Monday, October 7, 2013

Libya yataka Marekani ijieleze


Pwani ya Tripoli, Libya
Wakuu wa Libya wametaka maelezo kutoka Marekani, baada ya mtu anayedaiwa kuwa mfuasi wa al-Qaeda kutekwa mjini Tripoli na makamando wa Marekani.
Mwanamme huyo, Anas al Libi, alikuwa anasakwa kwa kuhusika na mashambulio dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania miaka 15 iliyopita.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema Anas al Libi sasa anazuwiliwa nje ya Libya.
Kaka ake amesema kukamatwa kwake kulikuwa kitendo cha uharamia.
Jumamosi makamando wa Marekani piya walishambulia nyumba mjini Barawe, Somalia, ambayo inadaiwa kutumiwa na kiongozi mmoja wa kundi la al-Shabaab aliyehusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi, lakini walishindwa kumpata.
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, amesema kuwa mashambulio hayo mawili yanaonesha dhamira ya serikali ya Marekani kuwasaka wale wanaohusika na ugaidi.

Taarifa na BBC Swahili

No comments:

Post a Comment