Takriban watu 30 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa kwenye makabiliani katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa wanasema kuwa makabiliano yalizuka kati
ya waliokuwa waasi na makundi ya kiraia ya ulinzi siku ya Jumatatu na
kuendelea hadi Jumanne.
Duru zinaarifu kwamba makundi hayo
ya kiraia ambayo hutoa ulinzi kwa raia, yalishambulia kijiji cha Garga
kilicho umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu Bangui.
Nchi hiyo masikini, imetokomea kwenye ghasia
tangu waasi waliokuwa wanaongozwa na rais Michel Djotodia kumwondoa
mamlakani mtangulizi wake Francois Bozize mwezi Machi.
Raia katika kijiji cha Garga, walithibitisha
kuwa mapigano yalizuka na kusababisha hadi vifo 60 huku baadhi ya
taarifa zikisema kuwa wenyeji wa kijiji hicho walimalizwa.
Mwanzo taarifa zilisema kuwa wenyeji walishambuliwa na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa rais aliyeondolewa mamlakani.
Waasi kutoka kundi la Seleka lililomwondoa
mamlakani aliyekuwa Rais Bozize waliingia kijijini humo na kuanza
kuwatafuta waasi hao . Raia mmoja alisema aliona miili ya watu 40 na
hakuna hata afisaa mmoja wa Seleka alikuwa miongoni mwa waliofariki.
Waasi wa Seleka waliohusika kwenye mapigano hayo
walijumuisha wapiganaji kutoka nchi jirani ya Sudan , kwa mujibu wa
taaifa za wenyeji.
Hata hivyo rais mpya aliwasihi wapiganaji wengi
kusalimisha silaha na kuingia jeshini lakini waasi wa Seleka wamekuwa
wakiendelea kufanya mashambulizi na kusababisha vijana kuanza kutoa
ulinzi kwa raia.
Waasi hao ambao hawana mafunzo ya kijeshi
wamekuwa wakidaiwa kupora kutoka katika vituo vya afya na kuwaibia raia
mali zao tangu Rais Djotodia kuingia mamlakani.
Rais huyo ameahidi kuondoka mamlakani baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2016.
Taarifa BBC Swahili
No comments:
Post a Comment