Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Kwa ufupi
Wakati viongozi wa dini wakijikita katika
kuhamasisha haki kutendekea katika uchaguzi na kuepuka vitendo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na Makamu wa Rais, Dk Mohamed
Ghalib Bilal aliwataka wananchi kuwatosa wagombea wote watakaotumia
rushwa kuwashawishi wawachague.
Dar es Salaam. Ujumbe mahususi wa jinsi ya
kushiriki na kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba ulitawala
salamu za kuukaribisha mwaka 2015 zilizotolewa juzi na viongozi wa dini
na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakati viongozi wa dini wakijikita katika
kuhamasisha haki kutendekea katika uchaguzi na kuepuka vitendo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na Makamu wa Rais, Dk Mohamed
Ghalib Bilal aliwataka wananchi kuwatosa wagombea wote watakaotumia
rushwa kuwashawishi wawachague.
Salamu hizo zilianza kutolewa juzi wakati wa
mkesha na Serikali ilitahadharishwa kuzingatia haki, usawa na demokrasia
katika kusimamia uchaguzi huo ili kuepuka machafuko hasa katika kipindi
cha uchaguzi huo.
Gwajima aonya
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji
Kiongozi, Josephat Gwajima katika misa ya mkesha uliyofanyika katika
viwanja vya kanisa hilo, Kawe Dar es Salaam, alisema: “Ili nchi iendelee
kuwa na amani, Serikali ihakikishe kuwa jeshi halitumiki katika hatua
yoyote ile kuelekea uchaguzi mkuu.”
Pamoja na kauli hiyo inayolenga mpango wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kutaka kutumia wanajeshi katika uandikishaji
wapigakura, Gwajima alisema pia ili kulinda amani ya nchi matokeo ya
uchaguzi yatangazwe kwa wakati na pasiwepo na wizi wa kura.
Alisema matumizi ya jeshi katika maandalizi na
usimamizi wa uchaguzi ni mwanzo wa uandaaji wa mapinduzi kwa kuwa
kufanya hivyo ni sawa na kuwatamanisha na kuwaonyesha askari hao njia za
kuingia Ikulu.
“Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, hakuna sababu
zozote za kulihusisha jeshi katika harakati za uchaguzi na uwezekano
ulio wazi ni kuwa mwitikio wa kujiandikisha unaweza usiwe mzuri kutokana
na hilo. Lakini pia kama kuna viongozi waandamizi ndani yake ambao
wanawaunga mkono baadhi ya wagombea wanaweza kutoa amri katika maeneo
yao ufanyike upendeleo,” alisema.
Alisema hakutakuwa na maombi yatakayokuwa na
msaada endapo matokeo ya uchaguzi hayatatangazwa kwa wakati kwa kuwa
wapigakura watakuwa na shauku ya kujua hatima ya wale waliowachagua.
Katika mkesha huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu
wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, Gwajima aliwaeleza maelfu ya waumini
waliohudhuria kuwa mwaka huu ni muafaka kwa ajili ya kuwaondoa wezi wote
wa rasilimali za umma katika nafasi za uongozi ili Taifa linufaike na
rasilimali lilizojaliwa.
Dk Slaa anena
Akiwahutubia waumini hao zaidi ya 70,000, Dk Slaa
alieleza misingi muhimu itakayoifanya Tanzania isonge mbele huku kila
mwananchi akinufaika na maendeleo husika.
No comments:
Post a Comment