funika Chakula chako kwa daki kadhaa ili kichemke vyema
Maji yakisha kauka geuza chakula ili kichanganyikane vizuri tayari kwa kupakua
Pakua chakula kwenye chombo kwa aajili ya kuandaa mezani
Unaweza kupamba chakula chako kwa vitu tofauti ulivyo andaa kama vile Nyanya, Hoho, Mbogamboga au Karoti.
Chakula tayari kwa kuliwa
pilau nzuri ila hukusema nyanya unaweka wakati gani na hoho
ReplyDeleteSoma vizuri bwana nimeelekeza sema hoho unaweza hata kusubiri mwishon kwa wale wasiopenda ilainike na wanapenda kusikia harufu yake na kuona ukijani unawza hata kuiweka badae sana itabaki juu ili ibaki na rangi yake na harufu yake nzur
DeleteNashkuru sana kwa msaada wako. Nimepata 'idea ya kupika pilau kwa ajili ya week end hii, pia nijumuike na family. Mwenyeezi mungu akulipe kwa hilo.
ReplyDeleteAhsante pia kwa kusoma mama Abdulrahman Endelea kusoma na kutoa maoni pale inapobid ahsante sana
Deletekizito unasema pilau nzuri sana kama umesaionja vile,
ReplyDeleteTunajifunza mengi..Mungu akulipe
ReplyDeleteShukran sana. Nimefuata haya maagizo na ukweli ni kwamba, nimetengeneza Pilau tamu sana. Mungu akubariki na uendelee kutupa 'recipe' zingine kama hizi. Baraka tele.
ReplyDeletehahaha pia mimi sikuona mahali nyanya na hoho huekewa but i now know where to start
ReplyDeleteDah pilau tamu sana
ReplyDeleteNyanya umeweka mda gani et
ReplyDeletenyanya sjaona
ReplyDelete