Stori: WAANDISHI WETU
AMA
kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze
yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji
mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa
wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine, Ijumaa linaibumburua.
Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM.
Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini
kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa
uchafu…
Stori: WAANDISHI WETU
AMA
kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze
yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji
mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa
wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine, Ijumaa linaibumburua.
Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM.
Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini
kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa
uchafu wa aina yake nyuma ya pazia.
Saluni hiyo maarufu kuliko Miji
ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza ambapo kwa muda mrefu sasa
imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi
wenye maadili yaliyotukuka.
TAARIFA MEZANI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
chini ya Global Publishers, ikiwa imetulia ndani ya mjengo wa makao yake
makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar, Mkuu wa kikosi maalumu cha Mtambo wa
Kurekebisha Tabia (MKT) ambacho ni kitengo ndani ya OFM, alipokea simu
kutoka kwa msamaria mwema akitoa ‘tipu’ juu ya ishu hiyo.
Mhudumu baada ya kumpatia dozi mteja.
Mtoa taarifa huyo alieleza malalamiko yake juu ya kero wanayoipata
raia waishio jirani na saluni hiyo kufuatia huduma chafu za kuchukiza
ambazo hufurahiwa na shetani na malaika wake tu.
Msamaria Mwema: Halooo.... halooo... jamani halooooo, hapo ni Makao Makuu ya OFM?
OFM: Ndiyo mama, tukusaidie nini?
Msamaria Mwema: Mna habari jamani?
OFM: Zimejaa tele, ila hata ya kwako inaweza kuwa bora kuliko tulizonazo.
Msamaria
Mwema: Hapa Sinza Kwaremi (Dar) kuna saluni moja inaendesha vitendo
vichafu vya ngono na hakuna sheria yoyote inayochukuliwa dhidi ya
wahusika.
...Huyu alinaswa akikimbia baada ya OFM kutia maguu eneo la tukio.
OFM: Saluni ya ngono? Kivipi mama? Hebu fafanua tafadhali!
Msamaria Mwema: (kwa sauti ya juu mno) ninyi njooni mtajua kila kitu hukuhuku lakini inaendesha mambo ya ajabu (simu ikakatika).
OFM MZIGONI
Bila kupoteza sekunde, mkuu huyo wa
MKT, aliwapanga ‘makamanda’ maalumu na kuwapa maelekezo muhimu ya jinsi
ya kujua ukweli juu ya uovu uliodaiwa kutendwa kwenye saluni hiyo.
UCHUNGUZI
OFM iliwatuma vijana wake ‘watanashati’
hadi eneo lililotajwa ili wachunguze kama kweli kuna saluni yenye jina
lililotajwa na mtoa habari wetu.
Baada ya maelekezo hayo, vijana hao
wakiongozwa na roho safi ya kunyoosha maadili katika jamii, walifika
hadi Sinza na kukuta saluni yenye jina hilo ambapo walianza kufanya
upelelezi wa hali ya juu mno huku wakiwa makini kuliko hata neno
lenyewe.
UTHIBITISHO
Baada ya kutinga eneo hilo, OFM
iliendesha upelelezi maalumu kwa kuwauliza baadhi ya wakazi na watu
wanaofanyia shughuli zao za kujiingizia riziki na kupata ukweli halisi
juu ya ufuska ufanywao ndani ya saluni hiyo.
Katika uchunguzi huo, OFM ilipata uthibitisho kuwa kweli ibilisi yuko katika hesabu zake za mwaka kwa kufanya uchafu wa kufuru.
Ilielezwa kwamba, watumishi wa saluni hiyo ambao ni warembo,
hujifanya wanatoa huduma ya kuchua mwili (body massage) kwa Sh. 25,000/=
kwa vyumba na huduma za kawaida, lakini kwa vyumba vyenye choo na bafu
kwa ndani (self contained) ni Sh. 35,000/=.
HUDUMA
Katika upelelezi huo, ilibainika kuwa
mteja akilipia gharama ya vyumba vya self contained, ana uhuru wa
kuchagua kama atapenda kufanyiwa huduma ya uchuaji kwa mikono tu au kwa
matiti na wakati mwingine mwili mzima huku mtoa huduma hiyo akiwa amevua
nguo zote!
Ikazidi kuelezwa kuwa, endapo mhudumiwaji atataka huduma hiyo ya
mchuaji kuvua nguo zote, atafanyiwa hivyo lakini kama atazidiwa na
kuhitaji huduma ya ngono, atatakiwa kuongeza Sh. 50,000/= kwa msichana
huyo wa huduma na kufanya gharama kuwa zaidi ya Sh. 80,000/=.
“Wamekuwa wakifanya vitendo viovu sana, yaani ngono njenje, jamani
hii siyo saluni, bali ni danguro la ngono fuatilieni mtangundua juu ya
ukweli huu,” alisema mmoja wa raia katika upelelezi wa OFM.
OFM NDANI YA NYUMBA
Ili kujiridhisha na maelezo
hayo, timu ya OFM ilituma vijana wake tofauti kwa muda wa siku tatu
mfululizo na kubaini kuwa yote yaliyosemwa na kutajwa kwa kirefu
yanatendeka ndani ya saluni hiyo!
‘Askari’ wa kwanza wa OFM aliingia
ndani ya saluni hiyo (jina linavunda kwenye droo za meza yetu) na
kuwakuta wahudumu wamejaa tele na alipowauliza juu ya huduma ya masaji
na ngono, walijibu kwa sauti ya furaha na bashasha kubwa bila kujua kuwa
kijana wetu alikuwa na vifaa maalumu vya kunasia sauti.
“Ni wewe tu jamani, kwani wewe ni mgeni maeneo haya? Mbona utaratibu
unaeleweka, lakini maelezo ni hayo kwa hiyo karibu sana,” alisema mmoja
wa warembo hao huku akilegeza macho mithili ya mgonjwa wa degedege.
Siku mbili zilizofuata, askari wa OFM waliendelea kupata stori na maelezo ya aina hiyohiyo.
MTEGO!
Siku ya tukio, (mwanzoni mwa wiki hii) OFM
iliweka mtego kwa kumpeleka kijana wake ili ajifanye anahitaji huduma
hiyo ya kufanyiwa masaji mwili mzima na baadaye ajifanye amezidiwa na
kuhitaji huduma ya ngono.
Katika mtego huo, OFM ilitoa taarifa polisi
ambapo ‘vijana wa IGP Ernest Mangu’ hawakulaza damu, wakatoa ushirikino
wa kutosha kwa OFM.
MTEGO WAFYATUKA
Kama kawaida, OFM huwa haishindwi
linapokuja suala la oparesheni maalumu kama hiyo, fuatilia sana. Mtego
wake ulifyatuka ambapo mmoja wa vijana wake alijifanya kuhudumiwa
(angalia picha ukurasa wa mbele).
Baada ya kuweka mazingira sawa, OFM
na polisi wa kike na kiume walivamia na kufanikiwa kufuma laivu matukio
mengi ya ufuska mkubwa (ukitaka kuona zaidi, unakaribishwa Bamaga
ofisini kwetu).
WAUME ZA WATU!
Baada ya zoezi hilo kukamilika,
baadhi ya mashuhuda (hasa akina mama) walisikika wakishukuru kufumuliwa
kwa saluni hiyo kwa kuwa ndoa zao zilikuwa zimeanza kuota magugu kwani
wateja wengi wa saluni hiyo ni waume za watu na vigogo serikalini!
“Jamani tunashukuru sana, waume zetu walikuwa wanakimbilia hapo,
ugomvi kidogo tu, mwanaume anakwenda hapo na akirudi nyumbani hana
habari kabisa na mkewe, safi sana OFM na polisi kwa jumla,” alisikika
mama Joyce akishangilia kufumuliwa kwa saluni hiyo.
SOO POLISI
Baada ya ‘sheshe’ hilo, warembo sita walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa upelelezi maalumu.
MMILIKI
Katika upelezi wa awali, watumishi hao
walimtaja mmiliki wa saluni hiyo kwa jina moja la Chifu huku wakishindwa
kuweka wazi na kufafanua kwa undani zaidi.
KAMANDA WAMBURA UPO?
Gazeti hili lilifanya
jitihada za hali ya juu kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
ACP Camilius Wambura ili azungumzie juu ya sakata hilo, lakini hadi
gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita
bila kupokelewa.
KUTOKA IJUMAA:
Timu nzima ya OFM na dawati la
Ijumaa kwa jumla, tunalaani vikali kuwepo kwa vitendo viovu kama hivi
vinavyokwenda kinyume na maadili na utamaduni wetu kwa sababu
vinachochea mmomonyoko wa maadili na ongezeko la maambukizi mapya ya
virusi vya Ukimwi.