Tuesday, November 5, 2013

Soma kiundani zaidi magazeti ya Jumatatu ya tarehe 4/11/2013 hapa..........

SHAROBARO ALA KICHAPO KISA MKE WA MTU


Issa Mnally Na Richard Bukos
KIJANA mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja juzikati alijikuta akichezea kichapo cha mbwa mwizi kisa kikidaiwa kuwa ni mke wa mtu.

Usione vyaelea: Sharobaro (katikati) akilia baada ya kuchezea kichapo kwa kukutwa na mke wa mtu.
Tukio hilo lilijiri saa saba usiku mwishoni mwa wiki iliyopita, Chalinze mkoani Pwani ambapo mapaparazi wetu walikwenda kwa ajili ya uzinduzi wa…

Issa Mnally Na Richard Bukos
KIJANA mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja juzikati alijikuta akichezea kichapo cha mbwa mwizi kisa kikidaiwa kuwa ni mke wa mtu.

Usione vyaelea: Sharobaro (katikati) akilia baada ya kuchezea kichapo kwa kukutwa na mke wa mtu.
Tukio hilo lilijiri saa saba usiku mwishoni mwa wiki iliyopita, Chalinze mkoani Pwani ambapo mapaparazi wetu walikwenda kwa ajili ya uzinduzi wa kundi jipya la sanaa liitwalo 3 Ways.
Wakati shamrashamra zikiendelea, ghafla liliibuka timbwili na katika kufuatilia ilibainika sharobaro anayeishi eneo hilo alikuwa akila kipigo kutoka kwa mwanaume mmoja akimtuhumu kuwa alimkuta akiwa amekaa chobingo kihasarahasara na mkewe.

Mke wa mtu sumu: Sharobaro hoi baada ya kipigo.
Licha ya baadhi ya wasanii kujaribu kuingilia kati ugomvi huo, jamaa huyo aliendelea kushusha kichapo hadi pale watu walipomtolea uvivu na kumzuia asije akasababisha mauaji.
“Unajifanya sharobaro halafu unazengea wake za watu, sasa wee umeipata fresh na huyo mwenzako akirudi nyumbani naye
atakiona,” alisikika akisema mwanaume huyo huku akionekana kufura.
Kufuatia kichapo hicho, sharobaro huyo alijikuta akiangua kilio huku akilalama kuwa mwanamke huyo amemponza na kumharibia siku yake.

Kilio: Sharobaro akizidi kububujikwa na machozi baada ya kipondo kutoka kwa mwenye mali.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walisema, kipigo alichopata kijana huyo ni fundisho kwa masharobaro wengine ambao wamekuwa na uhusiano wa karibu na wake za watu.
“Unajua hawa vijana hii ndiyo dawa yao, wanajisahau sana. Yaani anajua kabisa fulani ni mke wa mtu lakini anajiweka, sasa kwa kipigo hiki atakuwa fundisho,” alisema baba mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Baba Zulfa.
Aidha, wengine walimtetea kijana huyo na kudai kuwa mwanamke huyo ndiye anayestahili kulaumiwa kwa kukubali kukaa gizani na kijana huyo wakati akijua ni mke wa mtu.




AUNTY LAIVU NA MUMEWE CHUMBANI


Na Mwandishi Wetu

MCHEZA sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amejianika laivu mtandaoni kwa mara ya kwanza akiwa chumbani amelala na mumewe, Sunday Demonte, Dubai anakoishi mwanaume huyo huku msanii huyo akiwa na maskani yake jijini Dar.
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe, Sunday Demonte chumbani.
Aunt alitundika picha tatu kwenye ukurasa wake katika Mtandao wa Instagram akiwa na Demonte…

Na Mwandishi Wetu
MCHEZA sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amejianika laivu mtandaoni kwa mara ya kwanza akiwa chumbani amelala na mumewe, Sunday Demonte, Dubai anakoishi mwanaume huyo huku msanii huyo akiwa na maskani yake jijini Dar.
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe, Sunday Demonte chumbani.
Aunt alitundika picha tatu kwenye ukurasa wake katika Mtandao wa Instagram akiwa na Demonte huku akisindikizia na maneno ya kumsifia laaziz wake huyo kwa kuwa ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake (Demonte).
Baada ya tukio hilo, mashabiki wake walimmwagia sifa kemkemu kuwa watu wamekuwa wakimsema vibaya kwa kukaa mbali na mumewe lakini sasa amewaziba midomo.

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AIBUKA NA 'A LADY WITH CONFIDENCE', APEWA MILIONI MOJA NA DAR LIVE!

Pichani juu ni malkia wa mipasho Khadija Kopa akiwa stejini katika usiku wake maalumu, huku akisindikizwa na kundi zima la TOT.
Kiongozi wa TOT, Gasper Tumaini, akiushukuru uongozi wa Dar Live kwa kuandaa usiku wa Malkia muda mfupi kabla hajapanda stejini
Mkurugenzi wa Dar Live Masha James (kushoto) akimkabidhi Kopa bahasha yenye kitita cha shs milioni moja usiku wa kuamkia leo ndani ya Usiku wa Kumtoa Malkia, Dar Live.
MALKIA wa Mipasho Khadija Kopa, usiku wa leo ameibuka kwa mara ya kwanza na wimbo mpya uitwao 'A Lady with Confidence' katika kiwanja cha burudani cha Dar Live, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuimba baada ya kukaa ndani eda kwa muda wa miezi minne na siku 10. Wimbo huo, ambao unaonekana kuwa moto wa kuotea mbali, ameuimba katika onesho lake maalumu la kumtoa nje na umemuwezesha pia kupewa kitita cha shilingi milioni moja na uongozi wa Dar Live, pesa iliyokabidhiwa kwake na Mkurugenzi wa Dar Live na Global Publishers, Masha James.
PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

SNURA AACHA MAJANGA DAR LIVE!

Snura akifanya vitu vyake stejini…
Snura akifanya vitu vyake stejini
Pichani juu ni mwimbaji wa TOT Taarab, Abdul Misambano akicheza na shabiki wake wakati wa onesho maalum la Usiku wa Malkia.

NATURE APEWA TAFU JUKWAANI NA CHEKA USIKU WA MALKIA

Msanii kinara wa kundi la TMK halisi, Sir Juma Nature usiku wa kuamkia leo alipewa tafu stejini na bondia maarufu nchini Francis Cheka ambaye alipanda jukwaani kuungana nae kusalimia mashabiki wake ambao walimshangilia kwa sana. Aidha TMK walimpatia bondia huyo fulana maalumu ya kundi hilo. Picha zifuatazo zinajielezea zaidi:


Bondia Francis Cheka (kati) akiwa stejini wakati TMK Halisi wakifanya vitu…



Bondia Francis Cheka (kati) akiwa stejini wakati TMK Halisi wakifanya vitu vyao.

Cheka akifurahia burudani ya shoo ya TMK
Msanii wa TMK Halisi KR Mullar akitoa ishara ya kumuita bondia Cheka jukwaani kabla ya kuanza shoo yao.
PICHA: Richard Bukos/GPL 

MWANAHAWA JUU YA STAGE, SNURA YUKO TAYARI BACK SATGE!

Posted by Global Publishers on November 4, 2013 at 1:51am 0 Comments

Mwanahawa Ally akiwa msanii anayejitegemea, akiimba nyimbo zake maarufu katika usiku wa Malkia ndani ya Dar Live.

Msanii Snura (kati) akiwa na shabiki zake nyuma ya VIP Backstage tayari kwa kumsindikiza Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa ndani ya Dar Live.…

Mwanahawa Ally akiwa msanii anayejitegemea, akiimba nyimbo zake maarufu katika usiku wa Malkia ndani ya Dar Live.

Msanii Snura (kati) akiwa na shabiki zake nyuma ya VIP Backstage tayari kwa kumsindikiza Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa ndani ya Dar Live.

Wacheza shoo wa msanii Snura wakiwa Backstage ya Dar Live tayari kwa kupiga shoo ya kumtoa malkia wa mipasho Khadija Kopa.

Msanii Juma Nature akishoo love na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa muda mfupi kabla ya kupanda stajini.
PICHA: Richard Bukos/GPL

FRANCIS CHEKA NDANI YA DAR LIVE NA TMK!


Bondia maarufu nchini Tanzania, Francis Cheka (wa pili kushoto), amedhihirisha ushabiki wake wa wasanii wa TMK Halisi kwa kuhudhuria shoo yao Dar Live na kupiga nao picha akina KR Mullar na JB wanaounda kundi la TMK Halisi linaloongozwa na Sir Nature, wakati wa shoo maalumu ya kumtoa malkia wa mipasho, Khadija Kopa ndani ya Dar Live, Nov 3, 2013.
PICHA: Richard Bukos /GPL

HAMMER Q AFUNGUA PAZIA LA KUMTOA MALKIA KHADIJA KOPA DAR LIVE!


Mwimbaji wa kundi la Five Stars, Hamma Q, ambaye pia aliwahi kuwa mwimbaji wa Bongo Fleva, akiimba na bendi yake usiku huu wakati wa Usiku wa Kumtoa Malkia Khadija Kopa katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live!

Baadhi ya waimbaji wa kundi la Five Stars wakiimba wakati wa shoo maalum ya kumtoa malkia Khadija Kopa baada ya kukaa eda ya miezi mitatu akiomboleza kifo cha mumewe aliyefariki miezi mitatu…

Mwimbaji wa kundi la Five Stars, Hamma Q, ambaye pia aliwahi kuwa mwimbaji wa Bongo Fleva, akiimba na bendi yake usiku huu wakati wa Usiku wa Kumtoa Malkia Khadija Kopa katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live!

Baadhi ya waimbaji wa kundi la Five Stars wakiimba wakati wa shoo maalum ya kumtoa malkia Khadija Kopa baada ya kukaa eda ya miezi mitatu akiomboleza kifo cha mumewe aliyefariki miezi mitatu iliyopita. 

No comments:

Post a Comment