Tuesday, October 8, 2013

Maumivu ya Moyo yanaweza sababishwa na kitu chochote kinacho weza kukufanya upate maumivu.

Rose ni binti anayeishi na wazazi wake katika Mkoa wa Iringa mji mdogo wa Mafinga Kinyanambo. Walipokuwa wakila chakula alipokea simu na haikujulikana ya nani na nini kilitokea Leo tunaendelea.....


Baada ya Rose Kuzinduka aliendelea kulia mama yake alipo uliza kunani Rose alijibu kwa husuni Joel, mama aliposikia hivyo alishituka pia. Joel ni kijana anayeishi mjini Dar-es-salaam ni mchumba wa rose ambaye walipanga kuoana siku chache zijazo pia walishakua wamemaliza hatua zote za kufanya ajulikane ni mumewe mtalajiwa. Mama aliendelea kuuliza ili apate kujua ukiundani zaisi. 
"Mama Joel yupo kituo cha polisi na inaonekana hana hali nzuri kwani amepata ajali, kinachoniliza zaidi inasemekana alikua akisafilisha madawa ya kulevya kuelekea South Africa ndipo wakapata ajali na kupelekwa kitu cha polisi" Alisimulia Rose huku akili kwa uchungu mama alijitahidi kumbembeleza Rose lakini hakuelewa. 

Siku ilipita kesho yake Rose aliamua kusafiri kuelekea Dar-es-salaam kujua vyema mambo yaliyotokea. Aliwasili mnamo saa 10 jioni hakutaka kupumzika na kwenda moja kwa moja katika kituo cha police alicho elezwa. Alipofika akajieleza na polisi wakamruhusu aingie kumwona mtuhumiwa ambaye alidaiwa kuwa ni mchumba wake. Alipofika ndani alishitushwa kumkuta mtu anaye oneshwa si yeye. Rose alishangaa na kuwaeleza polisi kuwa huyo siye lakini polisi walimuhakikishia kuwa mwenye simu ile ndiye huyo. Baada ya Maelezo hayo yule mtuhumiwa alijaribu kusema ukweli kuwa simu hiyo si yake kuna gari walilogongana nalo ndio simu hiyo ilitoka nae kwakua na shida akaichukua na kuifanya yake na hakua anamfaham mwenye simu. Rose alizidi kuchanganyikiwa kusikia hivyo kwani alihisi kabisa Joel amefariki dunia. Alikimbia hospitali ya Muhimbili na kumkuta Joel katika wodi ya watu mahututi akiwa hawezi kuongea na akipumlia mipira uso wake ukiwa hautamaniki kwa dam na uvimbe. Rose aliwapigia simu ndugu na jamaa wa karibu wakiwemo wazazi wake na kuwaeleza ukweli wa mambo ulivyo. Alienda kuonana na Dacktari wa mifupa akaambiwa mgonjwa wake amepata shida kubwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji na kutolewa figo 1. hapo Rose alizidi kuhisi maisha ya Joel yanaishia hapo. Madaktari walipanga kumwingiza kwenye chumba cha upasuaji saa 3 asubuhi ya siku inayofuata. 

Masaa alisogea hatimaye kukakucha. Joel aliandaliwa kwa ajili ya kuingia chumba cha upasuaji (Machinjioni). Rose alisali kila dakika kumwomba Mungu amponye mpedwa wake. Mda ulifika hatimaye Joel akaingizwa chumba cha upasuaji. Rose akiwa nnje ya chumba aliendelea kusali masaa yalizidi kusonga mbele masaa mawili aliisha bila mtu yeyote kutoka nnje wala kuingia ndani ya chumba hicho. Baada ya dakika kadhaa alitoka Muuguzi mmoja akionekana kuwa na haraka sana na kukimbia kama mtu anayefuata kitu au anaye mkimbilia mtu furani. Rose alijalibu kumsimamisha lakini hakumsikiliza. Baada ya muda kidogo yule muuguzi alirudi tena na Rose alipo msimamisha alijalibu kumsikiliza lakini akiwa anatembea kwa kasi sana. 
"Dada samahani mgonjwa wangu vipi?"
"Samahanani anaonekana katokwa sana na damu nyingi sana tumwombe Mungu kwa bado madaktari wanaendelea na upasuaji"
Rose alikaa chini taratibu huku akimtaja mungu wake. Mala dactari alitoka na kuonekana kama mtu aliye kata tamaa vile. Rose hakuweza hata kumsogelea kwani hakuwa na nguvu tena .... Je Joel yupo katika hali gani na Dactari ana kipi cha kumweleza Rose. Tutaendelea keshoooooooo. Na Mayness Chapote

No comments:

Post a Comment