Monday, October 7, 2013

Jinsi ya kupika Kachori

Kachori


VIPIMO

Viazi (mbatata)                                         2lb
Thomu na Tangawizi                                 Kijiko 1 cha chakula
Chumvi                                                       Kijiko 1 cha chakula
Pilipili ya kusaga                                       kutegemea na unavyoipenda
Ndimu                                                        1
Mafuta ya kupikia
Unga wa dengu au Ngano                         Kiasi.



NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Chemsha viazi  mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.
2.      Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.
3.      Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi .
4.      Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.
5.      Tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray.
6.      Vuruga unga  wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.
7.      Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.
8.      Chovya madonge  kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia)
9.      Wacha kachori  zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.
10.  Weka Kachori  kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa. 

Unaweza kupika na chachandu kwa ajili ya kulia kwenye Kachori.

No comments:

Post a Comment