Sunday, November 3, 2013

Soma magazeti ya leo Jumamosi tarehe 2 November 2013 Hapa.............

Stori:IMELDA MTEMA
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.
Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham Sepetu.

DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.
                                                     STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond.
AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu.

MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein.
Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke ndipo waombolezaji wengine watawanyike.
“Jamani naomba sana itifaki izingatiwe, asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo.

DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.
Lakini kabla Rais Shein hajaanza kusimama, Diamond alinyanyuka na kuzua kasheshe kwa sababu baadhi ya watu, hasa wa umri wake walianza kumkimbilia huku wakikanyagana na kusababisha hali ya taharuki.

MC AWATULIZA WATU
Baada ya watu kuanza kukimbizana hovyo muongozaji wa msiba huo aliwaomba watulie na kusema kuwa wasiogope ila kuna staa ambaye anapita ndiyo maana watu wamemkimbilia.
“Naomba utulivu huyo ni staa f’lani kapita huko ndiyo maana watu wanamkimbilia hivyo tulieni kwanza viongozi wetu waondoke,” alisema.

USALAMA WA TAIFA NUSURA WAMKAMATE
Baada ya kuona watu wakikimbia hovyo baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa walitaka kumkamata msanii huyo wakisema alisimama kwa makusudi licha ya kusikia tangazo la kiitifaki.

WATU WAMSHANGAA DIAMOMD
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walionekana kushangazwa na kitendo cha Diamond na kusema kuwa ni vyema angesubiri viongozi wote waondoke ndipo na yeye atimke lakini kufanya vile si sahihi.
“Huyu Diamond kwani ana nini? Nakumbuka kwenye msiba wa Kanumba kule Dar pia aliingia kipindi ambacho ilitangazwa kuna kiongozi anakwenda, utaratibu ukatibuka, watu wakawa wanamshangilia yeye,” alisema mtu mmoja aliyetoka Dar kwenda Zanzibar kumzika mzee Sepetu.

HUKUMU YA MASOGANGE YAPINGWA

Stori: Makongoro Ogin’g       
MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.

WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.
                                                                                  NZOWA
WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.

MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.

NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.

KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.
Pata habari kama hii kwa ufupi kwenye simu yako ya mkononi ya Vodacom kwa kutuma neno GLOBAL kwenda 15778.

KICHAKA CHA NGONO

Stori: Jelard Lucas na Chande Abdallah
UCHAFU unaendelea kufichuliwa! Safari hii Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke wamekifyeka kichaka cha ngono maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.
Tukio hilo limetokea juzikati usiku wa manane baada ya wakazi wa kitongoji hicho kuchoshwa na tabia za madadapoa hao waliokuwa wakifanya vitendo vichafu karibu na nyumba zao na kutoa taarifa kwa OFM.
Kikosi hicho kiliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Temeke, Englebert Kiondo na kupewa askari wa Kituo cha Mbagala Kizuiani na kwenda kukifyekelea mbali kichaka hicho.
Kondom zikiwa zimezagaa eneo la tukio.
Kichaka hicho kilikuwa na akina dadapoa wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 38 ambao walikuwa wakitoa huduma kwa wateja wao kwa shilingi 5,000 kwa raundi moja.
Walionaswa wakiwa katika difenda.
Mara baada ya polisi na timu ya OFM kufika eneo husika waliwakuta akina dadapoa wakiwa wamekaa tayari kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Pia, kikosi hicho kilimkuta mteja mmoja akiwa anapewa huduma hiyo ndani ya kichaka hicho kilichotapakaa kila aina ya kondom katika kona zote.
Ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na sehemu maalum ya kufanyia ngono ambayo ilikuwa imetandikwa boksi chafu huku sehemu ya mlango ikizibwa na gunia aina ya ‘salfeti’.
OFM ilibaini kwamba kabla ya dadapoa na mteja wake kuingia ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na malipo ya fedha kwa  mmiliki wa kichaka hicho ambaye alifahamika kwa jina maarufu la Babu ambaye hata hivyo, alifanikiwa kukimbia baada ya kuona madadapoa hao wakikamatwa.
Pamoja na hayo, oparesheni hiyo ilimnasa kahaba mdogo kuliko wote aliyejitambulisha kwa jina moja la Sarah (16) ambaye alidai kuwa ni yatima kutoka Mkoa wa Mtwara na alijichanganya katika biashara hiyo haramu kwa ajili ya kutafuta kipato kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia.
Oparesheni hiyo pia ilimnasa mama mtu mzima aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce (38).
Pamoja na mama huyo kuhojiwa sababu ya kuingia katika biashara hiyo aligoma kuzungumzia kutokana na aibu.
Watuhumiwa wengine  pia waligoma kutoa ushirikiano kwa OFM kwa kuhofia kuvunja ndoa zao kwa kuwa ilibainika kwamba wengi wao ni wake za watu.
Madadapoa hao pamoja na mteja aliyenaswa walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kizuiani na kufunguliwa jalada la kesi namba MBG/RB/11343/13 KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA, kabla ya kupandishwa kizimbani kwa hatua zaidi za kisheria.

MAPYA YAIBUKA MWANAMKE ALIYEPIGWA RISASI

Stori: Mwandishi wetu, Arusha
NYUMA ya sakata la mwanamke, Violet Mathias, mkazi wa PPF jijini hapa aliyepigwa risasi begani na polisi baada ya kukaidi amri ya kutopaki gari sehemu isiyoruhusiwa katika Benki ya CRDB Jengo la TRA hivi karibuni, limeibua mambo mapya nyuma ya pazia.
Ilidaiwa kuwa, polisi alimuwahi mwanamke huyo baada ya yeye kuchukua bastola kwenye gari na kuikoki tayari kumfyatulia, akapigwa yeye mkononi.
Habari nyuma ya pazia zilidai kuwa, siku hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke huyo na watu wengine kuzuiwa kupaki sehemu hiyo ambayo ina mlango wa kuingilia mkono wa kushoto wa Jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo ndani yake kuna Benki ya CRDB.

Toyota Cresta lenye namba za usajili T888 BWW mali ya Vailet Mathias lililotolewa upepo na kusababisha ugomvi baina ya Polisi na mmiliki huyo aliyepigwa risasi begani.
Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, Violet alipaki tena gari eneo hilo na alipofuatwa na kuambiwa akalisogeze alikataa kwa nyodo.
Ilidaiwa kuwa baada ya kunusurika kifo Violet au Vai kama anavyojulikana jijini hapa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambayo ipo hatua kadhaa kutoka eneo la tukio.
Habari zilidai kuwa katika kuficha tukio hilo, Violet ambaye ni mwanamke mrembo na mfanyabiashara wa madini na kusafirisha watalii alihamishwa ‘kiaina’ katika hospitali hiyo na kupelekwa Hospitali ya Seliani iliyopo jijini hapo.
Hata hivyo, katika tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kumekuwa na usiri mkubwa wa waandishi wa habari kujua wodi aliyolazwa kwa kuwa ndugu hawataki apigwe picha.
Kutokana na kuzagaa kwa silaha mkoani hapa, jeshi la polisi limeombwa kukusanya silaha zisizo milikiwa kihalali kutoka mikononi mwa raia ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.

MSTAHIKI MEYA ALIVYONUSURIKA MKONG’OTO

Stori: Mashaka Baltazar,Mwanza
TUKIO la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, Henry Matata, kunusurika mkong’oto kutoka kwa madiwani wa manispaa hiyo wakidai kutomtambua lilikuwa kama sinema.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri juzi (Alhamisi) asubuhi baada ya meya huyo kufungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela.
Katika kikao hicho, madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtaka meya huyo aondoke kwenye kiti wakidai kutomtambua ndipo ukaibuka mtiti wa mshikemshike nguo kuchanika.
Huku vita ya maneno ikiendelea, Matata aliwaamuru madiwani hao watoke nje ya ukumbi lakini wakamvimbia wakimtaka yeye ndiye atoke.
Baada ya kadhia hiyo kuwa kubwa huku madiwani hao wakisukumana wao kwa wao wakitaka kumpiga meja huyo, ndipo simu ikapigwa polisi Kirumba ili waje kutuliza hali ya hewa.
Hata hivyo, wakati askari hao wakisubiriwa ndipo vijana wenye miili mikubwa ‘mabaunsa’ waliodaiwa kuwa wapambe wa
Matata wakavamia ukumbini kumnusuru na hakuna mtu aliyekamtwa wala kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ilikuwa ni sinema ya bure huku mabaunsa wakipongezwa kwa namna walivyomuokoa meya huyo kimafia.
“Kweli kabisa mabausa wamefanya kazi  nzuri kwa  sababu hali ilikuwa mbaya sana. Kama siyo kumuondoa kimafia na kiintelijensia, wangemalizana,” alisema Antony Maduhu aliyeshuhudia kila kitu.

Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha-8

Karibu msomaji wangu katika safu yetu hii, mada yetu ni ileile na tupo kwenye kipengele kinachosema “Kudhani mapenzi ni kitandani peke yake”, hayawezi kuwa bora kama mtakuwa na mtindo mmoja kila siku. Kama chakula ukila cha aina moja unakinai, hata mapenzi pia.Mapenzi bora ni yale yenye mashamshamu na mizuka mingi. Bafuni inawezekana kukata kiu zenu hukohuko. Nenda naye kuoga, mkiwa huko tumia utundu wako wa asili kumchokoza na kumchokonoa. Ataelewa na mwisho kitaeleweka tu.
Kama mpo kwenye nyumba ambayo mnaishi wawili, mnaweza kupeana huduma kwenye korido, sebuleni na mahali pengine popote ambapo patawaruhusu. Tafsiri ya maelezo haya ni kwamba hutakiwi kufikiria kitanda kila siku kwamba ndicho chenye ukomo wa tendo lenu.
Tambua pia kuwa kila hatua kuelekea kwenye kilele cha tendo lenyewe, inajitosheleza kuitwa kitendo cha mapenzi, kwa hiyo usibane hisia zako wala usitegee. Jinsi unavyojiachia na kutoa ushirikiano kwa asilimia 100, ndivyo mwenzi wako anaweza ‘kuinjoi’ hasa huduma yako.
Si yeye tu, wewe pia utakuwa na wakati mzuri wa kufurahia mapenzi kama utathamini kila kitendo mnapokuwa safarini, ukashea naye ubunifu na uzoefu wako wote hatua kwa hatua. Hivyo ndivyo mapenzi yanataka, kwani yalifanywa yatendeke kwa wawili.
Siyo mpaka mwanaume aseme, wewe unayo fursa ya kutoa mwongozo wa jinsi mambo yanapaswa kuwa. Achana na imani za kizamani kwamba mwanamke akianzisha mwendo ataonekana ana mambo mengi. Ishi kisasa, unapokuwa na mwenzio faragha, onesha utundu wako wote.
Ikae kichwani kwako kwamba mwanaume mwenye shauku ya mapenzi, anayejua maana na thamani ya tendo husika, anapokutana na mwanamke mtundu, huburudika zaidi. Asikwambie mtu, hakuna mwanamke anayetaka mwanamke ambaye yupoyupo.
Haya sasa, chukua fursa halafu mwende zenu. Acha mambo ya kukariri, badilika iwezekanavyo. Safari moja lakini inawezekana mkabadili mitindo kadhaa na ikawa safi. Ila kama uzoefu unaonesha mwenzi wako hufurahia zaidi mtindo fulani, basi ufanye uwe wa mwisho.

•KUHOFIA KUWA KINARA
Ni kweli kwamba wanawake hufurahia kuanzishiwa safari, hiyo ni kwa sababu huonesha jinsi mwanaume alivyo na shauku naye. Hili limekaa kimaumbile zaidi kwa sababu wanawake wana kawaida ya kusubiri kuelekezwa kuliko wao kuwaelekeza wanaume wao.
Ni tabia ambayo imejengwa na mfumo wa kudeka ambao wanawake wanao. Imestawishwa na mfumo dume unaotukizwa katika jamii zetu kwamba mwanaume ndiye mwenye sauti, kwa hiyo hata huduma ya faragha hupatikana pale mwanaume anapohitaji tu.
Huo mfumo dume unapojumlishwa na kauli zisizo za msingi za vijiwe vya wasioelewa mantiki ya mapenzi kwamba mwanamke anayekuwa kinara kitadani ni kicheche, kwa pamoja ni sababu ya kulemaa kwa wanawake wengi kiasi kwamba huwa waoga kufanya kilicho bora faragha, kwa kuchelea kuonekana hawajatulia.
Tupa kule imani hizo na mifumo hiyo. Simama kisasa, onesha uwezo wako wote, juu ya hapo ni kuwa kinara pale unapoona hisia zako zinakutaka ufanye hivyo. Omba mechi na mwenzio akikuelewa, basi mpe kile kilicho bora ambacho unaamini anastahili. Hutaonekana hujatulia, zaidi mwenzi wako atakukubali zaidi na zaidi.

•KUTAKA KILE TU UNACHOPENDA, KUTOTAKA USICHOPENDA
Katika vipengele ambavyo hutafurahishwa navyo, si vizuri kuonesha maringo au mapozi hasa unapobaini kwamba kipengele husika kitamfanya mwenzi wako afurahie tendo kikamilifu. Hii ni kwa sababu mapenzi hayataki ubinafsi, kwamba kwa vile wewe hutaki ndiyo ikubalike, la hasha!
Unapomsikiliza mwenzi wako ndiyo hasa unakamilisha tafsiri ya tendo la mapenzi. Mathalan, wewe hupendi denda lakini mwenzi wako anahitaji sana. Hapo hutakiwi kushika msimamo wako jumla, badala yake inatakiwa umpe anachotaka. Jilazimishe kumridhisha mwenzi wako.
Ukiwa faragha hujisikii kuzungusha nyonga. Hata hivyo, hiyo huwa hujizungushii wewe, kama anayezungushiwa anapenda, jilazimishe mpaka aridhike. Kwa kifupi ni kwamba inafaa uheshimu mambo mawili, yale ambayo ukifanyiwa ndiyo mwafaka, vilevile usisahau yanayompa ‘wazimu’ patna wako.
Vivyo hivyo kwa uvaaji wa chachandu, kama hupendi ila yeye anapenda, vaa kwa ajili yake. Ikiwa yeye hapendi ila wewe unapenda, mshawishi apende lakini ikishindikana achana nazo. Muhimu ni kila mmoja, yaani wewe na yeye, wote mfurahie kilele cha tendo.

•KUZUNGUMZA NINI NA WAKATI GANI
Linapokuja suala la mazungumzo wakati wa tendo, ukweli ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo wake. Jambo la muhimu kwako ni kumsoma mwenzi wako mapema sana, ujue yeye yupo upande gani. Jawabu lako litakusaidia mbele ya safari.
Hata hivyo, mwongozo katika sura pana ni kwamba mazungumzo tofauti na tendo yanaudhi. Mathalan, katikati ya shughuli mtu anaanza kuulizia habari za kazi, unadhani picha hapo zitakwenda au mtakatana stimu? Muhimu hapa ni kuangalia nini cha kuzungumza.


YANGA YAPAA VPL: YAICHABANGA JKT RUVU 4-0


Yanga SC imeichabanga JKT Ruvu mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar na kufikisha pointi 25. Wafungaji wa mabao ya Yanga: Mrisho Ngassa dakika ya 3 na 12, Oscar Joshua dakika ya 47 na Jerryson Tegete dakika ya 89.



No comments:

Post a Comment