Waangalizi wa kimataifa wameutaja uchaguzi wa urais
nchini Madagascar kuwa huru na wa haki huku matokeo ya uchaguzi huo
yakiendelea kusuburiwa.
Uchaguzi wenyewe uliofanyika siku ya Ijumaa ulikuwa wa kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika kisiwani humo mwaka 2009.
Matokeo ya mwanzomwanzo yanaonyesha mshirika wa rais aliyeng’olewa madarakani Marc Ravalomanana akiwa mbele kwa hesabu za kura.
Richard Jean-Louis Robinson ana asilimia 30 ya
kura hadi sasa huku mshindani wake, Hery Martial Rakotoarimanana
Rajaonarimampianina akipata asilimia kidogo zaidi ya 15%.
Matokeo rasmi huenda yakajulikana baada ya wiki moja.
Ikiwa hakuna mgombea yeyote atapata zaidi ya asilimia 50, ya kura zilizopigwa, duru ya pili itafanyika tarahe 20 Disemba.
Mkuu wa uangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa
Ulaya, Maria Muniz de Urquiza, amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru
na wa haki licha ya visa kadhaa vya ghasia.
Naye Nandi-Ndaitwah, mwangalizi mkuu wa uchaguzi
kutoka kanda ya Afrika Kusini, alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na
wenye amani , wazi na kuwa unaonyesha matarajio ya watu.
Wagombea wakuu wawili, wameahidi kuujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka mingi ya vurugu za kisiasa.
Zaidi ya 92% ya watu milioni 21 nchini humo wanaishi kwa dola mbili kwa siku , kulingana na benki ya dunia.
Bwana Rajaonarimampianina amesema kuwa ana nia
ya kuwasaidia vijana wasio na ajira , kujenga upya miundo msingi na
kuimarisha kilimo , kufanya mageuzi katika sekta ya elimu pamoja na
kuimarisha demokrasia nchini humo.
Bwana Robinson anasema kuwa mpango wake wa
maendeleo unatokana na ule wa Rais wa zamani Bwana kujaribu kujenga upya
sekta ya utalii inayokumbwa na changamoto si haba nchini humo.
Madagascar imekuwa ikikumbwa na vurugu za isiasa
tangu mwaka 2009, wakati Andry Rajoelina alipompindua kutoka mamlakani,
aliyekuwa Rais Marc Ravalomanana.
Mapinduyzi ya kijeshi yalisababisha nci hiyo kutengwa na jamii ya kimataifa, na hata kunyimwa misaada.
Lakini mapema mwaka huu Bwana Rajoelina na
Ravalomanana walikubali kutoshiriki uchaguzi mkuu kulingana na mpango
ulioafikiwa na muungano wa SADC.
Taarifa na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment