Tuesday, March 18, 2014

MTOTO ATESWA KWA WAYA NA MAMA WA KAMBO....

Na Haruni Sanchawa
MKE wa rais, mama Salma Kikwete alizungumza kweli kwamba, mtoto wa mwenzio ni wako! Lakini sivyo kwa mtoto Suleiman Riziki (4), mkazi wa Pugu Kinyamwezi, jijini Dar es Salaam ambaye amejikuta katika wakati mgumu kufuatia madai kwamba amekuwa akiteswa  na mama yake wa kufikia hadi kudhoofika afya.
Mtoto Suleiman Riziki (4) akiwa na makovu mwilini kutokana na kipigo.
Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Suleiman, mateso hayo yalikuwa yakitendwa na mwanamke huyo…

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Suleiman, mateso hayo yalikuwa yakitendwa na mwanamke huyo aliyemtambulisha kwa jina la Sharifa Kibwana.
Alisema mama huyo amekuwa akitumia waya wa umeme kumchapia mtoto wake mwilini hadi kumsababishia majeraha jambo ambalo hakuwa akilijua licha ya kuishi nyumba moja.
Katika mahojiano na Uwazi yaliyofanyika katikati ya wiki iliyopita nyumbani hapo,  baba huyo alisema tukio la kuumizwa kwa mtoto huyo liligundulika kwenye shule moja ya chekechea ambayo mtoto huyo anasoma.
Mtoto Suleiman Riziki akiwa na baba yake mzazi, Riziki Suleiman.
“Binafsi nilikuwa sijui kinachoendelea nyumbani mpaka mwalimu wake shuleni alipogundua,  lakini kweli alikuwa akipigwa halafu hasemi. Tatizo mimi huwa sionani na mwanangu kutokana  na muda ninaorudia,” alisema baba huyo.
Aliongeza kuwa, mtoto huyo akiwa shuleni alikuwa akilalamikia maumivu ya ndani kwa ndani hali iliyomfanya mwalimu wake kumvua nguo na kubaini majeraha hayo yaliyotokana na kupigwa.
Alisema ndipo mwalimu huyo alimtafuta na kumweleza, alipomwangalia akakutana na ukatili huo.
Akaendelea: “Hapa unapomuona mwanangu ana alama mwili mzima, da! Inauma sana!
“Huu ni ukatili ambao sitauvumilia hata kidogo, nimekwishachukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto wangu anapata matibabu na nimeshatoa taarifa polisi.”
Katika Kituo cha Polisi Stakishari kilichopo Ukonga, jijini Dar, Riziki alifungua jalada namba STK/RB/3146/2014
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
Mama huyo alipotafutwa kwa njia ya simu alikiri  kumchapa mtoto Suleiman lakini alisema hakutumia waya wa umeme kama inavyodaiwa.
“Suleiman ni mtoto anapokosa lazima achapwe na kisa cha kumchapa huwa anajinyea hovyo,” alisema mwanamke huyo.
Mwandishi alimtafuta Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Sophia  Simba ambaye ndiye mwenye dhamana na watoto, alipohojiwa kuhusu ukatili wanaofanyiwa watoto alisema:
“Inasikitisha sana. Tena sasa matukio hayo yanaongezeka siku hadi siku. Ndugu mwandishi huku ni kukosa maadili mema ya malezi maana mtu wa namna hiyo naye akumbuke alikuwa mtoto.
“Ni jambo la kushangaza na kusikitisha  kuona mama kama huyo anashindwa kumtunza mtoto wa mwenzake. Huyo ikibainika achukuliwe hatua za kisheria.”

No comments:

Post a Comment