Saturday, January 3, 2015

NINGEKUWA MIMI NYALANDU, NISINGETANGAZA KUGOMBEA URAIS

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.
Kwako Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.

Najua uko bize sana kwa sasa ukiweka sawa mipango yako kuhakikisha mwaka huu unaingia ikulu katika uchaguzi mkuu ujao, najua itakuwa vigumu kwa ‘kapuku’ kama mimi kuonana na wewe ndiyo maana nimeamua kutumia ukurasa huu kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mheshimiwa, mimi sikuzaliwa Agosti 18, 1970 kama wewe wala sijawahi kusoma Shule ya Msingi Pohama, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha wala sijawahi kusoma Shule ya Sekondari ya  Illboru na kuhitimu kidato cha sita kama wewe.
Sijawahi kusoma vyuo mbalimbali…

Sijawahi kusoma vyuo mbalimbali duniani kama University of Buckingham cha Uingereza, Wartburg College na Waldorf College, vyote vya Marekani kama wewe. Sijui chochote kuhusu uongozi wala siasa, niponipo tu, kapuku nisiye na mbele wala nyuma.

Hata hivyo, ningekuwa mimi katika nafasi yako, walahi nakuapia nisingepaza sauti yangu na kutangaza kwamba nataka kugombea urais kama ulivyofanya wewe hivi karibuni Katika Uwanja wa Ilongero, kwenye jimbo lako la Singida Kaskazini.
Najua ni haki yako ya msingi kugombea kama ilivyo kwa Mtanzania mwingine yeyote lakini nakuhakikishia, kama ungepata nafasi ya kujitathmini wewe kwanza, kuangalia udhaifu mkubwa uliouonesha tangu ulipokuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii hadi sasa ukiwa waziri kamili katika Wizara ya Maliasili na Utalii, usingethubutu kutangaza nia.
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyokumbwa na kashfa kibao za kudaiwa kushirikiana na kampuni za kigeni za utalii na uwindaji kuihujumu serikali kwa kujenga mazingira ya kukwepa kodi?

Umesahau jinsi ulivyohusishwa na kampuni ambayo inadaiwa una mgongano nayo wa kimaslahi ya Ahsante Tours, ikidaiwa ulishinikiza kampuni hiyo isamehewe mamilioni ya kodi mpaka TANAPA walipoikomalia ndiyo kodi ikalipwa?
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyoidhinisha ununuzi wa helikopta chakavu eti kwa ajili ya kukabiliana na ujangili, mwisho helikopta hiyo ikaanguka na kusababisha vifo vya marubani wetu wanne hivi karibuni?
Mheshimiwa, umesahau jinsi nchi yetu ilivyoingia kwenye doa kubwa kufuatia ujangili wa kupindukia na biashara ya meno ya tembo ilivyoshamiri kwa sababu ya wewe na wenzako kushindwa kutimiza majukumu yenu kwa umakini?
Vipi kuhusu marekebisho ya hovyo ya sheria ya uwindaji unayoshikia bango kwamba kipindi cha uwindaji kiongezwe kutoka muda wa miezi sita hadi tisa kwa manufaa ya wawindaji bila kujali uhifadhi na kuzaliana kwa wanyama wetu?
Madudu ambayo kwa namna moja au nyingine umekuwa ukidaiwa kuhusika nayo, ni mengi mno. Nikisema nitaje mojamoja, nitayajaza ukurasa mzima.

Hapana mheshimiwa, utendaji wako katika sehemu zote ulizopita, hauridhishi. Umekuwa ukionekana ‘mzigo’ kila unapopita achilia mbali jimboni kwako ambako kuna ahadi kibao ulizitoa wakati wa kampeni lakini mpaka sasa hujazitimiza.
Kama kuongoza jimbo lako la Singida Kaskazini na kuongoza wizara moja tu kumekushinda, utaweza kuongoza nchi? Ikulu ni mahali patakatifu mheshimiwa, waachie wenye uwezo watangaze nia ya kugombea lakini siyo wewe.

No comments:

Post a Comment