Asilimia kubwa ya watu hasa vijana tunafikiri pombe ni kiburudisho cha kutufanya tusahau matatizo yetu. Watu wengi huita pombe mfariji kwani akishapata kilevi hujiona kama kila kitu kwake ni rahisi na kujiona yeye anaweza kila kitu na husahau mambo na shida zake kwa muda mfupi kabla Pombe zake hazijaisha kichwani. Leo nimependa kuzungumzia kidogo maswala ya ulevi kifupi labda yanaweza kutusaidi mimi na wewe pia.
SABABU ZINAZOPELEKEA WATU KUJIUNGA KATIKA ULEVI/KUWA WALEVI
Kama tunavyo fahamu asilimia kubwa ya watu wanajifunza kunywa pombe ukubwani kutokana na mambo ambayo yamewakuta katika kipindi hicho. Ninaamini hakuna mtu aliyezaliwa na pombe. Leo nitaeleza sababu chache zinazowafanya watu wengi kujiingiza katika maswala ya ulevi/kutumia vileo
- Mapenzi - Hili ni swala kubwa lakini kiufupi mapenzi yakienda kombo huwa yana athiri sana Saikorojia ya mtu na kumsababishia mtu kujiingiza katika maswala yasiyofaa kama vile ulevi.
- Umaskini/Hali ya kukosa mahitaji yake ya kila siku - Mtu wa aina hii anaweza kushawishika kutumia vilevi kutokana na ugumu wa maisha yake na kukata tamaa na kujiona hana thamani tena zaidi kushinda akiwa amelewa kila siku.
- Urafiki na watu walevi - Marafiki ni watu wakubwa katika maisha yetu na siku zote huwa chanzo cha kubadili maisha yetu eitha kuyaharibu au kuyajenga, inategemeana upo na rafiki wa dizaini gani na mnashauliana vipi. Huwezi kila siku kuambatana na mlevi kama wewe si mlevi.
- Matatizo ya kifamilia/Matatizo katika ndoa - Hii inaweza kuwa sababu ya watu kujiingiza katika kilevi mfano mtu anaweza kuwa ameoa/kaolewa na mtu ambaye hakuwa chaguo lake au alilazimisha mahusiano mwisho wa siku anajikuta mtu wa kujuta kila siku. Tunaamini ndoa ni Paradiso ndogo kama tu tutafanya matwakwa yake na kujua nini maana ya ndoa. Lakini endapo ndoa yako itakua na doa utajikuta huna furaha na kuona Pombe yaweza kuwa faraja yako. Nimeshuhudia watu wengi wakijiingiza katika ulevi hata watoto wadogo ukiuliza sababu anakwambia kuwa nyumbani wazee wanazingua mfano anasoma akifeli kidogo mzazi/mlezi anakosa busara za kuongea nae katika hali nzuri anakua akimfokea na kumsemea maneno mabaya ndipo mtoto huyo anafikili pombe yaweza kuwa mfariji wake.
- Msongo wa Mawazo - Kipindi kilichopita nimeshaelezea sana msongo wa mawazo hii pia inachangia kwa nafasi mtu akiwa hana furaha hana amani mawazo kila kukicha anajikuta anatamani aingie katika ulevi ili asahau shida zake
NJIA ZA KUACHANA NA ULEVI
TAFUTA KITU CHA KUKUWEKA BUSY MUDA ULIOKUWA UNAFIKILI KWENDA KULEWA
Watu wengi wanafikiri na kuhisi kuwa ni ngumu kuacha pombe la hasha si kweli endapo utatafuta kitu mbada cha kufanya kwa kipindi kile ulichokua unafikiria kwenda kunywa pombe utaacha kabisa, kama kucheza mpira, kufanya mazoezi, kusoma vitabu vya hadidhi mbalimbali, kuangalia moves hata kusikiliza mziki. Au jaribu kufikiri kitu gani unapenda sana kufanya ukifanya hivyo itakusaidia.
EPUKA MARAFIKI WALEVI
Sina maana usiwe na marafiki hapana unaweza kuwa hata na rafiki mlevi lakini wewe ukawa hutumii kilevi chochote. Tengeneza mazingira mazuri na marafiki zako ili tu wasijekushawishi ukaingia katika ulevi. Epuka kwenda nao sehemu za vilevi kwani wanauwezo mkubwa wakukushawishi nawe ukajikuta umeingia kwenye dimbwi hilo.
USIKAE NA MAMBO YANAYO KUUMIZA KICHWA
Hapa ninamaanisha hushahiri kukaa na kufikiri matatizo ambayo unaweza kuyatatua kivyovyote. Kuna wakati mwingine mtu anaweza kuwa kakosana na mmoja wa familia yake hafikiri kukaa chini wakazungumza ili tu kupata suruhu yeye anaanza kuweka mambo kichwa na kuumia sana hii haitakiwi hata kidogo kwani inaweza ikakufanya urudi ulikotoka.
EPUKA MITOKO ISIYO YA LAZIMA
Unaweza kualikwa na watu kwenda mazingira ambayo yanavilevi na wao wakiwa watumiaji ni bora kuahirisha kutoka nao ili usije kushawishika
MADHARA YATOKANAYO NA ULEVI
Madhara ya Ulevi ni mengi lakini kwa leo ntajaribu kuandika machache tu bila shaka yatakusaidia katika maisha yako na utajifunza kitu.
- Akili inalala kwani hutaweza kufikiri na akili itakua imeathirika ki Saikologia
- Vidonda vya tumbo.
- Kansa ya utumbo.
- Kansa ya Ini.
- Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni.
- Kisukari.
- pungufu wa nguvu za kiume.
- Kukosa hamu ya kula.
- Magonjwa ya moyo.
- Heshima kushuka kwa watu wanao kuzunguka.
- Unapoteza kujiamini
HAYA NI BAADHI TU YA MAMBO YA ULEVI. ANGALIZO KWA WOTE POMBE SI CHAKULA KWAMBA UKIACHA UTAKUFA NJAA. KAMA BADO UNAPENDA KUENDELEA KUISHI NA UNATAKIWA KUCHUKUA HATUA POMBE SI NZURI KWA AFYA ACHA KABISA.