Tuesday, October 1, 2013

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa donge nono la shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia na kuwadhuru watu kwa tindikali.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova amesema: “Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa.” KWA KAULI HII YA JESHI LA POLISI, JE, NI KWELI KUWA JESHI LETU LIESHINDWA KAZI?

No comments:

Post a Comment