Miongoni
mwa vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu ni kupata furaha. Watu wengi
wamekuwa na harakati nyingi za kuhakikisha kuwa wanafurahika katika
kuishi kwao. Kuna wanaotafuta furaha kupitia kwa rafiki, wapenzi, ndoa
zao na hata jamii zao. Ni wazi kwamba kila afanyalo mwanadamu kupitia
maamuzi yake, msingi wake huwa ni kutafua furaha, hii haijalishi kama atafanya jambo mbaya au zuri kwa mtazamo wa watu.
Ifahamike,
watu wanavuja jasho katika kufanya kazi kwa sababu wanahitaji mshahara
au pato ambalo baadaye hulitumia katika kufurahi. Wasomi,
wafanyabiashara nao wanapohangaka katika hili na lile ukichunguza
utakuta nyuma yao kuna kiu ya furaha.
Hii
ina maana kuwa, furaha ndiyo jambo pekee ambalo watu hulitafuta zaidi.
Ni nadra au pengine hakuna mtu ambaye kwa akili timamu ana kiu ya kupata
mabaya na kuhangaika kuyatafuta. Mara nyingi yakimtokea basi huwa
yamejitokeza tu katika safari yake ya kutafuta furaha. Wezi, majambazi,
wazinifu hata watukanaji wote kwa pamoja wanapofanya hivyo huwa nyuma yao kuna hitaji la kupata furaha.
Pamoja
na shabaha ya binadamu kuwa katika kutafuta furaha, wengi wao wamekuwa
hawaipati kwa sababu hawajui njia za kuipata. Kuna watu wanahangaikia
utajiri, wakidhani wakiupata, basi watakuwa na furaha, lakini baada ya
kupata utajiri huo hujikuta hawana furaha. Wengine huamua kuoa, kuwa na
wapenzi na marafiki lakini nao matokeo huwa tofauti na malengo.
Ingawa
kuna matatizo mengi ambayo yanajitokeza katika maisha ya watu kila siku
ambayo huondoa furaha, lakini si sababu ya moja kwa moja ya kumfanya
mtu ahuzunike, eti tu kwa maana kafikwa na tatizo. Ukichunguza kwa
makini utafahamu kuwa furaha si kitu ambacho mtu anaweza kukipata na
kikamtosha. Unaweza kupata kila kitu lakini ukawa huna furaha.
Ukisema
pesa ndiyo furaha, unaweza kuzipata lakini usifurahike na ukashangaa
watu ambao ni masikini wakawa na furaha tele. Hivyo basi msingi wa
furaha ni uelewa wa namna ya kuitafuta na kuipata. Swali, furaha
inapaika wapi na katika vitu gani? Nibu ni kuishi kwa kuzingatia
muongozo ufuatao:
Unaitafutaje furaha?
Watu
wengi wanapopata matatizo huwa hawakubali kuyapokea. Kuna mfano wa mtu
mmoja ambaye alikuwa bosi katika kampuni, siku moja uongozi wa juu
uliamua kumshusha cheo kutoka ukurugenzi hadi mpokea wageni. Bosi huyo
alipotelemshwa cheo kwa kiwango hicho hakujiona duni kwa wafanyakazi
wenzake, badala yake alichofikiri yeye ni kwamba watu wote wanamuunga
mkono na kumsikitikia kwa unyama huo wa kushushwa cheo kupitiliza.
Zile
fikra za kuhurumiwa na watu zilimfanya awe na furaha na akawa mtu wa
kuwahi kazini kila siku ili watu wakamuone na kumsikitia, jambo ambalo
aliamini kuwa uongozi uliomshusha cheo ndiyo unaopata aibu mbele ya
jamii na wala sio yeye. Kitendo hicho cha kuwahi kazini na kuonekasna ni
mtu mwenye furaha kilimfanya awe mtu wa pekee kwenye jamii, aliweza
kutengeneza maswali mengi kwa watu na hatimaye minong’ono ya kuonewa
ilianza kusikika.
Kilichotokea
hatimaye, kampuni moja kubwa ilipata habari ya kuwepo kwa mtu wa aina
hiyo, ikafanya mawasiliano naye na kumwajiri, bila kujali kashfa
zilizokuwa zimemwengua katika wadhifa wake wa kwanza. Jamaa huyo
alipopata ajira mpya alijirekebisha makosa yake ya kugushi na wizi kwa
vile alikuwa amejifunza kilichokuwa kimempata. Bosi huyo aliweza
kuendesha kampuni hiyo kwa mafanikio makubwa, jambo lililowafanya wakuu
wake wa zamani wajute kumuondolea wadhifa.
Hapa
tunajifunza kuwa tunapopata matatizo kinachotufanya tupoteze furaha ni
fikra zetu, lakini tukijua kucheza nazo na kuzielekeza katika mlango wa
pili, tunaweza kuyatumia matatizo yetu kupata furaha pia. Lazima kila
mmoja wetu atambue kuwa matatizo ni shule, tunapoyapata tunajifunza.
Lakini hatuwezi kujifunza tukiwa na msongo wa mawazo, lazima tufanye
unafiki fulani wa kimawazo kama
alioufanya bosi aliyeshushwa cheo, yeye hakuangalia wadhifa wake wa
zamani, wala namna gani watu wanamtazama katika kazi yake mpya. Mawazo
yanawezaje kutuletea furaha?
Katika
hali ya kawaida hakuna mtu hata mmoja anayeweza kumwambia mwenzake lia
naye akafanya hivyo. Kila siku tunaona na kusikia mengi kutoka kwa
ndugu, rafiki, waalimu wahubiri, wachungaji mapadri wetu na hata kwenye
vyombo ya habari, lakini kusikia huko hakuna maana kuwa ni lazima
kutuondolee furaha, kwani ndani ya akili zetu kuna kitu muhimu ambacho
ni maamuzi yetu.
Utawala
wa mawazo yetu ni kazi ya kila siku na uamauzi wa nini ha kufikiri ni
suala ambalo lipo kwenye uwezo wa mwanadamu mwenyewe. Ingekuwa ni lazima
kila wazo baya tunaloliona na kulisikia lazima lituhuzunishe basi
tusingekuwa na furaha hata kidogo katika maisha yetu, kwani hakuna siku
ambayo itapita bila kuona, kusikia au kutendewa jambo baya na mtu
mwengine.
Ajali
zinatokea kila siku, watu wanakufa, wanaugua, wanateseka, wanalia,
wanaomboleza na kufanyiana hila, lakini kwa nini hatuyachukulii matukio
yote kwa uzito sawa kiasi ha kulia? Ni kwa sababu tuna uhuru wa kuchagua
tulie kwa sababu ya nani na kwa nina? Na hii ndiyo silaha pekee ya
kuyatumia mawazo kutuletea furaha. Yaani kuchagua lipi la kutuliza na
lipi la kutufurahisha na mwisho wa yote tuna uwezo wa kuyatumia mawazo
yetu kuchagua mambo ya kufurahisha na kuyapa kipaumbele, bila kujali ni
mema au mabaya. (Kumbuka mfano wa bosi aliyeshushwa cheo).
Hivyo ni vema wakati tunapokuwa na mawazo ndani yetu tukazingatia misingi ifuatayo ambayo inaweza kutusaidia kufikia uamuzi sahihi juu ya kila tunaloona na kulisikia, ili mawazo yasitufanye tuhuzunike na badala yake tufurahi. Kwanza ni kujipenda wenyewe. Tukijipenda hatutajihukumu na kujiona duni mbele ya wenzetu na hivyo kutopoteza furaha. Pili ni kujiamini, kuamini huku kutatuwezesha kuwa na msimamo juu ya maamuzi ya kila tunachoshibishwa ndani ya mawazo yetu kupitia mawasilia ya sauti na yasiyo na sauti.
Tatu, kumiliki mawazo yetu yasichukuliwe na ukubwa au udogo wa tatizo. Udhibiti huu lazima uyaone mambo yote yanayoingia kichwani kuwa ni ya kawaida kwa vile yapo duniani na yanawakuta watu kama sehemu ya changamoto za kimaisha. Katika hali ya kawaida ukubwa au udogo wa tatizo unatokana na mawazo ya mtu husika. Nne, kuwa na uvumilivu juu ya kila jambo kwa imani kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tano na mwisho ni kuhakiki maamuzi yetu kama yako sahihi kabla na baada ya kutenda jambo.
Kutojiheshimu kunavyohatarisha furaha yetu?
Ni muhimu kila mtu akaishi kama
yeye alivyo, lakini linapokuja suala la kuchangamana na ulimwengu,
lazima kuwe na kitu cha kujifunza kwa sababu huwezi kuishi nje ya
familia na watu wengine.
Kwa
msingi huo ili mtu aweze kupata furaha lazima afahamu namna
atakavyoweza kujisahihisha tabia yake kwa kujiheshimu yeye na
kuwaheshimu wengine anaoishi nao. Kwa maana kuishi kama
mtu anatakavyo bila kutazama wengine ni jambo baya. Hivyo dokezo
zifuatazo ni muhimu kwa kila mtu kuzifahamu ili kuondoa mkwaruzano kati
ya mtu na mtu.
A –Wafanyie wengine mema
Furaha haiwezi kuja kama
mtu hajiheshimu mwenyewe na kuwafanyia wengine mema ambayo angependa
atendewe. Watu wengi wamekuwa hodari kutembea na wake za watu, kuiba,
kudhuru, kutukana, kudharau wengine na hata kunyanyasa, bila kugeuza
upande wapili wa shilingi na kufikiri endapo wangefanyiwa wao hali
ingekuwaje, si wangepoteza furaha? Sasa kama jibu ni ndiyo kwa nini wao
wawe mahodari kuwaumiza wengine? Ni wazi kwamba kila mwanadamu angekuwa
makini kufanya yale ambayo angependa kufanyiwa, kiwango ha huzuni
kingepungua, na hii ndiyo changamoto kubwa kwa mtu atakaye kupata furaha
lazima awafanyie wengine wema kwanza kabla ya yeye kufanyiwa.
B – Kuwa kiongozi
Katika maisha kuna watu ambao hawaelewi kuhusu matumizi ya mawazo na namna ya kutenda kama
binadamu, hivyo kwa wale ambao wanaelewa nini maana ya maisha ni vema
wakawa viongozi kwa wengine, viongozi katika kusamehe, kukubali kosa,
kutenda haki na kusimamia ukweli.
C- Kushukuru
Ni watu wachache sana
ambao hushukuru wafanyiwapo mabaya, lakini inashauriliwa kwamba ili
kuuita furaha na kupunguza nguvu ya huzuni ni bora mtu akajifunza
kushukuru hata kama amefanyiwa jambo baya.
D - Kuwa na juhudi
Mambo
yote tunayoyafanya lazima yaambatane na juhudi. Ikiwa tunatafuta majibu
ya nini tunataka kifanyeke katika kupata furaha lazima tuwe na bidii,
tusifanye vitu kwa uzembe kwani matokeo yake ni kushindwa ambako
kutatuingiza katika shida ambazo zitatuhuzunisha. Umeolewa jitahidi
kulinda ndoa yako, jitahidi katika kazi na kila jambo ili usikwame.
E- Kuchunga ulimi
Kuna
watu wengi ambao wanapoteza furaha kwa kutojua namna ya kutumia ndimi
zao. Utakuta mtu yuko katika kati ya watu, anatukana na wakati mwingine
kutamka maneno ambayo wenzake hayawapendezi. Kujiheshimu ni pamoja na
kuchuja maneno ya kusema mbele za watu kulingana na mahitaji yaliyopo,
kuropoka ropoka kuna madhara. Kabla hujasema kitu tafakari kama usemecho kitaleta furaha au huzuni.
Kanuni za kuifikia furaha ya kweli
Wakati wa kutafuta furaha ya kweli lazima kujiuliza baadhi ya kanuni za kimaisha kama
unazifuata kwa ufasaha, vinginevyo unaweza kuwa mtafuta furaha lakini
usiwe miongoni mwa wanaoipata. Kama nilivyosema awali kuwa, kuna watu
hutafuta furaha kupitia kwa wake/waume zao, rafiki, wapenzi na hata
kwenye mali, lakini mwisho wa siku wanapokuja kutafakari zaidi hujikuta hawana furaha waliyoitaraji wakati wakihangaikia njia za kuipata.
Kuna watu ambao mawazo yao yanatamani sana kupata mtoto na wengine wameapa kabisa kwamba wakifanikiwa kushika ujauzito watakuwa na furaha, lakini bado kama
hawatakuwa makini wao wenyewe watajikuta wanapata furaha ya muda na
hatimaye kutoweka na kuanza kujutia harakati zao, huku wakianza safari
mpya za kufuata furaha kupitia jambo jingine. Hebu tujiulize maswali
haya.
A-Je tunapokuwa
tunatafuta furaha tunatumia uwezo wetu wote au kwa kiwango kidogo? Kama
tunatumia kiwango kidogo basi tujue kuwa hata kama
tutapata kitu tunachodhani kitatufurahisha utajikuta hatufurahi, kwa
sababu hatutafanikiwa au tutakuwa na furaha ya muda tu kwa vile nia yetu
hatukuijaza kikamilifu ili tuweze kupata furaha timilifu
B-
Je tunafanya sawa katika maamuzi au tunabahatisha tu? Endapo tutakuwa
tunafanya mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu
itakuwa kwenye makosa na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale
tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu wanatafuta watoto lakini
hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta mali,
elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa
usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata
yatakayotufurahisha.
C- Je tunatimiza wajibu wetu au tunadanganya? Wapo watu ambao walitamani kuoa ili wapate furaha, lakini walipofanikiwa katika hilo hawakutimiza majukumu yao
wakajikuta wanageukwa na wake/waume zao na kujutia uamuzi wao. Msomaji
wangu, unapokuwa katika safari ya kutafuta furaha kupitia utajiri,
elimu, uongozi ni vema ukatimiza wajibu wako, ili upate matokeo mazuri.
Maana kama utakuwa unatamani kufaulu mtihani wako halafu husomi kwa
bidii, sina shaka majibu utakayopata yatakuhuzunisha kwa sababu lazima
ufeli na furaha uliyotaka haitapatikana.
D-
Je tunafuata muongozo, au tunakiuka? Kila jambo tunalotaka kulifanya
lina kanuni zake, ukitaka kupika ugali upo muongozo ambao unakutaka uwe
na vifaa, uache maji yachemke na hata kutoharakisha upishi wenyewe,
lengo ni kupata matoke mazuri. Sasa kama tutakuwa kupata furaha ya
kudumu kupitia mambo fulani ni lazima tuyafanye kwa kufuata muongozi na
si kwa kukurupuka. Biashara, elimu, kazi, zote hizi zinamiongozo ambayo
lazima kuifuata kwa matokeo mazuri.
E-
Tunatumia tulivyopata au tunavitelekeza? Wapo watu ambao hutamani
kupata kazi, lakini wanapopata hawazitumii, kazi hizo kwa ukamilifu,
badala yake wanakuwa watu wa kufanya ujanja ujanja ujanja kwa kutoroka
na wakati mwingine kutojihusisha na shughuli nyingine kwa lengo lile
lile la kutafuta furaha. Kusema kweli mtu wa namna hii hawezi kuwa na
furaha kwa sababu anayolenga yamfurahishe hayatumii kufurahika na badala
yake anatafuta jambo jingine. Fikiria kuhusu mume, anaoa lakini anaacha
kumtumie mke wake wake anakwenda kwa hawara! Hili si jambo jema na
kamwe haliwezi kuleta furaha kupitia mambo tunayoyatafua.
Kushikilia
kitu unatumia nguvu
nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni
misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika
maisha na mengineyo.
Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi
kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at:
http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
Kushikilia
kitu unatumia nguvu
nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni
misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika
maisha na mengineyo.
Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi
kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at:
http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
Ushauri wa namna ya kupunguza msongo
wa mawazo.
-Kama tatizo lako ni kubwa, jaribu
kutatua shida ndogondogo kwanza hatimaye kumalizia na shida iliyokubwa.
-Kubali kutua mzigo wa msongo wa
mawazo kwa kuacha kubeba na kushikilia kichwani mambo ambayo yapo nje ya uwezo
wako. Utakapofanya hivyo ni kama kitendo cha kuhema, unatoa hewa chafu nje na
kuvuta hewa safi ya uzima ndani. Kwa kufanya hivyo unapumzisha akili.
-Kama
tatizo lako ni dogo tu labda
mtu amekuudhi au umeshindwa kabisa kumudu hisia zako na mawazo yako ni
heri kwenda
mahali penye watu wengi penye starehe ya aina fulani kama labda ni
beach, cinema
au mahali pa kukufanya ujiliwaze na kupunguza mawazo yako. Kwenda mahali
penye
watu wengi ni muhimu pia kwasababu unapokuwa katika sehemu yenye watu
wengi ni rahisi kusaidiwa na watu wanaokuzunguka iwapo utataka kufanya
jambo la ajabu kwasababu ya mawazo au hasira ulizonazo.
-Ikiwa
hupati majibu kwa yale mambo yanayokufanya uwaze sana, tafuta ndugu,
jamaa au rafiki yako wa karibu sana unayemuamini na umueleze matatizo
yanayokusibu huenda ukapata ushauri au njia mbadala ya kutatua matatizo
yako.
-Pima
uzito wa mambo yanayokupa mawazo tele, kama jambo hilo sio la msingi
sana katika maisha yako unaweza kuupuza na usilipe nafasi katika akili
yako. Mawazo mengi yasiyo ya kukujenga kimaisha au mawazo yasiyo na tija
ni vyema ukayapuuza ili kuondekana na msongo wa mawazo usio wa lazima.
Akili yako ina mambo mengi ya kufikiri, ijaze na mambo mazuri
yatakayokusaidia sasa na hapo baadae. Usiijaze na sumu kama hasira,
mawazo potofu na mambo mengine yatakayoweza kukubomoa.
- See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
Kushikilia
kitu unatumia nguvu
nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni
misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika
maisha na mengineyo.
Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi
kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at:
http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
No comments:
Post a Comment