Wednesday, November 20, 2013

Unyama uliopitiliza Mume amcharanga mapanga mkewe na kumkata mguu


Stori: Imelda Mtema

WAKATI mwingine unakosa maneno ya kuelezea ukatilia uliopitiliza unaofanywa na baadhi ya watu hapa duniani dhidi ya binadamu wenzao. Tukio lililompata binti Gati Chacha, mkazi wa Kijiji cha Kinyantila, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara

tena alilofanyiwa na mumewe Bw. Chacha Mwita, linahuzunisha na kusikitisha kama siyo kustaajabisha. Uwazi limekinasa kisa kizima.
Binti Chacha amepewa kilema cha maisha baada ya kukatwa mguu wa kuume na mumewe, sababu ikiwa ni kuchelewa tu kumfungulia mlango aliporejea nyumbani usiku saa tatu, unaweza usikubaliane na sababu hiyo, lakini hivyo ndivyo inavyoelezwa kwa mshangao wa kila mtu!
Simulizi kutoka kinywani kwa mwanamke huyo inadai kuwa, siku ya tukio asubuhi mumewe alimuaga anakwenda kutafuta mboga ya familia lakini…
Stori: Imelda Mtema
WAKATI mwingine unakosa maneno ya kuelezea ukatilia uliopitiliza unaofanywa na baadhi ya watu hapa duniani dhidi ya binadamu wenzao. Tukio lililompata binti Gati Chacha, mkazi wa Kijiji cha Kinyantila, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara
tena alilofanyiwa na mumewe Bw. Chacha Mwita, linahuzunisha na kusikitisha kama siyo kustaajabisha. Uwazi limekinasa kisa kizima.
Binti Chacha amepewa kilema cha maisha baada ya kukatwa mguu wa kuume na mumewe, sababu ikiwa ni kuchelewa tu kumfungulia mlango aliporejea nyumbani usiku saa tatu, unaweza usikubaliane na sababu hiyo, lakini hivyo ndivyo inavyoelezwa kwa mshangao wa kila mtu!
Simulizi kutoka kinywani kwa mwanamke huyo inadai kuwa, siku ya tukio asubuhi mumewe alimuaga anakwenda kutafuta mboga ya familia lakini hakurudi mpaka saa tatu usiku.
Alisema: “Aliporudi hiyo saa tatu alibisha hodi, mimi kwa sababu nilishalala nikachelewa kusikia, lakini niliposikia nilikwenda kumfungulia mlango, lakini akaja juu akitaka kujua ni kwa nini nilichelewa kumfungulia mlango.
“Nilimuomba msamaha, nikamwambia nilishapitiwa na usingizi, hata watoto walishalala, hakunisikiliza, akachukua  panga na kunikata miguu yote.
“Huu mguu wa kulia aliukata kabisa, ukatengana na sehemu yake, huu wa kushoto hakuumalizia, ukawa unaning’inia, nikawahishwa Hosptali ya Wilaya Tarime kushonwa ndiyo ikawa salama yangu kubaki na mguu mmoja kama hivi.” (akalia).
“Inauma sana jamani! Ni kwa nini mume wangu alinikata miguu kwa panga kama anayekata pingili za mua?
“Siamini hata sasa kama ni akili zake kwani mimi ni mke wake nimemzalia watoto wawili, ni adhabu gani hii aliyonipa?” alihoji mwanamke huyo huku machozi yakiendelea kumchuruzika.
Akaendelea: “Kutoka moyoni nasema kuwa, baada ya tukio lile nilitaka sana kurudi nyumbani kwa wazazi nikauguze vidonda, lakini  tatizo ni kwamba kwa vile nililipiwa mahari siwezi kurudi wala mama hawezi kunikubalia nirudi mpaka baba aje kutoa ruhusa.” (matatizo ya mila na desturi na ukatili dhidi ya mwanamke).
Naye mama mzazi wa mwanamke huyo (hakutaja jina lake) maarufu kama mama Gati akilia kwa uchungu mkubwa alisema kwamba amekuwa akimwaga machozi kila siku tangu kutokea kwa tukio hilo la mwanaye kukatwa mguu na mumewe.
“Mimi nalia tu jamani! Nalia kila siku, nakumbuka siku nilipomzaa huyu mwanangu furaha niliyokuwa nayo na siku alipokatwa huu mguu uchungu nilioupata, lakini nimemwachia Mungu,” alisema mama huyo huku akilia.
Aliongeza: “Kwa utamaduni wetu huku, baba wa mtoto aliyekatwa mguu yaani mume wangu ndiye mwenye mamlaka ya kuamua binti yetu arudi nyumbani au aendelee kubaki kwa mume wake kwa hiyo nashindwa kuamua chochote.”
Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime-Rorya lilimtia mbaroni  mtuhumiwa huyo na kumfikisha  mahakamani.
Kwa kumalizia, Gati alimewaomba Watanzania watakaoguswa na tatizo lake wamsaidie ili aweze kurudi nyumbani kwa wazazi wake na kuachana na mila zinazomzuia kwa sababu baba mkwe wake (hakumtaja jina) amekuwa akimkejeli kwamba yeye (Gati) anaona raha kulala kitandani wakati mtoto wake (mtuhumiwa) analala chini jela.
“Hii kauli ya baba mkwe wangu inaniweka hatarini mimi. Naomba nisaidiwe nirudi nyumbani kwa wazazi wangu,” alisema Gati.
Hata hivyo, mama mzazi wa Gati alisema hana uwezo wa kumsaidia mwanaye huyo atakaporudi nyumbani akiwa katika hali hiyo kwa kuwa maisha yao ni duni.
Akaomba kwa yeyote atakayeguswa na tatizo la binti yake Gati awasaidie msaada wowote wa kibinadamu kwa kutumia namba 0713 612533 na Mungu atawabariki.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kikatili. Mguu wa Gati unaoonekana pichani umehifadhiwa chumba cha baridi katika hospitali hiyo.
Usikose kuangalia Kipindi cha  Wanawake Live cha Joyce Kiria kitakachorushwa leo usiku na Runinga ya EATV ili uupate mkasa huu ‘laivu’.

No comments:

Post a Comment