Rais aliyeng’olewa mamlakani nchini Misri, Mohammed
Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo pamoja na vigogo wengine 14
wa chama cha Muslim Brotherhood, wakati kesi yake itakapoanza
kusikilizwa mjini Cairo.
Wameshitakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya
waandamanaji wakati wa vurugu za kisiasa nje ya ikulu ya Rais mwezi
Disemba mwaka jana.Morsi aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Ingawa alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Baada ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka Morsi aachiliwe.
Polisi walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa nguvu.
Serikali ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood, chama chake Morsi.
Serikali pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa mashirika hayo.
Wafuasi wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya kisiasa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi yao bila uwajibikaji.
Taarifa na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment