Saturday, January 11, 2014

LULU AMSHANGAZA MAMA KANUMBA

Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema

MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
Keki aliyoleta Lulu kwa ajili ya mama Kanumba.
Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.…
Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
Keki aliyoleta Lulu kwa ajili ya mama Kanumba.
Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.
Lulu akimpatia keki mama Kanumba.
“Yaani mama Kanumba alikuwa hajui kuwa Lulu anajua siku yake ya kuzaliwa, Lulu akatumia nafasi hiyo kumfanyia ‘sapraizi’,” alisema rafiki wa karibu wa Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
...Lulu akimlisha keki mama Kanumba.
Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia mama Kanumba akiwa amepigwa na butwaa huku akilengwalengwa na machozi ya furaha. Mahojiano yalifanyika kama ifuatavyo;
Ijumaa: Hongera mama, sasa unatimiza miaka mingapi?
Mama Kanumba: Nimetimiza miaka 58.
Mama Kanumba akimlisha keki mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila.
Ijumaa: Umejisikiaje kwa zawadi ya keki uliyoletewa na Lulu?
Mama Kanumba: Nimejisikia furaha sana kwa kweli, Lulu ni mwanangu, nimefarijika, kwa sababu watoto wangu hawapo, leo ningekuwa peke yangu lakini kama unavyoona, mama na mwanaye wamekuja toka asubuhi tunasherehekea nao kwa kula na kunywa na Lulu amegharamia kila kitu.
Baada ya swali hilo Ijumaa lilihamia kwa Lulu.
Kutoka kushoto: Flora Mtegoa, Lulu na Lucresia Karugila katika pozi.
Ijumaa: Ulijuaje leo ni siku ya kuzaliwa ya mama Kanumba?
Lulu: Nilijua katika maongezi siku sita zilizopita, kwani ilikuwa ni tarehe moja ya mwezi huu ambapo amezaliwa mama yangu mzazi na dada yangu.
Ijumaa: Kwa nini uliamua kumfanyia Sapraizi ya keki mama Kanumba?
Mama Kanumba akikata keki.
Lulu: Niliamua kumfurahisha kwa sababu ni siku yake ya kuzaliwa na sikufanya kwa sababu mwanaye hayupo, hata angekuwepo ningemfanyia tu.
Ijumaa: Asanteni, mama na Lulu tunawatakia maisha mema.
Flora Mtegoa akipozi na Lulu.

MASOGANGE ANASWA NA BWANA WA JACK

Na Mwandishi Wetu

VIDEO Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.
Masogange akipozi na Jux.
Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.
http://api.ning.com/files/Iht4Psekqy0wttdXe*EsPRkqo*eRW*Qp69gUzbFS7smv8PTpbqof801LuB2JiAsnEHN0DmKCmtkMNQ9uNA-PB4Cq4PCBRIbh/jacknajux.jpg%3Fwidth%3D650 Jux akiwa na mpenzi wake…
Na Mwandishi Wetu
VIDEO Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.
Masogange akipozi na Jux.
Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.
http://api.ning.com/files/Iht4Psekqy0wttdXe*EsPRkqo*eRW*Qp69gUzbFS7smv8PTpbqof801LuB2JiAsnEHN0DmKCmtkMNQ9uNA-PB4Cq4PCBRIbh/jacknajux.jpg%3Fwidth%3D650Jux akiwa na mpenzi wake Jack Patrick.
Akiuzungumzia ukaribu wake na Jux, Masogange alisema: “Wala hakuna lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa  tunabadilishana mawazo tu.”
Masogange akiwa na Jack.
Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange wakijiachia kumeibua maswali mengi.


MREMBO AZUA KASHESHE, KISA WIVU WA MAPENZI!


Mrembo akizua kasheshe baada ya kutolewa nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala, Dar.
Stori: Issa Mnally

AMA kweli pombe siyo chai. Timbwili la aina yake liliibuka ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala jijini Dar hivi karibuni baada ya dada mmoja kuanzisha kasheshe alipomkuta mpenzi wake akiwa amekaa kimahaba na demu mwingine.…

Mrembo akizua kasheshe baada ya kutolewa nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala, Dar.
Stori: Issa Mnally
AMA kweli pombe siyo chai. Timbwili la aina yake liliibuka ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala jijini Dar hivi karibuni baada ya dada mmoja kuanzisha kasheshe alipomkuta mpenzi wake akiwa amekaa kimahaba na demu mwingine.
Mrembo akiwa mikononi mwa baunsa.
Kisa kizima kilichoshuhudiwa na paparazi wetu kilitokea majira ya saa 8:00 usiku baada ya dada huyo kwenda kujisaidia msalani na aliporudi akamkuta mpenzi wake akiwa ameinamiwa na demu mwingine kimahaba.
...Akitolewa nje ya ukumbi na baunsa.
Dada huyo alipomuona mpenzi wake anamsomesha demu mwingine, hakukubali akamrukia yule demu aliyekuwa akizungumza na mpenzi wake na kuwafanya wote kuanguka chini ndipo timbwili lilipoanza.
...Twende nje.
Hata hivyo, timbwili hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani walinzi wakiwemo mabaunsa walifanya kazi ya ziada kumtoa dada huyo ukumbini hapo huku akiwa hana viatu.
...Mrembo akitaka kurudi tena.
Hata hivyo, katika kuepusha vurugu zaidi, walinzi wa eneo hilo walimuomba mpenzi wa sistaduu huyo naye atoke nje ili wakamalize ugomvi wao kisha waende wakalale.
...Akizidi kukinukisha.

JOHARI AWARUSHA ROHO RAY, CHUCHU HANS

Stori: SHAKOOR JONGO

HUKU Ray na Chuchu Hans wakionekana penzi lao limepamba moto, mpenzi wa zamani wa  Ray, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuwarusha roho wawili hao baada ya kutupia mtandaoni picha inayomuonesha kidoleni amevaa pete ya ndoa.
Johari.
Wakizungumza na Ijumaa baadhi ya watu waliobahatika kuiona picha hiyo wamesema kuwa kitendo cha Johari kuweka picha hiyo ni sawa na kuwarusha roho wawili hao kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuolewa kabla ya Chuchu na Ray kufunga ndoa.…
Stori: SHAKOOR JONGO
HUKU Ray na Chuchu Hans wakionekana penzi lao limepamba moto, mpenzi wa zamani wa  Ray, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuwarusha roho wawili hao baada ya kutupia mtandaoni picha inayomuonesha kidoleni amevaa pete ya ndoa.
Johari.
Wakizungumza na Ijumaa baadhi ya watu waliobahatika kuiona picha hiyo wamesema kuwa kitendo cha Johari kuweka picha hiyo ni sawa na kuwarusha roho wawili hao kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuolewa kabla ya Chuchu na Ray kufunga ndoa.
Ray na Chuchu.
“Unajua kila mtu ana njia yake ya kufikisha ujumbe, kitendo cha hivi juzi Ray na Chuchu kujiachia bila ya kificho katika Viwanja vya Leaders Club, ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Bongo Movie ni sawa na kumwambia Johari hana chake ndiyo maana na yeye ameamua kurudisha kijembe kwa staili ya kuweka picha aliyovaa pete ya ndoa ili kuonyesha kuwa yeye ataolewa ila Chuchu atachezewa tu na kutupwa,” alidai mmoja wao.
Baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa wadaku hao Ijumaa lilimuendea hewani Johari ambapo alipokea simu na kusema atafutwe muda mwingine kwani  alikuwa yupo bize.

SANDRA NA RUSHWA YA NGONO BONGO MOVIE

Stori: Mayasa Mariwata

STAA wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’ amesema kuwa tangu ajiunge Bongo Movie hakuna manufaa aliyoyapata kwa kuwa chama hicho kinaendekeza ubaguzi kwa kuthamini rushwa ya ngono.
Salma Salmini ‘Sandra’.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kikubwa kinachoikwamisha tasnia hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni watu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa labda wanatoka kimapenzi au kutegemea kupewa rushwa ya ngono ili impe shavu mtu.
“Namsihi…
Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’ amesema kuwa tangu ajiunge Bongo Movie hakuna manufaa aliyoyapata kwa kuwa chama hicho kinaendekeza ubaguzi kwa kuthamini rushwa ya ngono.
Salma Salmini ‘Sandra’.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kikubwa kinachoikwamisha tasnia hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni watu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa labda wanatoka kimapenzi au kutegemea kupewa rushwa ya ngono ili impe shavu mtu.
“Namsihi sana huyu kiongozi wetu wa sasa awe makini na hili suala, yeye pamoja na utawala wake wote wapinge haya mambo na tushikamane ile kuleta maendeleo, maana kila siku wanaopewa madili ya maana ni walewale lakini wengine tunaheshimika kwa majina tu huku dhiki zikitutawala,” alisema Sandra.


BASI LA MTEI LATEKETEZWA KWA MOTO BAADA YA KUGONGA NA KUUA SINGIDA

Basi la mtei likiteketea kwa moto baada ya kuchomwa na watu wenye hasira kali.…
Basi la mtei likiteketea kwa moto baada ya kuchomwa na watu wenye hasira kali.
Muonekano wa basi la Mtei baada ya kuzimwa moto huo.
Habari ambazo mtandao huu umezipata kutoka Singida zinasema Basi la abiria la Matei linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Dar  limechomwa moto na kuteketea kabisa na watu wenye hasira kali baada ya kugonda bodaboda ambayo ilikuwa imepakia ‘mshikaki’ wa watu watatu ambao walikufa papohapo eneo la tukio.
Hakuna abiria wa basi aliyeumia.  Mwandishi wetu aliye kwenye tukio amesema Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela yupo eneo ya tukio akishughulikia sakata hilo.

No comments:

Post a Comment