Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan amezitaka nchi za
Magharibi kuisaidia kukomessha kuenea kwa makundi ya wapiganaji wenye
ikitadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC Bwana Zeidani alisema kuwa Libya inatumika kama sehemu ya kusambazia silaha katika kanda nzima.
“Hizi silaha zinapelekwa kwa wingi
katika nchi jirani kwa hivyo lazima pawepo ushirikiano wa kimataifa
kukomesha jambo hilo,’’ alisema bwana Zeidan.
Mnamo siku ya Jumatatu serikali ya Libya
ilimhoji balozi wa Marekani nchini humo kuhusu kukamatwa kwa mshukiwa wa
ugaidi na mmoja wa viongozi wa kundi la al-Qaeda mjini Tripoli.
Anas al-Liby, alikuwa anasakwa kwa kuongoza
mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na
Tanzania mwaka 1998 na baada ya zaidi ya miaka kumi aliweza kukamatwa
mjini Tripoli na makomando wa Marekani.
Marekani imetetea hatua ya kukamatwa kwa gaidi huyo ikisema kuwa kilikuwa kitendo halali kuambatana na sharia za kimataifa.
Lakini bunge la Libya Jumanne lilitaka al Liby
kurejeshwa nchini humo likitaja kukamatwa kwake kama kitendo cha utekaji
nyara na kupuuza utawala wa Libya.
Rais Barack Obama aliambia waandishi wa habari
Jumanne kuwa Marekani ina ushahidi wa kutosha kuonyesha kua Al Liby
alipanga na kusaidia katika kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini
Marekani na kuwaua watu wengi sana.
Obama aliongeza kuwa Al Liby atafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.
No comments:
Post a Comment