Thursday, October 31, 2013

Welcome and Join my site







and if Don't have any of these? Create a new Google Account

Miili 87 ya wahamiaji yapatikana jangwani

Jangwa la Sahara
Waokozi nchini Niger wanasema kuwa wamepata miili 87 ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa wanajaribu kuvuka jangwa la Sahara.
Mmoja wa waliokuwa wanaendesha shughuli ya ukozi Almoustapha Alhacen, alisema kuwa miili yao ilikuwa katika hali mbaya ya kuharibika na kuwa ilikuwa imeliwa sehemu moja na wanyama pori.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Wengi walikuwa wanawake na watoto.
Niger ni kivukio kikubwa cha wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika Kaskazini.
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
Akizungumza kutoka katika kiwanda cha kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.

Taarifa na BBC Swahili

Watu 2 wakutwa na kiganja cha mkono wa Binadam jijini Mwanza

Photo: Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.

Washukiwa walikamatwa karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza, wakawapekulia wakakutwa mteja ana 100 million na mganga ana kiganja ambacho bado kibichi kinatoa damu, kina tunguri pia na nywele za binadamu

Taarifa zaidi => http://bit.ly/HsvvgDi


Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukutwa na kiganja cha mtu akitaka kukiuza kwa Sh Milioni 100. Washitakiwa hao walikamatwa karibu na uwanja wa ndege jijini humo. Walipopekuliwa mnunuaji alikutwa na sh Milioni 100 wakati mganga mmoja aliyedaiwa kuwa ni muuzaji wa kiganja hicho alikutwa na kiganja ambacho bado kibichi kinatoa damu na tunguli pamoja na nywele za binadamu.

Taarifa na mitandao

Soma magazeti ya leo Jumatano tarehe 30/10/2013


Haya ndiyo yaliyojili kwenye magazeti ya leo

llo



p

o

Wednesday, October 30, 2013

Ni kweli soda ni mbaya kuliko tunavyo fikilila. Hebu jifunze athari za soda


Mala nyingi tunatumia Soda kama kiburudisho tukihisi kwamba ni tamu na hata kufikili kukata kiu zetu.


KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususan soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUIPIGA KIBUTI SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.

Kuwa makini sana ni bora kunywa maji mtu akakuona mshamba kuliko kunywa kinywa ambayo madhara yake ni makubwa na ya mda mrefu.

UN:Makali ya waasi wa M23 yamekwisha

 
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa makali ya kundi la waasi la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha
Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka katika maeneo yao ya kivita mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako katika eneo dogo karibu na mpaka wa Rwanda.
Eneo lengine la tano lililokuwa ngome ya waasi hao liliweza kudhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Jumatatu.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.
Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu karibu na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumai kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na serikali.
Alisema: ‘‘Bwana Kobler ametuarifu kuwa wanashuhudia mwisho wa kundi la M23 kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata kulikuwa na makubaliano kuwa sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini Kampala.’’
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala, yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao
Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
‘‘Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili tutakavyoimarisha hali ya wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa kwa huduma za serikali katika muda wa masaa 24,’’ alisema Paluku.
Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50 Kaskazini mwa Goma, mji rasmi wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi

Taarifa na BBC Swahili

Soma magazeti ya leo Jumanne tarehe 29/10/2013















































Tuesday, October 29, 2013

Njia 10 za kuimarisha kumbukumbu kichwani


Miongoni mwa hazina muhimu kwa mwanadamu ni kuwa na uwezo wa kukumbuka vitu kwa urahisi. Wanafunzi wengi hushindwa kufanya vizuri mitihani yao kwa sababu ya kukabiliwa na tatizo la usahaulifu,  ambao huchochewa na mambo mengi ukiwemo ulevi wa pombe, utumiaji wa dawa za kulevya na msongo wa mawazo ya kimaisha.

Licha ya uwezo  wa kumbukumbu kupungua kutokana na umri wa mtu, sayansi yaitegemei kijana mwenye umri wa chini ya miaka 28 kukabiliwa na tatizo hili kwa kiwango kikubwa, ingawa wale wenye miaka zaidi ya 40 wanatajwa kuzorota katika uwezo wa kukumbuka mambo.

Hata hivyo uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao huzingatia suala la kanuzi za afya zikiwemo mbinu za kukuza kumbukumbu ya akili hupunguza kwa kiasi kikubwa mmeng�enyeko wa seli zinazojenga uwezo wa akili katika kutunza kumbukumbu. (Susan Tapert  mwanasaikolojia kutoka Chuo cha California San Diego na kituo cha VA San Diego nchini Marekani anathibitisha haya pia).

Hivyo basi, ili mwanafunzi aweze kuwa na uwezo wa kutunza vema mambo anayosoma na kufundishwa na waalimu wake darasani lazima aweze kuiongezea akili yake uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa kufanya yafuatayo:

1        . LISHE BORA
Ni wazi kuwa wengi wetu tunafahamu maana ya lishe bora, lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo cha American Academy of Neurology kinachojihusisha na mambo ya neva, ulibaini kuwa machungwa, Spinachi, Karoti, brokoli (aina fulani ya mboga kama kabichi), viazi vitamu na mboga mboga huuongezea uhai ubongo na kumfanya mwanadamu asiweze kushambuliwa na magonjwa wa kupooza.

Aidha matunda na vyakula vyenye vitamini B, Foliki Asidi (folic acid), Niasini (niacin) Kalkumini (curcumin) husaidia kuufanya ubongo uwe na mawasiliano ya kutosha na viungo vingine vya mwili na kupunguza kwa asilimia 11 uhalibifu wa seli ndani ya ubongo. (Utafiti wa National Research Council nchini Milan, Italy unathibitisha kuwa vyakula vyenye Vitamini C na E hupunguza kiwango cha usahaulifu)

           2. MAZOEZI YA MWILI
Ufanyaji wa mazoezi ya mwili huimarisha misuli na kusaidia akili kuweza kufanya kazi vema, hii inatokana na ukweli kwamba tunapofanya mazoezi tunakuwa tunaongeza msukumo wa damu mwilini na hivyo kuufanya ubongo kufikiwa na damu ya kutosha ambayo ni muhimu kwa uimara wa kumbukumbu.

Mara nyingi,  mazoezi yanayofaa zaidi kwa afya ya mwili na uimarisha wa ubongo ni yale ya asubuhi na jioni. Kuhusu aina ya mazoezi inategemea na umbo la mtu, lakini kukimbia, kuruka kamba, kucheza mpira na hata kuinua vitu vizito vinavyolingana na uwezo wa mtu ni bora kwa afya. Mazoezi ya aina hii yakifanywa na wanafunzi yanaweza kuwasaidia pia kutunza kumbukumbu za masomo wanayofundishwa.

3 : MAZOEZI YA AKILI
Ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na mazoea ya kuifanyisha akili yake mazoezi ya kutunza kumbukumbu kwa kuingiza kichwani mambo ambayo hakuyazoea na kuyafanyia mazoezi ya kuyakumbuka. Kwa mfano mwanafunzi anaweza kundika namba zisizopungua 14 na kuanza kuzitaja kwa kufuta mpangilio aliojiwekea.

Namba zinatakiwa ziandikwe kwa kuchanganywa si kwa kuzifuatanisha kwa mtindo wa kuhesabu. Mfano, 23938393835575, baada ya kuziandika kwa mfumo huo mwanafunzi atatakiwa kuzikariri kwa dakika tano kisha kufumba macho au kutazama pembeni na kuanza kuzisoma kwa kufuata mfululizo huo, huku akihakikiwa na mtu mwingine. Mazoezi haya yatamsaidia kuondoa tatizo la kusahau na kumpa kipimo ni kwa kiwango gani hana uwezo wa kukumbuka.

Endapo mwanafunzi atashindwa kufikia kiwango cha zaidi ya nusu ya namba alizojiwekea afahamu kuwa ana uwezo mdogo wa kutunza kumbukumbu hivyo anatakiwa kuongeza juhudi za kujiimarisha.

Njia nyingine ya kuifanyisha mazoezi akili ni kujifunza mara kwa mara mambo mapya, ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo kwa  lugha ya kigeni, kujifunza lugha za makabila mengine, kutembelea mitandao mbalimbali ya intaneti na kusoma, kucheza michezo ya kwenye simu na kompyuta.

Aidha usomaji  wa  vitabu, urudiaji wa mara kwa mara wa notisi za darasani, husaidia kuongeza msukumo wa akili katika kutunza kumbukumbu kichwani. Hata hivyo tafiti nyingi zinaonesha kuwa uhudhuriaji wa majadala na uongeaji wa mambo ya msingi mbele ya watu wengi huimarisha uwezo wa mtu kukumbuka mambo kwa urahisi.

4. UTUMIAJI WA VINYWAJI

Vinywaji kama kahawa, chai nyeusi navyo huchangia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu. Inashauriwa kwa mwanadamu kutumia walau kikombe kimoja cha vinywaji hivyo ili kuongeza enzymes ambazo ni muhimu kwa kuuongezea nguvu ubongo ili uweze kutunza kumbukumbu. Hata hivyo vinywaji vikali kama pombe haviruhusiwi kwani huchangia kudumaza uwezo wa kukumbuka.

5. PUNGUZA MSONGO WA MAWAZO

Ubongo unaweza kushindwa kutunza kumbukumbu endapo mtu husika atakuwa na msongo wa mawazo yatokanayo na shida za kidunia. Endapo mwanafunzi atakuwa mtu mwenye kuutumikisha ubongo wake katika mawazo yenye kuumiza kila wakati, hawezi kuwa na uwezo wa kukumbuka anayofundishwa.

 Hivyo ni vema kupunguza mawazo kwa kuwashirikisha wengine magumu unayokutana nayo maishani na kukubali kuyaacha yapite ili yakupe nafasi ya kuishi kama wewe. Hatari ya msongo wa mawazo ni kuongeza kiwango cha seli za cortisol ambayo huharibu ubongo wa kati ambao ni muhimu kwa kutunza kumbukumbu.


6. KULALA
Watu wengi wakiwemo wanafunzi wamekuwa wakipuuza usingizi kwa kusoma sana usiku na kuacha kupumzisha miili yao kwa kulala, jambo ambalo hili ni hatari kwa utunzaji wa kumbukumbu kichwani.

Ifahamike kuwa usingizi ni kama chujio la akili ya mwanadamu, ambapo mtu anapolala mchakato hufanyika akilini kwa kuyachambua mamilioni ya mambo ambayo mhusika aliyaona, kuyasikia, kuhisi na pengine kuyatenda. Mchakato huo huweza kuchuja mambo mabaya na kuyatupa  na mema huhifadhiwa kwenye kumbukumbu.

Hivyo, kama mwanafunzi hatolala, mambo yote yakiwemo ya kipuuzi aliyofanya mchana yatabaki kwenye akili yake na kama mtindo huo wa kutolala utaendelea unaweza kuufanya ubongo uchoke na kupoteza kumbukumbu ya mambo muhimu yakiwemo ya shuleni.

Utafiti uliofanywa mwaka 2008 na Chuo cha Pennsylvania ulionesha kuwa wanafunzi wanaolala kwa saa 6 kwa siku huwa na kumbukumbu nzuri zaidi ya wale wanaolala kwa kiwango cha chini ya saa hizo. Utafiti wa aina hii ulifanywa pia na Chuo Cha Luebeck na kubainisha kuwa akili huongezewa uwezo mara tufu kwa kutunza kumbukumbu pale mtu anapokuwa analala usingizi mnono.

7. TUMIA MUZIKI
Muziki unatajwa kuwa na faida katika kumsaidia mtu kukumbuka mambo yaliyopita, inawezekana kabisa kwa kupita wimbo ukakumbuka mambo ambayo uliyafanya siku za nyuma. Hivyo kuufurahisha mwili kwa kucheza muziki, kusikiliza nyimbo, kunaweza kuongeza uwezo wa mtu kukumbuka mambo. Hata hivyo kujifunza lugha au jambo fulani kwa njia ya wimbo ni rahisi kukumbuka kuliko kuhifadhi maneno yenyewe.


8. KUANDIKA
Ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na kumbukumbu za pembeni nikiwa na maana ya maandishi ya mkono. Ni muhimu kuorodhesha mambo ambayo umekusudia kuyafanya au yalikutokea kwa kuyaandika kwenye kitabu kidogo cha kumbukumbu. Mfano, unaweza kuandika siku uliyoanza shule, uliyozaliwa, tarehe uliyomaliza darasa la saba n.k.

9. ONDOA HOFU

Kuna wanafunzi wengine hushindwa kukumbuka mambo si kwa sababu akili imesahau, bali wanajichanganya kwa hofu na kutojiamini kwamba wanachokumbushwa na akili kwa wakati huo kiko sahihi. Hivyo ni wajibu wa mtu kujiamini na kutupilia mbali wasi wasi wote unaojitokeza wa kuhofu kuchekwa au kutofanya vizuri katika jambo lililopo mbele yake.


10. AFYA
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu katika uimarishaji kumbukumbu za kichwani ni mtu kuwa na afya kwa maana ya kuhakikisha kuwa anatibiwa magonjwa yake na anakuwa mfuasi mzuri wa huduma za kitabibu kwa ajili ya kuuwesha mwili wake ufanye kazi kama unavyokusudia.

Njia za kutafuta na kupata furaha maishani

Miongoni mwa vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu ni kupata furaha. Watu wengi wamekuwa na harakati nyingi za kuhakikisha kuwa wanafurahika katika kuishi kwao. Kuna wanaotafuta furaha kupitia kwa rafiki, wapenzi, ndoa zao na hata jamii zao. Ni wazi kwamba kila afanyalo mwanadamu kupitia maamuzi yake, msingi wake huwa ni kutafua furaha, hii haijalishi kama atafanya jambo mbaya au zuri kwa mtazamo wa watu.
Ifahamike, watu wanavuja jasho katika kufanya kazi kwa sababu wanahitaji mshahara au pato ambalo baadaye hulitumia katika kufurahi. Wasomi, wafanyabiashara nao wanapohangaka katika hili na lile ukichunguza utakuta nyuma yao kuna kiu ya furaha.
Hii ina maana kuwa, furaha ndiyo jambo pekee ambalo watu hulitafuta zaidi. Ni nadra au pengine hakuna mtu ambaye kwa akili timamu ana kiu ya kupata mabaya na kuhangaika kuyatafuta. Mara nyingi yakimtokea basi huwa yamejitokeza tu katika safari yake ya kutafuta furaha. Wezi, majambazi, wazinifu hata watukanaji wote kwa pamoja wanapofanya hivyo huwa nyuma yao kuna hitaji la kupata furaha.
Pamoja na shabaha ya binadamu kuwa katika kutafuta furaha, wengi wao wamekuwa hawaipati kwa sababu hawajui njia za kuipata. Kuna watu wanahangaikia utajiri, wakidhani wakiupata, basi watakuwa na furaha, lakini baada ya kupata utajiri huo hujikuta hawana furaha. Wengine huamua kuoa, kuwa na wapenzi na marafiki lakini nao matokeo huwa tofauti na malengo.
Ingawa kuna matatizo mengi ambayo yanajitokeza katika maisha ya watu kila siku ambayo huondoa furaha, lakini si sababu ya moja kwa moja ya kumfanya mtu ahuzunike, eti tu kwa maana kafikwa na tatizo. Ukichunguza kwa makini utafahamu kuwa furaha si kitu ambacho mtu anaweza kukipata na kikamtosha. Unaweza kupata kila kitu lakini ukawa huna furaha.
Ukisema pesa ndiyo furaha, unaweza kuzipata lakini usifurahike na ukashangaa watu ambao ni masikini wakawa na furaha tele. Hivyo basi msingi wa furaha ni uelewa wa namna ya kuitafuta na kuipata.  Swali, furaha inapaika wapi na katika vitu gani? Nibu ni kuishi kwa kuzingatia muongozo ufuatao:

 Unaitafutaje furaha?
Watu wengi wanapopata matatizo huwa hawakubali kuyapokea. Kuna mfano wa mtu mmoja ambaye alikuwa bosi katika kampuni, siku moja uongozi wa juu uliamua kumshusha cheo kutoka ukurugenzi hadi mpokea wageni. Bosi huyo alipotelemshwa cheo kwa kiwango hicho hakujiona duni kwa wafanyakazi wenzake, badala yake alichofikiri yeye ni kwamba watu wote wanamuunga mkono na kumsikitikia kwa unyama huo wa kushushwa cheo kupitiliza.
Zile fikra za kuhurumiwa na watu zilimfanya awe na furaha na akawa mtu wa kuwahi kazini kila siku ili watu wakamuone na kumsikitia, jambo ambalo aliamini kuwa uongozi uliomshusha cheo ndiyo unaopata aibu mbele ya jamii na wala sio yeye. Kitendo hicho cha kuwahi kazini na kuonekasna ni mtu mwenye furaha kilimfanya awe mtu wa pekee kwenye jamii, aliweza kutengeneza maswali mengi kwa watu na hatimaye minong’ono ya kuonewa ilianza kusikika.
Kilichotokea hatimaye, kampuni moja kubwa ilipata habari ya kuwepo kwa mtu wa aina hiyo, ikafanya mawasiliano naye na kumwajiri, bila kujali kashfa zilizokuwa zimemwengua katika wadhifa wake wa kwanza. Jamaa huyo alipopata ajira mpya alijirekebisha makosa yake ya kugushi na wizi kwa vile alikuwa amejifunza kilichokuwa kimempata. Bosi huyo aliweza kuendesha kampuni hiyo kwa mafanikio makubwa, jambo lililowafanya wakuu wake wa zamani wajute kumuondolea wadhifa.
Hapa tunajifunza kuwa tunapopata matatizo kinachotufanya tupoteze furaha ni fikra zetu, lakini tukijua kucheza nazo na kuzielekeza katika mlango wa pili, tunaweza kuyatumia matatizo yetu kupata furaha pia. Lazima kila mmoja wetu atambue kuwa matatizo ni shule, tunapoyapata tunajifunza. Lakini hatuwezi kujifunza tukiwa na msongo wa mawazo, lazima tufanye unafiki fulani wa kimawazo kama alioufanya bosi aliyeshushwa cheo, yeye hakuangalia wadhifa wake wa zamani, wala namna gani watu wanamtazama katika kazi yake mpya. Mawazo yanawezaje kutuletea furaha?
Katika hali ya kawaida hakuna mtu hata mmoja anayeweza kumwambia mwenzake lia naye akafanya hivyo. Kila siku tunaona na kusikia mengi kutoka  kwa ndugu, rafiki, waalimu wahubiri, wachungaji mapadri wetu na hata kwenye vyombo ya habari, lakini kusikia huko hakuna maana kuwa ni lazima kutuondolee furaha, kwani ndani ya akili zetu kuna kitu muhimu ambacho ni maamuzi yetu.
Utawala wa mawazo yetu ni kazi ya kila siku na uamauzi wa nini ha kufikiri ni suala ambalo lipo kwenye uwezo wa mwanadamu mwenyewe. Ingekuwa ni lazima kila wazo baya tunaloliona na kulisikia lazima lituhuzunishe basi tusingekuwa na furaha hata kidogo katika maisha yetu, kwani hakuna siku ambayo itapita bila kuona, kusikia au kutendewa jambo baya na mtu mwengine.
Ajali zinatokea kila siku, watu wanakufa, wanaugua, wanateseka, wanalia, wanaomboleza na kufanyiana hila, lakini kwa nini hatuyachukulii matukio yote kwa uzito sawa kiasi ha kulia? Ni kwa sababu tuna uhuru wa kuchagua tulie kwa sababu ya nani na kwa nina? Na hii ndiyo silaha pekee ya kuyatumia mawazo kutuletea furaha. Yaani kuchagua lipi la kutuliza na lipi la kutufurahisha na mwisho wa yote tuna uwezo wa kuyatumia mawazo yetu kuchagua mambo ya kufurahisha na kuyapa kipaumbele, bila kujali ni mema au mabaya. (Kumbuka mfano wa bosi aliyeshushwa cheo).

Hivyo ni vema wakati tunapokuwa na mawazo ndani yetu tukazingatia misingi ifuatayo ambayo inaweza kutusaidia kufikia uamuzi sahihi juu ya kila tunaloona na kulisikia, ili mawazo yasitufanye tuhuzunike na badala yake tufurahi. Kwanza ni kujipenda wenyewe. Tukijipenda hatutajihukumu na kujiona duni mbele ya wenzetu na hivyo kutopoteza furaha. Pili ni kujiamini, kuamini huku kutatuwezesha kuwa na msimamo juu ya maamuzi ya kila tunachoshibishwa ndani ya mawazo yetu kupitia mawasilia ya sauti na yasiyo na sauti.

Tatu, kumiliki mawazo yetu yasichukuliwe na ukubwa au udogo wa tatizo. Udhibiti huu lazima uyaone mambo yote yanayoingia kichwani kuwa ni ya kawaida kwa vile yapo duniani na yanawakuta watu kama sehemu ya changamoto za kimaisha. Katika hali ya kawaida ukubwa au udogo wa tatizo unatokana na mawazo ya mtu husika. Nne, kuwa na uvumilivu juu ya kila jambo kwa imani kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tano na mwisho ni kuhakiki maamuzi yetu kama yako sahihi kabla na baada ya kutenda jambo.

Kutojiheshimu kunavyohatarisha furaha yetu?

Ni muhimu kila mtu akaishi kama yeye alivyo, lakini linapokuja suala la kuchangamana na ulimwengu, lazima kuwe na kitu cha kujifunza kwa sababu huwezi kuishi nje ya familia na watu wengine.
Kwa msingi huo ili mtu aweze kupata furaha lazima afahamu namna atakavyoweza kujisahihisha tabia yake kwa kujiheshimu yeye na kuwaheshimu wengine anaoishi nao. Kwa maana kuishi kama mtu anatakavyo bila kutazama wengine ni  jambo baya. Hivyo dokezo zifuatazo ni muhimu kwa kila mtu kuzifahamu ili kuondoa mkwaruzano kati ya mtu na mtu.

A –Wafanyie wengine mema
Furaha haiwezi kuja kama mtu hajiheshimu mwenyewe na kuwafanyia wengine mema ambayo angependa atendewe. Watu wengi wamekuwa hodari kutembea na wake za watu, kuiba, kudhuru, kutukana, kudharau wengine na hata kunyanyasa, bila kugeuza upande wapili wa shilingi na kufikiri endapo wangefanyiwa wao hali ingekuwaje, si wangepoteza furaha? Sasa kama jibu ni ndiyo kwa nini wao wawe mahodari kuwaumiza wengine? Ni wazi kwamba kila mwanadamu angekuwa makini kufanya yale ambayo angependa kufanyiwa, kiwango ha huzuni kingepungua, na hii ndiyo changamoto kubwa kwa mtu atakaye kupata furaha lazima awafanyie wengine wema kwanza kabla ya yeye kufanyiwa.

 B – Kuwa kiongozi
Katika maisha kuna watu ambao hawaelewi kuhusu matumizi ya mawazo na namna ya kutenda kama binadamu, hivyo kwa wale ambao wanaelewa nini maana ya maisha ni vema wakawa viongozi kwa wengine, viongozi katika kusamehe, kukubali kosa, kutenda haki na kusimamia ukweli.

C- Kushukuru
Ni watu wachache sana ambao hushukuru wafanyiwapo mabaya, lakini inashauriliwa kwamba ili kuuita furaha na kupunguza nguvu ya huzuni ni bora mtu akajifunza kushukuru hata kama amefanyiwa jambo baya.

D - Kuwa na juhudi
Mambo yote tunayoyafanya lazima yaambatane na juhudi. Ikiwa tunatafuta majibu ya nini tunataka kifanyeke katika kupata furaha lazima tuwe na bidii, tusifanye vitu kwa uzembe kwani matokeo yake ni kushindwa ambako kutatuingiza katika shida ambazo zitatuhuzunisha. Umeolewa jitahidi kulinda ndoa yako, jitahidi katika kazi na kila jambo ili usikwame.

E- Kuchunga ulimi
Kuna watu wengi ambao wanapoteza furaha kwa kutojua namna ya kutumia ndimi zao. Utakuta mtu yuko katika kati ya watu, anatukana na wakati mwingine kutamka maneno ambayo wenzake hayawapendezi. Kujiheshimu ni pamoja na kuchuja maneno ya kusema mbele za watu kulingana na mahitaji yaliyopo, kuropoka ropoka kuna madhara. Kabla hujasema kitu tafakari kama usemecho kitaleta furaha au huzuni.

                  Kanuni za kuifikia furaha ya kweli
Wakati wa kutafuta furaha ya kweli lazima kujiuliza baadhi ya kanuni za kimaisha kama unazifuata kwa ufasaha, vinginevyo unaweza kuwa mtafuta furaha lakini usiwe miongoni mwa wanaoipata. Kama nilivyosema awali kuwa, kuna watu hutafuta furaha kupitia kwa wake/waume zao, rafiki, wapenzi na hata kwenye mali, lakini mwisho wa siku wanapokuja kutafakari zaidi hujikuta hawana furaha waliyoitaraji wakati wakihangaikia njia za kuipata.
Kuna watu ambao mawazo yao yanatamani sana kupata mtoto na wengine wameapa kabisa kwamba wakifanikiwa kushika ujauzito watakuwa na furaha, lakini bado kama hawatakuwa makini wao wenyewe watajikuta wanapata furaha ya muda na hatimaye kutoweka na kuanza kujutia harakati zao, huku wakianza safari mpya za kufuata furaha kupitia jambo jingine. Hebu tujiulize maswali haya.
A-Je tunapokuwa tunatafuta furaha tunatumia uwezo wetu wote au kwa kiwango kidogo? Kama tunatumia kiwango kidogo basi tujue kuwa hata kama tutapata kitu tunachodhani kitatufurahisha utajikuta hatufurahi, kwa sababu hatutafanikiwa au tutakuwa na furaha ya muda tu kwa vile nia yetu hatukuijaza kikamilifu ili tuweze kupata furaha timilifu

B- Je tunafanya sawa katika maamuzi au tunabahatisha tu? Endapo tutakuwa tunafanya mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu itakuwa kwenye makosa na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu wanatafuta watoto lakini hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta mali, elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata yatakayotufurahisha.

C- Je tunatimiza wajibu wetu au tunadanganya? Wapo watu ambao walitamani kuoa ili wapate furaha, lakini walipofanikiwa katika hilo hawakutimiza majukumu yao wakajikuta wanageukwa na wake/waume zao na kujutia uamuzi wao. Msomaji wangu, unapokuwa katika safari ya kutafuta furaha kupitia utajiri, elimu, uongozi ni vema ukatimiza wajibu wako, ili upate matokeo mazuri. Maana kama utakuwa unatamani kufaulu mtihani wako halafu husomi kwa bidii, sina shaka majibu utakayopata yatakuhuzunisha kwa sababu lazima ufeli na furaha uliyotaka haitapatikana.

 D- Je tunafuata muongozo, au tunakiuka? Kila jambo tunalotaka kulifanya lina kanuni zake, ukitaka kupika ugali upo muongozo ambao unakutaka uwe na vifaa, uache maji yachemke na hata kutoharakisha upishi wenyewe, lengo ni kupata matoke mazuri. Sasa kama tutakuwa kupata furaha ya kudumu kupitia mambo fulani ni lazima tuyafanye kwa kufuata muongozi na si kwa kukurupuka. Biashara, elimu, kazi, zote hizi zinamiongozo ambayo lazima kuifuata kwa matokeo mazuri.

 E- Tunatumia tulivyopata au tunavitelekeza? Wapo watu ambao hutamani kupata kazi, lakini wanapopata hawazitumii, kazi hizo kwa ukamilifu, badala yake wanakuwa watu wa kufanya ujanja ujanja ujanja kwa kutoroka na wakati mwingine kutojihusisha na shughuli nyingine kwa lengo lile lile la kutafuta furaha. Kusema kweli mtu wa namna hii hawezi kuwa na furaha kwa sababu anayolenga yamfurahishe hayatumii kufurahika na badala yake anatafuta jambo jingine. Fikiria kuhusu mume, anaoa lakini anaacha kumtumie mke wake wake anakwenda kwa hawara! Hili si jambo jema na kamwe haliwezi kuleta furaha kupitia mambo tunayoyatafua. 
Kushikilia kitu unatumia nguvu nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika maisha na mengineyo. Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
Kushikilia kitu unatumia nguvu nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika maisha na mengineyo. Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU

Ushauri wa namna ya kupunguza msongo wa mawazo.
-Kama tatizo lako ni kubwa, jaribu kutatua shida ndogondogo kwanza hatimaye kumalizia na shida  iliyokubwa.
-Kubali kutua mzigo wa msongo wa mawazo kwa kuacha kubeba na kushikilia kichwani mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako. Utakapofanya hivyo ni kama kitendo cha kuhema, unatoa hewa chafu nje na kuvuta hewa safi ya uzima ndani. Kwa kufanya hivyo unapumzisha akili. 
-Kama tatizo lako ni dogo tu labda mtu amekuudhi au umeshindwa kabisa kumudu hisia zako na mawazo yako ni heri kwenda mahali penye watu wengi penye starehe ya aina fulani kama labda ni beach, cinema au mahali pa kukufanya ujiliwaze na kupunguza mawazo yako. Kwenda mahali penye watu wengi ni muhimu pia kwasababu unapokuwa katika sehemu yenye watu wengi ni rahisi kusaidiwa na watu wanaokuzunguka iwapo utataka kufanya jambo la ajabu kwasababu ya mawazo au hasira ulizonazo.    
-Ikiwa hupati majibu kwa yale mambo yanayokufanya uwaze sana, tafuta ndugu, jamaa au rafiki yako wa karibu sana unayemuamini na umueleze matatizo yanayokusibu huenda ukapata ushauri au njia mbadala ya kutatua matatizo yako. 
-Pima uzito wa mambo yanayokupa mawazo tele, kama jambo hilo sio la msingi sana katika maisha yako unaweza kuupuza na usilipe nafasi katika akili yako. Mawazo mengi yasiyo ya kukujenga kimaisha au mawazo yasiyo na tija ni vyema ukayapuuza ili kuondekana na msongo wa mawazo usio wa lazima. Akili yako ina mambo mengi ya kufikiri, ijaze na mambo mazuri yatakayokusaidia sasa na hapo baadae. Usiijaze na sumu kama hasira, mawazo potofu na mambo  mengine yatakayoweza kukubomoa.
- See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU
Kushikilia kitu unatumia nguvu nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika maisha na mengineyo. Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. - See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/05/namna-ya-kupunguza-msongo-wa-mawazo.html#.Um9bS1MdHIU

Monday, October 28, 2013

Breaking news a Photo of Burning vehicle in Beijing's Tiananmen Square that killed 3

Don’t miss any updates

 

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 28 OCTOBER 2013





 

 

























 

 

 

 

 





 

 

 

 

Madagascar:Uchaguzi huru na wa haki

Waangalizi wa kimataifa wameutaja uchaguzi wa urais nchini Madagascar kuwa huru na wa haki huku matokeo ya uchaguzi huo yakiendelea kusuburiwa.
Uchaguzi wenyewe uliofanyika siku ya Ijumaa ulikuwa wa kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika kisiwani humo mwaka 2009.
Matokeo ya mwanzomwanzo yanaonyesha mshirika wa rais aliyeng’olewa madarakani Marc Ravalomanana akiwa mbele kwa hesabu za kura.
Richard Jean-Louis Robinson ana asilimia 30 ya kura hadi sasa huku mshindani wake, Hery Martial Rakotoarimanana Rajaonarimampianina akipata asilimia kidogo zaidi ya 15%.
Matokeo rasmi huenda yakajulikana baada ya wiki moja.
Ikiwa hakuna mgombea yeyote atapata zaidi ya asilimia 50, ya kura zilizopigwa, duru ya pili itafanyika tarahe 20 Disemba.
Mkuu wa uangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya, Maria Muniz de Urquiza, amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki licha ya visa kadhaa vya ghasia.
Naye Nandi-Ndaitwah, mwangalizi mkuu wa uchaguzi kutoka kanda ya Afrika Kusini, alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wenye amani , wazi na kuwa unaonyesha matarajio ya watu.
Wagombea wakuu wawili, wameahidi kuujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka mingi ya vurugu za kisiasa.
Zaidi ya 92% ya watu milioni 21 nchini humo wanaishi kwa dola mbili kwa siku , kulingana na benki ya dunia.
Bwana Rajaonarimampianina amesema kuwa ana nia ya kuwasaidia vijana wasio na ajira , kujenga upya miundo msingi na kuimarisha kilimo , kufanya mageuzi katika sekta ya elimu pamoja na kuimarisha demokrasia nchini humo.
Bwana Robinson anasema kuwa mpango wake wa maendeleo unatokana na ule wa Rais wa zamani Bwana kujaribu kujenga upya sekta ya utalii inayokumbwa na changamoto si haba nchini humo.
Madagascar imekuwa ikikumbwa na vurugu za isiasa tangu mwaka 2009, wakati Andry Rajoelina alipompindua kutoka mamlakani, aliyekuwa Rais Marc Ravalomanana.
Mapinduyzi ya kijeshi yalisababisha nci hiyo kutengwa na jamii ya kimataifa, na hata kunyimwa misaada.
Lakini mapema mwaka huu Bwana Rajoelina na Ravalomanana walikubali kutoshiriki uchaguzi mkuu kulingana na mpango ulioafikiwa na muungano wa SADC.

Taarifa na BBC Swahili

Wednesday, October 23, 2013

Anas al Liby afikishwa mahakamani US

Mshukiwa wa ugaidi aliyekamatwa na wanajeshi wa Marekani nchini Libya mapema mwezi huu wakati wa operesheni ya jeshi hilo mjini Tripoli, amefikishwa mahakamani kwa mara ya pili mjini New York.
Abu Anas al-Liby anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeeda aliwakilishwa na wakili wa serikali ya Libya.
Bwana Liby anatuhumiwa kuwa na uhusiano na al-Qaedana pia kuhusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 2008.
Hata hivyo amekanusha madai dhidi yake.
Bwana Liby, mwenye umri wa miaka 49, ambaye jina lake halisi ni Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, alifikishwa mahakamani kujadili kuhusu mawakili wake.
Wakati wa kwanza kwa Liby kufikishwa mahakamani, aliwakilishwa na mawakili walioteuliwa na mahakama baada ya kusema kuwa hangeweza kumudu gharama ya mawakili wake.
Hata hivyo inaarifiwa baadaye serikali ya Libya ilimwajiri wakili kuweza kumwakilisha Liby.
Wakili huyo, Bernard Kleinman, alisema kuwa itachukua muda wa miezi kadhaa kudurusu stakabadhi nyingi kabla ya kesi hiyo kuanza rasmi.
Pia alisema sharti Liby arejeshewe Quran yake iliyochukuliwa na wanajeshi hao wakati wa kukamatwa kwake.
Alisema kuwa anawakilisha mshukiwa mmoja anayezuiliwa katika jela la Guantanamo Bay,nchini Cuba.
Bwana Liby anatarajiwa kurejea tena mahakamani tarehe 12 Disemba.
Kumekuwa na ghadhabu nchini Libya kufuatia kukamatwa kwa Al Liby na wanajeshi wa Marekani baadhi wakidai kuwa serikali ya Libya ilihusika.

Tuesday, October 22, 2013

AUWAWA KWA WIZI WA KUKU WATATU KUKU ALIYEIBIWA ATAGA YAI PEMBENI YA MWILI WA MAREHEMU

Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa napolisi
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Frank







WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada  watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.
Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.
Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao  alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.
Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Alisema mtuhumiwa huyo  baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Aidha Baada  mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea  wa kuwabaini watu waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.