Thursday, October 3, 2013

JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG'OMBE

Leo nataka niwape somo la upishi wa Pilau. Jamani mchele ni mmoja lakini mapishi ni mbalimbali wapo watakao loweka wapo watao kaanga lakini mwisho tunapata chakula ki 1. Leo nitaongelea kidogo kuhusu Pilau.

Pilau ni Chakula kitam sana na chenye mvuto wa mwonekano wake hasa kikipabwa kwa vitu tofauti tofauti. Kama Karoti, Hoho, Njegere na hata Nyanya pia.
 Leo tutapika Pilau la Nyama ya Ngombe kwanza unatakiwa kuandaa vitu vifuatavyo.

MAHITAJI
Mchele (Basmati) 3 vikombe 

                             
Nyama ya ngo’mbe 1 kg
                       
Pilipili boga  1 kubwa
                                
Nyanya  2 kubwa
                         
Vitunguu maji 2 vikubwa
                       
Tangawizi 1 kijiko cha chai
                          
Ndimu1




                               







Mafuta ya kupikia  ½ kikombe
                  
Mdalasini   ½  kijiko cha chai
             


















Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
                           
Pilipili manga   ½ Kijiko cha chai
Hiliki  ½ Kijiko cha chai
                        

                                 

                                
     
             
                              




Hatua:
  • Chemsha nyama yako mpaka iive, uwe umeweka chumvi kiasi, hakikisha nyama ina supu ya kutosha wakati wa kuichemsha
  • Osha mchele wako tayari kwa kuutumia na kisha utenge pembeni
  • Weka sufuria jikoni, kisha ongeza mafuta. Yakisha pata moto weka vitunguu maji vilivyokatwakatwa na kuaanga viive. Ongeza chumvi kiasi na endelea kukoroga
  • Ongeza vitunguu swaumu vilivyopondwa na endelea kukoroga, koroga mpaka vitunguu vigeuke kuwa rangi ya kahawia na kuiva
  • Ongeza viazi ulaya, vilivyomenywa na kukatwakatwa kwa ukubwa uupendao, endelea kukoroga ili vipate kuiva


  • Ongeza njegere na endelea kukoroga ili vipate kuiva




  • Weka vipande vya nyama iliyochemka vyema ndani ya mchanganyiko wako. Koroga mchanganyiko huo na acha kwa dakika chache uive vyema




  • Na hivi ndo itakavoonekana baada ya dakika kama 10 hivi ulizoacha mchanganyiko uive vyema 






  • Sasa ndo tunaanza kuweka viungo vya pilau na tunaanza na vile ambavyo havijatwangwa. Anza na iliki na Mdalasini huku unaongeza maji pale yanapokauka





  • Ongeza viungo vingine naongelea  weka binzari nyembamba pia na koroga ili vichanganyike vyema. Lazma harufu nzuri utaisikia maana mchanganyiko wa viungo hivi una harufu tamu mnoo 

  • .




      
    • Supu uliyochemshia nyama itakua inaonekana hivi baada ya kuondoa nyama. Yaonekana tamu kunyweka ila usiinywe inahusika sana kwenye pishi letu 
    • Weka mchele wako uliokwisha kuuosha jikoni kisha endelea kuchanganya ili viungo vichanganyike vyema

                                        


    • Weka supu ya ya nyama kisha endelea kuchanganya

                                 


    • Weka viungo vya unga na Endelea kuchanganya kwa mda kidogo ili mchanyanyiko wa viungo uchanganyikane vizuri







  • Acha mchanganyiko uweze kuchanganyiko vyema huku vikichemka kwa dakika kadhaa na hivi ndo itakavoonekana





    • Funika Chakula chako kwa daki kadhaa ili kichemke vyema










  • Baada ya dakika kama 5 angalia chakula chako, kumbuka kupunguza moto pale maji yanapoanza kukauka. Angalia wali kama umeanza kuiva na kama bado haujaiva na maji yamepungua basi ongeza maji huku unaacha viweze kuiva vyema






  • Hivi ndio itakavyoonekana pale pilau yako itakapoanza kuiva vyema. endelea kupunguza moto kwani tayari menyu inakaribia kuiva




  • Maji yakisha kauka geuza chakula ili kichanganyikane vizuri tayari kwa kupakua
                                           

    Pakua chakula kwenye chombo kwa aajili ya kuandaa mezani
                                                  
    Unaweza kupamba chakula chako kwa vitu tofauti ulivyo andaa kama vile Nyanya, Hoho, Mbogamboga au Karoti.

    Chakula tayari kwa kuliwa











                                                   

    Vijue Vidonda vya Tumbo na jinsi ya kuepuka.



     Vijue vidonda vya Tumbo kwa faida ya Maisha yako.









    VIDONDA vya tumbo ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.


    Vidonda vya tumbo vimegawanyika sehemu mbili; vidonda vya ndani ya tumbo (gastric ulcer) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcer).

    Vidonda vinavyotokea katika utumbo ndivyo maarufu sana na huonekana zaidi kutokea kwa wanaume, na vidonda vya ndani ya tumbo huwashambulia wote wanaume na wanawake


    . Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja kati ya watu kumi atakuwa na vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo hutokeaje mwilini?

    Chakula kinapoingia tumboni kwa ajili ya kusagwa, tumbo huzalisha majimaji mbalimbali, miongoni mwayo yaliyo muhimu zaidi ni asidi hidrokloriki.

    Asidi hii huanza kula kuta za tumbo/doudeni. Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

    Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa na baadhi ya dawa kama corticostisteroids, caffeine, reseprine, n.k.


    Pili, udhaifu wa ute au kuta za tumbo/duodeni kuzuia ushambuliaji wa asidi. Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kuongeza kinga ya ute au kupunguza uzalishaji wa asidi.


    Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha

    Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

    Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo imetengenezwa kwa ajili ya kukisaga chakula chochote haraka iwezekanavyo.

    Lakini kama hakuna chakula cha kufanyiwa kazi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

    Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonesha kuwa akili hutumia biokemia katika mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangakia sana katika kutokeza kwa magonjwa mengi.

    Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

    Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili/mawazo yatokanayo na shida za maisha.

    Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, wenye kupewa talaka na wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

    Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya tendo.

    Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe hadhiri zaidi, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni yenye nguvu huongezeka.

    Kadiri mfadhaiko unavyokuwa mfupi, ndivyo pia athari yake inavyokuwa fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapokuwa mrefu, kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo, athari yake huendelea.

    Dalili za mfadhaiko

    Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko.

    Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote, kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi, kupoteza hamu ya tendo la ngono na kupoteza hamu ya chakula (au kula sana).

    Nyingine ni kukosa usingizi (au kulala sana), wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia pamoja, kushindwa falakinika, kushindwa kukumbuka na kushindwa kuamua, kughadhibishwa na vitu vidogo, kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

    Haraka haraka

    Haraka! Haraka! Lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba pia husababisha matumbo nayo kubanana.

    Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: "Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, husikia kiungulia baada ya kula". Haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

    Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

    Vyakula vya kusisimua

    Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile kachapu, haradali, achali, pilipili na vingine vingi huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji huchoma. Tumbo linahitaji kupozwa na si kusasuliwa.

    Dalili za vidonda vya tumbo

    Vidonda vya tumbo huambatana na maumivu ya kuchoma, kuwaka katika sehemu ya juu ya tumbo. Kwa kuwa aina mbili zote za vidonda vya tumbo hutofautiana, ni vizuri zaidi kuelezea kila kimoja.

    (a) Vidonda vya tumboni

    Maumivu ya vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takribani kati ya nusu ya chini na kwenye kitovu na mara nyingi kula huifanya kuwa mbaya zaidi. Tofauti na maumivu ya vidonda vya utumbo, maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi hayaishi mara moja pindi yanapoanza.

    (b) Vidonda katika utumbo

    Maumivu ya vidonda vya katika utumbo pia hukaa pale pale (kama katika vidonda vya tumboni). Tofauti na vidonda vya tumboni, katika vidonda vya utumbo mara nyingi kula husaidia kupunguza maumivu.

    Tofauti nyingine ni kuwa, wakati katika vidonda vya tumboni maumivu huongezeka haraka baada ya kula chakula, katika vidonda vya utumbo inaweza kuchukua saa mbili au tatu. Tabia nyingine ya vidonda vya utumbo ni kupotea kwa majuma au hata miezi bila sababu ya wazi.

    Mtu anaweza kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya duodeni, huchukua takribani saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya kidonda.

    Utambuzi wa vidonda vya tumbo

    Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hujumuisha X-Ray. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama 'endoskopy' au 'biopsy', ambayo huyakinisha hali halisi.

    Matibabu ya vidonda vya tumbo

    Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

    Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa muhimu.

    Katika vidonda vya tumbo ambavyo ni vikali, matibabu yake hutumia maziwa kwa mwanya wa dakika 15 hadi saa mbili kwa kutegemea ukali wa ugonjwa; kwa wiki moja. Maziwa hutumiwa pamoja na dawa.

    Maziwa si kwamba hupambana na asidi tu, bali pia huchelewesha muda wa tumbo kuruhusu dawa kufanya kazi kwa muda mrefu. Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4-6 za matibabu.

    Kuzuia mfadhaiko

    Kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kuwasabishia maradhi kama vidonda vya tumbo au maradhi ya moyo, n.k.

    Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha?

    (a) Kuridhika na maisha

    Kama tutakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, tukaacha kuyakopa maisha ya jana na tukaacha kuhofu maisha ya kesho, hakika kabisa matumbo yetu pia yatatulia.

    Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

    Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika kiwiliwili. Unaweza kuleta ugonjwa ambao ni wa kufisha kama ambao hutokana na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.

    (b) Kutopata usingizi wa kutosha

    Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahala. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii.

    Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.

    Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.

    Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.

    Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.

    Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne saa 12-14 kwa siku, miaka sita hadi minane saa 11-12 kwa siku, miaka minane hadi 11 saa 10-11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 saa 8-9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane. 


    NJIA ZA KUEPUKA VIDONDA VYA TUMBO
    • Ili kujiepusha na vidonda vya Tumbo jitahidi kuzuia mawazo yasiyo la lazima  
    • Epuka kujifikirisha mambo ya kuumiza. 
    • Jitahidi kula kwa wakati.
    •  Pia ukiridhika na maisha uliyo nayo hakuna kinacho shindikana.

    Wednesday, October 2, 2013

    HATARI MBEYA

    WAFANYA BIASHARA KUGOMA KUNUNUA MASHINE ZA TRA ZENYE THAMANI YA THS 800,000 JIJINI MBEYA, MADUKA YAFUNGWA. WANANCHI WAKAZANA KURUSHA MAWE NA KUCHOMA MATAIRI

     Polisi wakiwa katika ulinzi mkali 
     Maduka yakiwa yamefungwa 
     Wafanya biashara wakiwa uwanjani kungoja kusikiliza nini  hatma yao
     Baadhi ya watu wakiwa wanakimbia Baada ya Mabomu ya machozi kuanza kurushwa kuepusha vurugu
     Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
     Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
     Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia 
     Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite

    Tuesday, October 1, 2013

    WelcomeUniversity of Dodoma

    WelcomeUniversity of Dodoma

    slide1
    The University of Dodoma is a public institution, established in March 2007 following the signing of a Charter by the President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete. As a University, our core responsibility is to provide a conducive environment for teaching and learning, knowledge generation and community service.The educational programmes that are offered have been carefully designed to suite a wide range of clientele. Individual students have the opportunity to choose programmes depending on their interest and convenience. 
     slide6
    We wish therefore to invite individuals, institutions, development partners, the private sector, and well wishers to join us in this exciting initiative. Embracing knowledge is our motto. We are committed to create an outstandingly attractive enviroment to study and work. We are committed to build UDOM to an Institution of global standing that is capable of harnessing the power of knowledge to serve humanity. Join us in whatever way you can.

    slide2

    HUYU NDIO BINTI ALIYEVULIWA NGUO HADHARANI NA WANAKIJIJI MARA BAADA YA KUMCHANA NA VIWEMBE RAFIKI YAKE ALIYEMFUMANIA NA MPENZI WAKE..!

      ,  



    Hawa  ni  mabinti  wawili  ambao  walikuwa  ni  marafiki wa  damu.Urafiki wao uliingia  dosari  baada  ya  mabinti  hao  kusalitiana  na  kuchukuliana  wapenzi....

    Anayevuja  damu  usoni ni  binti  ambaye  amechanwa   nyembe  na Magreth  ( rafiki yake ) akimtuhumu  kutembea  na  mpenzi wake.

    JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI

    Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa donge nono la shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia na kuwadhuru watu kwa tindikali.
    Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova amesema: “Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa.” KWA KAULI HII YA JESHI LA POLISI, JE, NI KWELI KUWA JESHI LETU LIESHINDWA KAZI?