Tuesday, October 21, 2014

Mahusiano ni jambo ambalo linachukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku. Ukiwa na mahusiano mazuri na mwenzi wako unajiweka katika mazingira mazuri ya kufanya shughuli zako mbalimbali. Leo ninapenda kuzungumzia mambo machache katika mahusiano ikiwa ni pamoja na Jinsi ya kudumisha mahusiano ya mbali, Nini Mwanaume/Mwanamke anapenda kufanyiwa, Mambo yanayopelekea watu kuvunja mahusiano na Heri kuvunja uhusiano ukigundua haya.



JINSI YA KUDUMISHA UHUSIANO WA MBALI.
Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa.
Hata hivyo, mapenzi ya mbali huwa ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na wakati mwingine mmoja wapo anaweza kutafuta nafasi na kwenda kumsabahi mwenzi wake japo kwa siku chache, au  kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama anakofanyia kazi laazizi na mwandani wake
Pamoja na hayo yote bado umbali hauwezi kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na mpenzi wako. Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo
utafanya haya:-

1. MAWASILIANO MARA KWA MARA.
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Jitahidi kila unapo amka asubuhi kumjulia hali umpendae, kuna baadhi ya watu hasa sisi kina dada tunasubili mpaka tutafutwe sisi na si sisi kuanza kuwajulia hali wenzi wetu, hapo tunakosea sana kwani katika mahusiano kila mmoja anajukum la kuhakikisha anamfanya mwenzi wake awe na furaha na kuzidisha upendo hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.
Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe. Maana ukikaa kimya unampa wakati mgumu na inaweza kuwa chanzo cha malumbano.

2. HESHIMU HISIA ZAKO:
Heshima ni kitu cha bure na heshima humfanya mtu akaheshimika zaidi. Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.
Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake lakini sio ule wakubomoa! Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.

Mambo hayo machache yanaweza kukufanya ukadumisha mapenzi yako na mpenzi aliyeko mbali na hatimaye kufikia malengo yenu.

MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAMKE HUPENDA KUFANYIWA NA MWENZI WAKE
  1. Jamani ukweli ni nguzo tosha ya mahusiano. Hakuna mwanamke anayependa kudanganywa nikiwa mmoja wapo. Ingawa naume wengi wanadai wasipotudanganya inakua ngumu kutupata ila wanakosea sana.
  2. Wanawake wengi tunapenda kuwa na wapenzi wetu muda mwingi kuliko hata marafiki zetu.
  3. Mwanamke hupenda mwanaume anaejali zaidi kuliko mbabaishaji 
  4. Wanawake tunapenda kusifiwa. Msifie mwenzi wako pale anapokua kapendeza sio mpaka akuulize "Eti baby nimependeza" Ukifanya hivyo atahamia kwa wale wanaomjali na kumsifia
  5. Mwanamke anapenda kuthaminiwa na mpenzi wake, hata ukiwa na watu wengi, onyesha unajali kuwa nae karibu, hujiona wa pekee
  6. Mwanamke hupenda kusikilizwa japokuwa wanaume hujifanya vichwa na kutuona hatuna la kuongea lakini sio kweli ni fikra zenu tu. Msikilize mpenzi wako uone kama na wewe hatokusikiliza.
  7. Mwanamke anapenda mpenzi wake akumbuke mambo muhimu ambayo amemwambia mfano tarehe ya kuzaliwa. Binafsi hapa naweza kuwa zaidi nafurahi sana mwenzi wangu anapokumbuka tarehe yangu ya kuzaliwa na kukumbuka japo kuniimbia najisikia burudani starehe. Ingawa hata sisi pia tunatakiwa kukumbuka tarehe ya kuzaliwa na mambo muhimu tunayoambiwa na wenzi wetu
  8. Mwanamke huthamini sana msg za mpenzi wake kuliko simu apigiwayo na mwenza wake, maana kuona faraja zaidi pindi asomapo msg hizo zaidi ya kupoteza muda kusubiri apigiwe au akupigie.
  9. Mwanamke hapendi kukalipiwa hata kama kakosea. Jitahidi umwite kwa upole umwambie kama amekosea na umrekebishe sio kuanza kumropokea hata mbele za watu.
  10. Mkumbuke kila wakati hata mara 2 kwa siku hata kama umetigwa jitahidi walau asubuhi ukiwa hujaanza shughuri zako na jioni pia ukimaliza shughuri zako.
  11. Punguza jeuri na kauli chafu kwa mwenzi wako.
Hayo yakizingatiwa utaona kama mwanamke anaweza kukufanyia lolote baya. Wanaume wengi wanapenda kuwachezea akili wanawake hasa pale watakapojua kuwa mwanamke huyo anampenda kutoka moyoni. Jitahidi kuwa na mapenzi ya dhati hasa kwa mwanamke anayeonesha kukujali.

MAMBO AMBAYO MWANAUME ANAPENDA KUFANYIWA
  1. Heshima, mwaume anapenda sana mwanamke amweshimu hapo anaona kama amefika mbingu ya pili. Wewe mwanamke unayekaa hata ujawahi kuitika vizuri kwa mpenzi wako utampoteza wenzio wakamdake mana kuna wanawake wengine hata wakiitwa utasikia anaitika "Nini" au "Unasemaje". Hizo sio kauli nzuri hebu jitahidi kumweshimu mwenzi wako kwa kila kitu.
  2. Jamani wanawake wenzangu mwanaume ni kama mtoto mdogo anapenda ahudumiwe vizuri na kujaliwa pia. Lakini msizidi sana mana wanaume wengine wakisikia hivyo sasa wanataka hadi mikono wanawishwe sina maana hiyo lakini tunatakiwa kuwajali na kuwatunza vyema pale panapobidi
  3. Wanaume wengi hawapendi kufuatiliwa katika maisha yao ingawa sio wote lakini kuna baadhi. Wanawake nasi mda mwingine tunakua na gubuza mala kidogo uko wapi na nani unafanya nini wanaume wengi hawapendi mambo hayo
  4. Pekupeku kwa simu zao. Wanaume wengi hawapendi wapenzi wao wawe wanapekua pekua simu zao za mkononi japo kuwa wao ndo kwanza kimbelembele kupekua simu zetu. Mi humo simo.
 MAMBO YANAYOPELEKEA WATU KUVUNJA MAHUSIANO
Kuna mambo mengi sana yanayopelekea mahusiano kuvunjika, endapo tu wampenzi watashindwa kujizuia na kuyakwepa  katika mahusiano yao
  • Uongo ulio kithili. Hatukatai kwenye mapenzi kunakudanganyana lakini uongo ukizidi mahusiano mengi huvunjika.
  • Wivu, kunawatu wanawivu jamani mpaka basi akimkuta mwenzi wake amesimama na mtu au hata kaenda kutembelewa nyumbani ye tatizo. Mi ninaamini mtu mwenye wivu sikuzote hajiamini kwanini usijiamini kama upo pekeako kwa mpenzi wako? Wivu unachangia sana watu kuvunja mahusiano.
  • Ku cheat, Kutobaki njia kuu kunasababisha sana mahusiano mengi kuvunjiaka mana mmoja wa wapenzi akigundua mwenzake anatoka hawezi kuvumilia kuendelea kuwa nae katika mahusiano.
  • Matumizi mabaya ya simu za mikononi na Mitandao ya kijamii vinachangia sana kuvunja mahusiano. unaweza kukuta mtu yupo na mpenzi wake lakini simu haiishi kuingia sms au kupigiwa na watu wasio na mana. Na kunawakati mwingine mwingine yupo na mpenzi wake lakini simu ndo kaikumbatia anachati mda wote sijui Whatsapp, Twitter,  Facebook na mitandao mingine ya kijamii. Hapo lazima umboe uliye naye hata ningekua mimi.
  • Marumbano na Migogolo ya mala kwa mala kugombana kwa wapenzi mala kwa mala kunakatisha sana tamaa ya kuendelea na mahusiano.
  • Kuzungumzia mahusiano yaliyopita. Jamani kunawatu wanakela ukikaa nae ye ndo kumwaga sifa tu za mpenzi wake wa zamani. Utasikia tulipendana mala alikua ananifanyia hivi hee jamani ye sio yeye kila mmoja anayake huwezi kufanyiwa kama alivyokua anakufanyia aliyepita. Kwani hadi mkaanza mahusiano si mlishasimuliana sasa kila siku gubu hilo hilo jamani inakera sana kusikia sifa za yule tu kila siku mie utanisifia lini. Au kuongelea mabaya ya aliyepita kila siku inakera jamani
Nimeandika baadhi tu ya mambo kwani hata mimi ni binadamu ninasahau pia lakini ukijitahidi kuyakwepa hayo utadumu na mwenzi wako milele


 UKIGUNDUA MAMBO HAYA NI BORA KUVUNJA MAHUSIANO
Kuna wakati tunakua kwenye mahusiano na watu ambao si sahihi kwetu: Hapa nakutajia mambo machache ambayo ukigundua ni bora kuvunja mahusiano kabisa.
1. Kama umefanya uchaguzi usio sahihi. Kunawakati tunakurupuka kuingia kwenye mahusiano eitha baada ya uachana na wapenzi wetu, au tukiwa tayari kwenye msongo wa mawazo.
2. Dini zetu, kama upo kwenye mahusiano na mtu wa Dini tofauti na wewe na mkashindwa kufika muafaka wa nini kifanyike ni bora kusitisha mahusiano yenu.
3. Kukosa Uaminifu (Ku cheat) ni bora kuvunja mahusiano iwapo utagundua mwenzi wako anatoka nje ya mahusiano yenu.
4. Kuwa na tamaa ya maisha makubwa tofauti na uwezo hii hasa inatugusa sisi wanawake kwani wengi hawana mapenzi na wanapenda mali hivyo ukiona upo katika mahusiano hayo ni bora kusitisha mapema kabla hamjafikia maamuzi magumu ya kuishi pamoja.
5. Uchumba wa mda mrefu, kuwa na mchumba kwa muda mrefu bila ndoa ni bora kuvunja mahusiano kwani Mungu atakua hakupanga ninyi muishi pamoja.

Vijana wenzangu ambao bado hamjaoa wala kuolewa twapaswa Kujitambua kwanza kabla hatujaamua kufanya maamuzi ya kutafuta wenza wa kuishi nao. Haya ni baadhi ya mambo tu lakini kila kitu bila kumshirikisha Mwenyezi Mungu haziendi kwahiyo kwa kila tunachokifanya hata tunapofikilia kuanzisha mahusiano mapya tumshirikishe Mungu kwanza mambo mengine yatafuata kwani kwake hakuna linalo shindikana. Twayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.

No comments:

Post a Comment