Wednesday, November 6, 2013

Mamilioni ya watu wahitaji msaada Syria

Takriban watu milioni 9.3 nchini Syria, wanahitaji msaada wa kibinadamu, hii ni kwa mujibu wa mkuu wa misaada ya kibinadamu katika umoja huo,Valerie Amos.
Idadi hii imeongezeka kwa watu milioni 2.5 kutoka watu milioni 6.8 idadi iliyotolewa na shirika hilo mapema mwezi Septemba.
 
‘‘Mgogoro wa kisiasa nchini Syria, unaendelea kuwa mbaya kila kukicha na kwamba hauzuiliki,’’ Bi Mos aliambia baraza la usalama la UN.
Wakati huohuo, mjumbe wa Jumuiya ya nchi za kirabu Lakhdar Brahimi anatarajiwa kukutana na wanadiplomasia wa Marekani na Urusi kwa mazungumzo yatakayotoa mwelekeo kwa kongamano la amani kuhusu Syria.
Wakati akiwa Mjini Geneva, bwana Brahimi pia atakutana na waakilishi wengine wa baraza hilo pamoja na majirani wa Syria kabla ya kongamano la amani lililopangwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Serikali ya Syria pamoja na makundi ya upinzani, wanatofautiana kuhusu mpangilio wa mazungumzo: Upinzani unataka Rais Bashir ajiuzulu huku serikali ikisema upinzani haupaswi kutoa vikwazo kwa mazungumzo hayo.

Na BBC Swahili

No comments:

Post a Comment