Saturday, January 3, 2015

URAIS 2015: NYALANDU AKESHA AKICHEZA SEBENE!


Stori:Mwandishi wetu, Kibaha

WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi amefanya kufuru kubwa katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani baada ya kusakata sebene la Injili usiku wa manane.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiselebuka.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM), alifanya hayo juzi katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2015…
Stori:Mwandishi wetu, Kibaha
WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi amefanya kufuru kubwa katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani baada ya kusakata sebene la Injili usiku wa manane.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiselebuka.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM), alifanya hayo juzi katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2015 ambapo alipanda jukwaani na kusakata muziki huku akishangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Kuonesha msisitizo, Nabii Mwingira naye aliingilia jukwaani na kucheza muziki huo wa Injili huku akighani maneno ya Mungu kwa kutumia kipaza sauti alichokuwa nacho mkononi saa zote za hafla hiyo.
Mara baada ya saa sita na dakika 35 usiku kutimia Nyalandu ambaye alikuwa mgeni rasmi alikaribishwa kusema neno ambapo alipanda jukwaani na kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka mpya 2015.
Hata hivyo, alijipigia kampeni kwa kuwakumbusha waumini hao kuwa Oktoba mwaka huu Tanzania itakuwa na tukio kubwa, hivyo waumini hao kwake ni muhimu kwani wakati ukifika atawaomba kura zao.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na viongozi wa kanisa.
Naye Nabii Mwingira alisema mwaka 2015 anatamka wale wote ambao wapo kanisani hapo na wana dhamira moyoni mwao, watatimiziwa na Mungu wa Efatha.
“Huwa sisi hatuamini katika mashetani, tunaamini katika roho saba... hivyo natamka kwamba wote waliopo hapa na wana nia zao katika vifua vyao, basi Mungu atawapa,” alisema Mwingira huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya pili kwa Nyalandu kujipigia kampeni za urais kanisani, mara ya kwanza ni hivi karibuni katika jimbo lake alipokwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kijijini Ilongelo, Singida.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wa siasa waliozungumza na gazeti hili juzi jijini Dar walisema kuwa anachofanya Nyalandu ni kinyume na maadili ya chama chake ambacho kinakataza kutumia makanisa na misikiti kujipigia debe katika mambo ya siasa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Taifa wa CCM,  Nape Nnauye hakupatikana ili aweze kutoa maoni yake kuhusu vitendo hivyo kwani simu yake ilikuwa haipatikani.
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kutoka CCM ni Dk Hamisi Kigwangalla, Januari Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wengine wanaotajwatajwa ni Steven Wassira, Bernard Membe, Samwel Sitta na Edward Lowassa.  

NINGEKUWA MIMI NYALANDU, NISINGETANGAZA KUGOMBEA URAIS

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.
Kwako Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.

Najua uko bize sana kwa sasa ukiweka sawa mipango yako kuhakikisha mwaka huu unaingia ikulu katika uchaguzi mkuu ujao, najua itakuwa vigumu kwa ‘kapuku’ kama mimi kuonana na wewe ndiyo maana nimeamua kutumia ukurasa huu kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mheshimiwa, mimi sikuzaliwa Agosti 18, 1970 kama wewe wala sijawahi kusoma Shule ya Msingi Pohama, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha wala sijawahi kusoma Shule ya Sekondari ya  Illboru na kuhitimu kidato cha sita kama wewe.
Sijawahi kusoma vyuo mbalimbali…

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.

Kwako Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.
Najua uko bize sana kwa sasa ukiweka sawa mipango yako kuhakikisha mwaka huu unaingia ikulu katika uchaguzi mkuu ujao, najua itakuwa vigumu kwa ‘kapuku’ kama mimi kuonana na wewe ndiyo maana nimeamua kutumia ukurasa huu kufikisha ujumbe wangu kwako.

Mheshimiwa, mimi sikuzaliwa Agosti 18, 1970 kama wewe wala sijawahi kusoma Shule ya Msingi Pohama, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha wala sijawahi kusoma Shule ya Sekondari ya  Illboru na kuhitimu kidato cha sita kama wewe.
Sijawahi kusoma vyuo mbalimbali duniani kama University of Buckingham cha Uingereza, Wartburg College na Waldorf College, vyote vya Marekani kama wewe. Sijui chochote kuhusu uongozi wala siasa, niponipo tu, kapuku nisiye na mbele wala nyuma.

Hata hivyo, ningekuwa mimi katika nafasi yako, walahi nakuapia nisingepaza sauti yangu na kutangaza kwamba nataka kugombea urais kama ulivyofanya wewe hivi karibuni Katika Uwanja wa Ilongero, kwenye jimbo lako la Singida Kaskazini.
Najua ni haki yako ya msingi kugombea kama ilivyo kwa Mtanzania mwingine yeyote lakini nakuhakikishia, kama ungepata nafasi ya kujitathmini wewe kwanza, kuangalia udhaifu mkubwa uliouonesha tangu ulipokuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii hadi sasa ukiwa waziri kamili katika Wizara ya Maliasili na Utalii, usingethubutu kutangaza nia.
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyokumbwa na kashfa kibao za kudaiwa kushirikiana na kampuni za kigeni za utalii na uwindaji kuihujumu serikali kwa kujenga mazingira ya kukwepa kodi?

Umesahau jinsi ulivyohusishwa na kampuni ambayo inadaiwa una mgongano nayo wa kimaslahi ya Ahsante Tours, ikidaiwa ulishinikiza kampuni hiyo isamehewe mamilioni ya kodi mpaka TANAPA walipoikomalia ndiyo kodi ikalipwa?
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyoidhinisha ununuzi wa helikopta chakavu eti kwa ajili ya kukabiliana na ujangili, mwisho helikopta hiyo ikaanguka na kusababisha vifo vya marubani wetu wanne hivi karibuni?
Mheshimiwa, umesahau jinsi nchi yetu ilivyoingia kwenye doa kubwa kufuatia ujangili wa kupindukia na biashara ya meno ya tembo ilivyoshamiri kwa sababu ya wewe na wenzako kushindwa kutimiza majukumu yenu kwa umakini?
Vipi kuhusu marekebisho ya hovyo ya sheria ya uwindaji unayoshikia bango kwamba kipindi cha uwindaji kiongezwe kutoka muda wa miezi sita hadi tisa kwa manufaa ya wawindaji bila kujali uhifadhi na kuzaliana kwa wanyama wetu?
Madudu ambayo kwa namna moja au nyingine umekuwa ukidaiwa kuhusika nayo, ni mengi mno. Nikisema nitaje mojamoja, nitayajaza ukurasa mzima.

Hapana mheshimiwa, utendaji wako katika sehemu zote ulizopita, hauridhishi. Umekuwa ukionekana ‘mzigo’ kila unapopita achilia mbali jimboni kwako ambako kuna ahadi kibao ulizitoa wakati wa kampeni lakini mpaka sasa hujazitimiza.
Kama kuongoza jimbo lako la Singida Kaskazini na kuongoza wizara moja tu kumekushinda, utaweza kuongoza nchi? Ikulu ni mahali patakatifu mheshimiwa, waachie wenye uwezo watangaze nia ya kugombea lakini siyo wewe.

Friday, January 2, 2015

Mkesha wa Mwaka Mpya: Kila kona Uchaguzi Mkuu



Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali akiwaongoza wakazi wa Dar es Salaam kusherehekea Mwaka mpya katika Uwanja waTaifa, Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa, Saidi Mecky Sadiki na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya mkesha, Godfrey Mallase. Picha na Anthony Siame 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi


Kwa ufupi
Wakati viongozi wa dini wakijikita katika kuhamasisha haki kutendekea katika uchaguzi na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal aliwataka wananchi kuwatosa wagombea wote watakaotumia rushwa kuwashawishi wawachague.

Dar es Salaam. Ujumbe mahususi wa jinsi ya kushiriki na kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba ulitawala salamu za kuukaribisha mwaka 2015 zilizotolewa juzi na viongozi wa dini na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakati viongozi wa dini wakijikita katika kuhamasisha haki kutendekea katika uchaguzi na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal aliwataka wananchi kuwatosa wagombea wote watakaotumia rushwa kuwashawishi wawachague.
Salamu hizo zilianza kutolewa juzi wakati wa mkesha na Serikali ilitahadharishwa kuzingatia haki, usawa na demokrasia katika kusimamia uchaguzi huo ili kuepuka machafuko hasa katika kipindi cha uchaguzi huo.
Gwajima aonya
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima katika misa ya mkesha uliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe Dar es Salaam, alisema: “Ili nchi iendelee kuwa na amani, Serikali ihakikishe kuwa jeshi halitumiki katika hatua yoyote ile kuelekea uchaguzi mkuu.”
Pamoja na kauli hiyo inayolenga mpango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kutaka kutumia wanajeshi katika uandikishaji wapigakura, Gwajima alisema pia ili kulinda amani ya nchi matokeo ya uchaguzi yatangazwe kwa wakati na pasiwepo na wizi wa kura.
Alisema matumizi ya jeshi katika maandalizi na usimamizi wa uchaguzi ni mwanzo wa uandaaji wa mapinduzi kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwatamanisha na kuwaonyesha askari hao njia za kuingia Ikulu.
“Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, hakuna sababu zozote za kulihusisha jeshi katika harakati za uchaguzi na uwezekano ulio wazi ni kuwa mwitikio wa kujiandikisha unaweza usiwe mzuri kutokana na hilo. Lakini pia kama kuna viongozi waandamizi ndani yake ambao wanawaunga mkono baadhi ya wagombea wanaweza kutoa amri katika maeneo yao ufanyike upendeleo,” alisema.
Alisema hakutakuwa na maombi yatakayokuwa na msaada endapo matokeo ya uchaguzi hayatatangazwa kwa wakati kwa kuwa wapigakura watakuwa na shauku ya kujua hatima ya wale waliowachagua.
Katika mkesha huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, Gwajima aliwaeleza maelfu ya waumini waliohudhuria kuwa mwaka huu ni muafaka kwa ajili ya kuwaondoa wezi wote wa rasilimali za umma katika nafasi za uongozi ili Taifa linufaike na rasilimali lilizojaliwa.
Dk Slaa anena
Akiwahutubia waumini hao zaidi ya 70,000, Dk Slaa alieleza misingi muhimu itakayoifanya Tanzania isonge mbele huku kila mwananchi akinufaika na maendeleo husika.

AUNT: MUME WANGU HAJUI KAMA NINA MIMBA


www.maynesschapote.blogspot.com Stori:Musa mateja


Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.


Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’.
Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na…
Stori:Musa mateja
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.







Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’.
Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.
“Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.

JOKATE: DIAMOND HANA AKILI TIMAMU

Stori: Imelda Mtema
Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.
Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’.
MAHOJIANO
Katika mahojiano maalum ya hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Runinga ya GlobalTV Online chenye makao yake makuu ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge, Dar, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha kupata mtoto.
Alisema kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka nao kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na uvumba.

MZOZO MKUBWA
Hata hivyo, madai hayo ya Diamond yalizua mzozo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku warembo hao wakipigwa za uso hivyo kutafuta namna ya kujitetea.“Hao akina…(wanatajwa warembo wa Diamond) watakuwa wana matatizo ya uzazi siyo bure.
“Ndiyo maana Dangote (Diamond) ameona bora aende kwa Zari (msanii wa Uganda, Zarinah Hassan) ambaye tayari ana mwanga wa kuzaa (ana watoto watatu),” ilisomeka sehemu ya maoni juu ya madai hayo ya Diamond kwenye Mtandao wa Instagram.

SIKIA MADAI YA DIAMOND
Diamond alifunguka: “Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”

JOKATE AJIBU MAPIGO
Kufuatia tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa staa huyo wa Ngoma ya Ntampata Wapi inayokimbiza kwa sasa.
Jokate alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.

JOJO ASHUKA NA MISTARI
“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kwenda kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,” alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.
Wema akiwa na Diamond.
WEMA HATAKI MALUMBANO
Ukiacha Jokate na Wema ambaye naye aliwekwa kwenye kapu moja la kuchenga kumzalia, hakutaka kumjibu Diamond kwa kuwa hataki malumbano au makuu na mtu.

PENNY ALISHAJIBU
Pia jamaa huyo alimzungumzia aliyekuwa mwandani wake mwingine, Penniel Mwingilwa ‘Penny’ kuwa yeye alitoa mimba zake mbili kwa visingio tofauti. Katika majibu yake kupitia gazeti tumbo moja na hili, Risasi Jumamosi, toleo la wiki iliyopita, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.

Thursday, January 1, 2015

Ahsante sana wadau wangu mnao shiriki nami kikamilifu kusoma na kutoa maoni na mapendekezo katika Blog yangu. Ninawatakia mafanikio katika mwaka huu 2015 Kipekee ......

Ninamshukuru sana mwenyezi Mungu kwa ulizi wake Mkuu kwangu amenilinda mwaka Mzima uliopita 2014 mpaka sasa 2015. Ahsante sana wadau wangu mnao shiriki nami kikamilifu kusoma na kutoa maoni na mapendekezo katika Blog yangu. Ninajua kazi hii ni ngumu sana na ninakua nikipata wakati mgumu kutokana na ugumu wa majukumu niliyonayo. Inanipelekea wakati kutowapa taarifa mala kwa mala. Ninatamani kuwa nanyi kila siku lakini kuna wakati nazidiwa ila muamini kitu kimoja kuwa ninawapenda sana wadau wangu. Kipekee pia napenda kuishukuru sana Familia yangu kwa kunipa moyo na kuniombea katika magumu yote ninayo yapitia. Leo ninapenda kuwapa zawadi ndogo picha zangu ili mpate fahari ya macho. Pia ninawaomba msisite kutoa maoni kwani maoni yenu ndo yananijenga kurekebisha pale ninapo kosea.

Happy new year 2015 ndugu zangu. Nawapenda saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana
Utulivu kidogo

 Mapumziko kidogo


Na my dada

 Baba na watoto.

 Na rafiki yangu kipenzi

Nikiwa na My baba

 Ki kwetu kwetu

Dadaz na Mtoto

Nikiwa na dadaz

Hapa ni Dodoma na Bibi na Babu.
 
Burudani Dar es salaam

Mapumziko Mbeya moja




Weekend 


 Ofisi za watu

 Ibadani J2


 Nawapenda sana nina waahidi kuwapa habari na taarifa moto moto katika mwaka huu mpya 2015.