Tuesday, March 18, 2014

Dawa ya kuondoa Mistari, Michirizi, Mipasuko (Strech Marks) mwilini

Ukiangalia picha hizi utaelewa nazungumzia nini au namaanisha nini? 
ALAMA ZA MICHIRIZI KWENYE PAJA

Kabla hatujaangalia namna alama hizi zinavyotokea, tukumbushane sehemu muhimu za ngozi. Ngozi imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya nje (Epidermis), sehemu ya kati (Dermis) na sehemu ya ndani (Hypodermis).
Alama hutokea baada ya sehemu ya kati ya ngozi, dermis, kutanuka ghafla ndani ya muda mfupi kutokana na vitu kama mazoezi makali (kunyanyua vitu vizito), mtu kuongezeka uzito ghafla au obesity, pia kuna baadhi ya dawa au homoni (Glucocorticoids), ambazo kwa namna moja au nyingine huathiri tishu za kwenye ngozi na hivyo kupelekea mtu akapata alama za michirizi. Ujauzito kwa baadhi ya wanawake na pia mambo ya kurithi yameonekana kuchangia mtu kupata alama hizi katika ngozi yake.

Michirizi, mipasuko, mistari au kwa kitaalum Strech marks
inasababishwa na vitu vifuatavyo:-
- Ujauzito
- Kuongezeka kwa mwili (unene)
- Ukuaji wa haraka wakati wa kubalehe
- Mabadiliko ya mwili

Mpenzi msomaji, kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote, bali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani pindi anapokuwa mbele za watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.

Lakini hii hali inaweza kupotea kabisa iwapo utafanya mambo yafuatayo:-
1. Upakaji wa mafuta laini (Lotion) aina ya
Vaseline Intensive care tumboni katika kipindi chote cha
ujauzito kinasaidia kutopata tatizo hili.

2. Upakaji wa srub ya Apricot ni dawa ya haraka ya tatizo hili

3. Upakaji wa Mafuta ya Lavender mara 2 kwa siku yanaondoa
tatizo hili kwa muda mfupi sana
4. Mchanganyiko huu ni dawa nzuri na ya kuaminika,
ni vizuri ukihifadhi mchanganyiko wako ndani
ya Friji kwa kipindi chote cha matumizi.

- 1/2 kikombe cha olive oil
- 1/4 kikombe cha alove vera gel
- Majimaji ya vidonge 6 vya vitamini E
- Majimaji ya Vidonge 4 vya Vitamini A

Urusi yatambua Crimea kama taifa huru

Putin na Obama
Rais wa Urusi Vladmir Putin ametia saini ilani ya katiba inayotambua jimbo la Crimea kama taifa huru. Hatua hiyo inajiri muda mfupi baada ya marekani na Muungano wa Ulaya kutangaza vikwazo dhidi ya maafisa wa serikali ya Urusi na wa Ukraine waliohusika na njama ya Moscow kuiondoa Crimea katika Ukraine.
Rais Obama amesema kuwa anataka kuweka bayana kwamba kutakuwa na adhabu kwa wale walioanzisha mikakati ya Crimea kujitenga na Ukraine akiongeza kuwa vikwazo zaidi vitatolewa. Hata hivyo amesisitiza kuwa bado kuna njia ya kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya kidiplomasia.
Awali bunge la Crimea lilitangaza rasmi kuwa jimbo hilo liko huru kutoka kwa Ukraine na kutoa maombi ya kujiunga na mataifa yanayobuni muungano wa Urusi. Balozi wa Marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt, ameiambia BBC kwamba ilani iliyotiwa saini na rais Putin kutambua uhuru wa Crimea haitabadili mtizamo wa Marekani kuhusu hali ilivyo.
" Kadri marekani inavyozingatia, hapatakuwa na mabadiliko kuhusiana na makadirio yetu kuhusu hali, mtizamo wetu wa Crimea kama sehemu ya Ukraine iliyo huru na mtizamo wetu kuhusu kwamba kura ya maamuzi ya siku ya jumapili iliyofanyika baada ya uvamizi wa kijeshi uliotekelezwa na Urusi ni kinyume na sheria kwa vyovyote," anasema.
Mwanajeshi wa Ukraine karibu na jimbo la Crimea.
Msemaji wa Ikulu ya White House Jay Carney, alipoulizwa na waandishi wa habari ikiwa rais Putin atalengwa baadaye na vikwazo hivyo amesema kuwa Marekani haitawasaza baadhi ya watu katika uwezekano wa kuwawekea vikwazo.
"Uwezo wa kutoa vikwazo dhidi ya watu mbali mbali upo. Tutatoa tathmini kuhusu hatua mwafaka wakati hali ikiendelea kubadilika. Hatutawasaza baadhi ya watu. Kutakuwa na gharama kwa Urusi, Gharama ya ziada itakayotolewa kwa Urusi, ikiwa Urusi hatabadili mwelekeo hapa kuhusiana na jinsi inavyoshughulikia hali nchini Ukraine," anasema.
Miongoni mwa maafisa waliolengwa na vikwazo vya Marekani na Muungano wa Ulaya ni maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa jimbo la crimea, rais wa Ukraine aliyengolewa madarakani Viktor Yanukovich, naibu waziri mkuu wa Urusi, wabunge wa Urusi na makamanda wa jeshi.

Chanzo na BBC Swahili

BABU SEYA, PAPII FURAHA UPYA!

Na Elvan Stambuli na Haruni Sanchawa
MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.
Wakili Mabere Nyaucho Marando.
KASORO HUKUMU YA MWANZO Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika kesi ya Babu Seya na…

Na Elvan Stambuli na Haruni Sanchawa
MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.
Wakili Mabere Nyaucho Marando.
KASORO HUKUMU YA MWANZO Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar aligundua kuna vielelezo muhimu ambavyo havikuambatanishwa hivyo kuwa vigumu kwake kuviingiza na kuvitetea katika ngazi ya mahakama ya rufaa iliyoshindilia adhabu dhidi ya wawili hao.
Marando alisema mwanga mwingine wa kupitiwa upya wa mashitaka yao umekuja baada ya kuwepo kwa kesi mpya inayofanana na ya akina Babu Seya kwa asilimia mia moja. Alisema kesi hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo ushindi wake utamfanya apate nguvu ya kurudi mahakamani kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa mwaka 2004.
Nguza Viking ‘Babu Seya’ akiwa na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
DIRA KWENYE KESI HIYO “Kuna kesi mahakama kuu kanda moja nchini inayotetewa na wakili maarufu (jina tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri wake ina dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo. MAHOJIANO Mazungumzo kati ya Marando na Uwazi yalikuwa hivi:
Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko? Marando: Ni kweli, lakini ni jambo linalowezekana.
Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.
Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake inahusu nini? Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu Seya na wanawe. Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo hoja inapokuja, kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu Seya wengine viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi. Uwazi: Ukiwaandikia mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza ombi lako?

Marando: Hilo ni la mahakama lakini idadi inaweza kuongezwa na kufikia majaji sita au saba.Uwazi: Una hakika utashinda na kukubaliwa? Marando: Kama nilivyokueleza, ikipita ile kesi halafu mahakama ya rufaa wakakubali kupitia tena jalada, nina uhakika wa kushinda.
ANALIPWA NA NANI? Wakili huyo maarufu alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye kesi yao ikiwa katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada lenye kurasa 1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa na kifungo wateja wake.
“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa moja na wafungwa hao.
HUKO NYUMA Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe Papii Kocha, Mbangu na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.
Wakili Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwaremmy, Dar es Salaam.

MIAKA 10 YA... MATESO KITANDANI; Umaskini unaniua

HUJAFA hujaumbika. Hicho ndicho unachoweza kusema ukimuona na baadaye kumsikiliza Disnia Rajabu,32, mkazi wa mtaa wa Geza Ulole mkoani Tanga ambaye anaumwa uvimbe wa mguu kwa muda wa miaka 10 sasa bila kupata nafuu.
Disnia hakuzaliwa na tatizo hilo, bali alilipata ukubwani, tena akiwa tayari ameshaolewa, lakini katika hali ya masikitiko makubwa, anadai mumewe alimkimbia mara baada ya kugundua kuwa yupo katika majaribu makubwa kabisa katika maisha yake.
Na kutokana na kukimbiwa na mumewe, mwanamke huyo sasa anaishi na wazazi wake, ambao nao wana uwezo mdogo kiuchumi, hivyo licha ya kutopata matibabu ya uhakika, pia maisha yake yeye na watoto wake watatu ni ya kubahatisha, kwani mara kadhaa hukosa kula.
“Ni bora nisingezaliwa kwa mateso niliyonayo, sina raha…

“Ni bora nisingezaliwa kwa mateso niliyonayo, sina raha kabisa duniani kwani nina miaka kumi nipo kitandani, huwa nalia wanangu wanaponijia na kunililia kuwa wana njaa hawajui kuwa sina uwezo wa kuwatunza,” anasema mama huyo.
Akisimulia kuhusu mume wake, anadai walioana mwaka 2002 kwa ahadi ya maisha ya raha na shida, licha ya ukweli kwamba maisha yao yalikuwa ya chini, lakini alipopata ugonjwa huo, mwenzake alimkimbia bila kuaga na simu zake hazipatikani kila anapompigia.
“Nilizaliwa nikiwa mzima wa afya njema, mwaka 2004, usiku nikiwa nimelala, kichwa kiliniuma ghafla huku mwili wote ukitokwa na jasho, asubuhi kulipokucha, mwili ulikuwa umevimba.
“Nilichukuliwa hadi Hospitali ya Bombo, nililazwa siku saba, presha ilikua juu, niliwekewa dripu, nilichomwa sindano, presha ikashuka, uvimbe ulipungua isipokuwa mguu, madaktari waliniruhusu kwenda nyumbani ili nianze kliniki.
“Walinipima damu wakifikiri ni ugonjwa wa matende, walipogundua haukuwa huo, walinipa vidonge vya kutumia nyumbani lakini haikusaidia kwani nilikuwa napata maumivu makali sana huku mguu ukiendelea kuvimba,” anasimulia mama huyo kwa uchungu mkubwa.
Alisema hakuwa akipumua vizuri na mguu wake uliendelea kuvimba hadi alipojikuta akishindwa kutembea. Kuanzia wakati huo, akawa ni mtu wa kitandani, akila na kujisaidia hapo hapo. Ni wakati huo ndipo mumewe, ambaye hakumtaja jina alipoamua kumtoroka na kuwafanya wazazi wake kwenda kumchukua alipokuwa akiishi naye.
“Hali ilizidi kwa mbaya, wazazi wangu wakawa ni watu wa kulia tu, hawakuwa na uwezo, wakajiuliza jinsi ya kunileta Hospitali ya Muhimbili kwani baba ni kuli na mama yangu anapika na kuuza maandazi.”
Lakini anasema baadaye wazazi wake walipata wazo la kuomba msaada kwa watu na kufanikiwa kupata fedha zilizowatosha kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili, Februari mwaka jana.
“Nililazwa kwa muda wa wiki mbili, wazazi wakaambiwa wanichukue na kunipeleka hospitali moja ya binafsi ili nikapate kipimo ambacho pale Muhimbili hakipatikani kinachogharimu shilingi 470,000, walipigwa na butwaa, ilibidi wachukue picha yangu na kuanza kutembeza bakuli mtaani, Mungu akawasaidia wakapata hizo fedha.
“Walinichukua hadi hospitali hiyo, hata hivyo, haikugundulika kinachonisumbua, nilirejeshwa Muhimbili, daktari akanishauri nitafute pa kukaa ili niwe nahudhuria kliniki, sikuwa na ndugu Dar es Salaam, wazazi wakanirudisha nyumbani Tanga tukisubiri muda wa kwenda kliniki.
“Nililetwa Muhimbili mara mbili ndani ya wiki mbili, baadaye daktari alinieleza niendelee kukaa nyumbani nikisubiri muda wa kwenda India ambapo ugonjwa wangu ungeweza kujulikana na kupatiwa matibabu, sasa ni muda mrefu napata maumivu, nakaa nyumbani bila matibabu yoyote na haijulikani lini nitapelekwa nje kutibiwa.
“Baada ya kuona kimya muda mrefu,  tulimpigia simu daktari wangu wa Muhimbili ili kujua siku ya kwenda India, akajibu haijulikani kwani serikali haina bajeti, tulipouliza ni kiasi gani, wakasema zinatakiwa shilingi milioni 20.
“Nilipowaeleza wazazi waliinamisha vichwa chini na kuniambia nisubiri kufa, hakuna jinsi, nilitokwa na machozi nikatamani kujiua, sasa naleta ombi kwenu wananchi, naomba muokoe maisha yangu.
“Licha ya matatizo ya matibabu lakini hata njaa inanikabili, wazazi hawana uwezo, kuna wakati tunakosa hata chakula, nina watoto watatu nimetelekezewa na baba yao, naishi kwa kutegemea msaada wa kila kitu, nyumba ninaishi na wazazi wangu nusu ya paa imeezekwa kwa makuti na bati, imekuwa ikivuja wakati wa mvua,” alisema Disnia.
Kwa yeyote aliyeguswa na mateso ya mama huyu na ana nia ya kumsaidia awasiliane kwa namba 0755 033718, 0685 836159 au 0719 546505.

WOLPER: LAZIMA NIOLEWE NJE YA NCHI

Na Hamida Hassan
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.
Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.…

Na Hamida Hassan
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.
Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.
“Kule bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”

MTOTO ATESWA KWA WAYA NA MAMA WA KAMBO....

Na Haruni Sanchawa
MKE wa rais, mama Salma Kikwete alizungumza kweli kwamba, mtoto wa mwenzio ni wako! Lakini sivyo kwa mtoto Suleiman Riziki (4), mkazi wa Pugu Kinyamwezi, jijini Dar es Salaam ambaye amejikuta katika wakati mgumu kufuatia madai kwamba amekuwa akiteswa  na mama yake wa kufikia hadi kudhoofika afya.
Mtoto Suleiman Riziki (4) akiwa na makovu mwilini kutokana na kipigo.
Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Suleiman, mateso hayo yalikuwa yakitendwa na mwanamke huyo…

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Suleiman, mateso hayo yalikuwa yakitendwa na mwanamke huyo aliyemtambulisha kwa jina la Sharifa Kibwana.
Alisema mama huyo amekuwa akitumia waya wa umeme kumchapia mtoto wake mwilini hadi kumsababishia majeraha jambo ambalo hakuwa akilijua licha ya kuishi nyumba moja.
Katika mahojiano na Uwazi yaliyofanyika katikati ya wiki iliyopita nyumbani hapo,  baba huyo alisema tukio la kuumizwa kwa mtoto huyo liligundulika kwenye shule moja ya chekechea ambayo mtoto huyo anasoma.
Mtoto Suleiman Riziki akiwa na baba yake mzazi, Riziki Suleiman.
“Binafsi nilikuwa sijui kinachoendelea nyumbani mpaka mwalimu wake shuleni alipogundua,  lakini kweli alikuwa akipigwa halafu hasemi. Tatizo mimi huwa sionani na mwanangu kutokana  na muda ninaorudia,” alisema baba huyo.
Aliongeza kuwa, mtoto huyo akiwa shuleni alikuwa akilalamikia maumivu ya ndani kwa ndani hali iliyomfanya mwalimu wake kumvua nguo na kubaini majeraha hayo yaliyotokana na kupigwa.
Alisema ndipo mwalimu huyo alimtafuta na kumweleza, alipomwangalia akakutana na ukatili huo.
Akaendelea: “Hapa unapomuona mwanangu ana alama mwili mzima, da! Inauma sana!
“Huu ni ukatili ambao sitauvumilia hata kidogo, nimekwishachukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto wangu anapata matibabu na nimeshatoa taarifa polisi.”
Katika Kituo cha Polisi Stakishari kilichopo Ukonga, jijini Dar, Riziki alifungua jalada namba STK/RB/3146/2014
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
Mama huyo alipotafutwa kwa njia ya simu alikiri  kumchapa mtoto Suleiman lakini alisema hakutumia waya wa umeme kama inavyodaiwa.
“Suleiman ni mtoto anapokosa lazima achapwe na kisa cha kumchapa huwa anajinyea hovyo,” alisema mwanamke huyo.
Mwandishi alimtafuta Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Sophia  Simba ambaye ndiye mwenye dhamana na watoto, alipohojiwa kuhusu ukatili wanaofanyiwa watoto alisema:
“Inasikitisha sana. Tena sasa matukio hayo yanaongezeka siku hadi siku. Ndugu mwandishi huku ni kukosa maadili mema ya malezi maana mtu wa namna hiyo naye akumbuke alikuwa mtoto.
“Ni jambo la kushangaza na kusikitisha  kuona mama kama huyo anashindwa kumtunza mtoto wa mwenzake. Huyo ikibainika achukuliwe hatua za kisheria.”

Sunday, March 16, 2014

Ndege ya Malaysia iliyopotea toka week iliyopita inasemekana ilibadili mkondo 'Maksudi'

Marubani wawili waliokuwa wanaendesha ndege ya Malaysia
Mtambo wa mawasiliano wa ndege ya Malaysia iliyotoweka wiki moja iliopita, ulizimwa kwa maksudi.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.
Alisema kuwa ndege hiyo ilibadili mkondo na kuendelea kuruka kwa saa saba zaidi ya muda uliotakiwa kulingana na mawasiliano yaliyorushwa kwa Satelite na mtambo wa Radar.
Bwana Razak aliongeza kwamba hatua za ndege hiyo zinaambatana na matakwa ya mtu binafsi ambaye alikuwa akiielekeza.
Ngege hiyo ilitoweka wiki jana ikiwa imewabeba abiria 239.

Nusura bwana Razak aseme kuwa ndege hiyo ilitekwa nyara ingawa alisisitiza kwamba uchunguzi ungali unaendelea kubaini ilikokwenda ndege hiyo.

Dhana kwamba ndege hiyo ilitekwa nyara ilipingwa vikali awali lakini sasa inaonekana imerejea kuwa mojawapo ya sababu za kutoweka kwake.
Juhudi za kuitafuta ndege ya Malaysia bado zinaendelea
Mtambo wa mawasiliano wa ndege hiyo ulizimwa kwa maksudi na huenda marubani walifanya hivyo kwa hiari au kwa kulazimishwa.
Darubini sasa inawalenga watu waliokuwa wameabiri ndege hiyo na wafanyakazi wa ndege.
Wapelelezi watataka kujua ikiwa kumekuwa na tukio lolote la matatizo ya kiakili, changamoto za kifamilia na shinikizo la mawazo kwa yeyote aliyekuwa katika ndege hiyo, hasa marubani.
Ni wiki nne tu zimepita tangu rubani wa ndege ya Ethiopia kuiteka nyara ndege akitaka kupata hifadhi nchini Switzerland.
Marubani wa ndege hiyo ya Malaysia walikuwa na rekodi nzuri tu ya kikazi ingawa polisi bado wamefanya msako nyumbani kwao.
Chanzo BBC Swahili

Crimea yapiga kura kuamua iwapo jimbo hilo libaki Ukraine au lijiunge na Urusi

Wacrimea wakipiga kura ya maoniInaarifiwa kuwa upigaji kura unaendelea haraka Crimea katika kura ya maoni ya kuamua iwapo jimbo hilo libaki Ukraine au lijiunge na Urusi. Waandishi wa habari wanasema kuna kama sherehe wakati wa kupiga kura, huku bendera za Urusi na Crimea zikipepea na watu wanatakiana "siku njema ya kupiga kura'. Lakini piya kuna Wacrimea - pamoja na wale wa kabila la Tartar ambao ni asili-mia-12 ya watu wa Crimea - hao wanasusia kura. Huku nyuma kaimu waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema Urusi imekubali kuacha kuzingira makambi ya jeshi la Ukraine huko Crimea hadi Ijumaa, ambapo bunge la Urusi litaanza kujadili sheria ya kuungana na maeneo mapya.
Chanzo BBC Swahili