Patrick Ole Sosopi ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA (Baraza la Vijana Chadema). Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi mbalimbali vya maisha yake. Historia yake ya uongozi ni kuanzia akiwa Elimu ya Sekondari mpaka Chuo Kikuu.
Patrick Ole Sosopi. Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani. Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO).
Ni mpenda maendeleo na amekua mstari wa mbele kutetea ukombozi wa Taifa letu. Akielezea historia yake kwa ufupi Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na watu wote kwa ujumla na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.
Patrick Ole Sosopi ni
mojawapo wa waanzilishi wa Chadema Students Organizati (CHASO) mkoani Iringa,
Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa
wa Iringa pamoja na Mbeya.
Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na
kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali
za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA
Bara. Hivyo anaomba kula zako wewe Mtanzania ili kuleta mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu. Uchaguzi unategemewa kufanyika tarehe 10/9/2014 Dar es salaam Makao makuu ya Chama.
Partick Ole Sosopi akihutubia Wananchi wa Iringa Mjini
Alipokuwa kwenye uchaguzi wa Kalenga Mwanzoni mwa mwaka huu
Akihutubia wananchi wa Wilaya ya Kilolo
Akiwa katika Jimbo lake la Isamani kama Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo hilo.
Akiwa Pawaga na wadau wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
No comments:
Post a Comment