Monday, August 11, 2014

Gazeti la leo tarehe 11 Agosti Michezo ARSENAL BINGWA NGAO YA JAMII

Arsenal wakiwa na Ngao ya Jamii baada ya kuipiga Manchester City 3-0.
Santi Carzola akishangilia bao lake la kwanza kwa Arsenal.
Aaron Ramsey akifunga bao la pili kwa Arsenal.
Bao la tatu la Arsenal lililofungwa na Olivier Giroud.

Raha ya ushindi.
KLABU ya Arsenal imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Manchester City mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Wembley jijini London usiku huu. Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Cazorla 21, Ramsey 42 na Giroud 60.

Friday, June 6, 2014

Boko Haram wafanya mauaji: zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.

Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.

Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.

'Jeshi lakanusha madai'
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
nyumba zimechomwa Borno 

Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.

Chanzo BBC Swahili

Morogoro: Gari aina ya Prado laacha njia na kuvamia bank ya CRDB jana mapema

Gari aina ya Prado limeacha njia na kupamia bank ya CRDB Mkoani Morogoro. tukio hilo lilitokea mapema sana jana. Ajali hiyo imetokea wakati mmoja wa wafanyakazi wa hapo (Jane Maganga) akipaki gari yake, gari ilipitiliza na kuingia ndani. Hakuna mtu aliye umia katika ajali hiyo.

 Picha ya gari lililo pamia bank


Sehemu iliyogongwa

Wednesday, June 4, 2014

Ukatili unazidi kuendelea: Mwanamke mmoja jina lake halijaweza kufahamika. Amediliki kumuua mtoto na kumtupa barabarani...

Mwanamke mmoja asiyefahamika jina wala sehemu anayoishi amefanya tendo la kinyama kwa kumuua mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike kwa kumfunga plasta puani na mdomoni hali iliyompelekea mtoto huyo kushindwa kupumua na kupoteza maisha. Tukio hilo la kikatili limekutwa pembezoni mwa barabara ya Kawe Beach Jiji Dar es salaam


Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembeni ukiwa na damu hali iliyowashangaza wakaamua kuusogelea na kukuta kichanga hicho kimefungwa na plasta mdomoni na puani kikiwa kimeshafariki.


Tuesday, May 20, 2014

Hatimaye Msanii Adam Philip azikwa leo katika viwanja vya Kinondoni.


Mwingizaji huyu mwenye umri wa miaka 38 alifariki ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar.Kifo chake kilitokea  akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. 

 Marehemu Adamu Enzi za uhai wake


Chanzo cha kifo chake inasemekana ni vidonda vya tumbo ambao msanii wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti,  Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu.
Gari lililo beba mwili wa Marehemu kuelekea nyumbani kwake Bunju

Waombolezaji wakilia kwa majonzi


 Mwili wa Marehemu ukitolewa kuajili ya kupelekwa Leaders kuajili ya kuaga

 Baadhi ya wasanii wakiomboleza


Wasanii wameubeba mwili wa Marehe

 Wakijiandaa kuupokea mwili wa marehem

Mwili ukitolewa kwenye gari



Msanii Steve akilia kwa kuondokewa na mpendwa wao


Hivyo ndivyo Adam Philip alivyo tutoka. Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaindi. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahara pema Amina.





Saturday, May 10, 2014

RAY C ASIMULIA ALIVYOKICHUNGULIA KIFO


Stori: MUSA MATEJA

MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye…
Stori: MUSA MATEJA
MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.