Wednesday, November 6, 2013

Soma kiundani magazeti ya leo Jumanne ya tarehe 5/11/2013 na habari motomoto hapa...

TANGAWIZI: NI TIBA YA KICHEFUCHEFU
TANGAWIZI ni chakula cha asili chenye uwezo wa kupambana na ugonjwa wa kichefuchefu na kutapika. Uwezo huu hutokana na vitamin B6 iliyopo kwa kiasi kikubwa katika tangawizi ambayo ni maarufu duniani kote kwa matumizi kama kiungo ‘spice’ kwa vyakula vingine.

Vitamin B6 iligunduliwa mwaka 1934 na Dr. Paul Gyorgy huko Hungary na akabainisha wazi kuwa ml.100 za B6 ni dozi tosha kwa siku kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 19 hadi 70 katika kupambana na kichefuchefu na hata kuzuia kutapika pia.
Tangawizi licha ya kuwa na uwezo wa kumaliza tatizo hili, bado imegundulika kuwa na uwezo tena wa kukinga maradhi ya uvimbe ndani ya mwili wa binadamu ambao husababisha wengi kupatwa na maradhi ya saratani za aina tofauti tokana na uvimbe huo.
Hata…

Hata hivyo, ukiwa unatumia tangawizi katika kila mlo wako kwa muda mfupi tu utajikuta maumivu ya mgongo, kiuno, maungio ya miguu na mikono yamepungua na kama siyo kuisha kabisa. Hii ndiyo kazi halisi ya tangawizi duniani na leo ni fursa kwako kulijua hili.
Kichefuchefu ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi duniani na chanzo kikiwa ni kupanda kwa joto la mwili kunakosababishwa na homa au maambukizi ya bakteria wa maradhi tofauti yakiwemo malaria pia. Hata hivyo, ugonjwa huu huwakumba sana akina mama wajawazito na kujikuta wakitapika mara kwa mara na kupoteza maji na madini mengi mwilini na kuhatarisha maisha yao wenyewe, watoto waliomo matumboni na pengine kuhatarisha maisha yao wote mama na mtoto.
Mbali na akina mama wajawazito kuugua ugonjwa huu watu wengine ambao hukumbwa na ugonjwa ni wasafiri wa baharini, wagonjwa wanaotumia dawa kali, watumiaji wa mihadarati, walaji wa vyakula vyenye sumu baridi, walevi wa kupindukia na pengine hata wanaokutana na harufu mbaya na kali kushinda uwezo wa kuimudu pia hupatwa na kichefuchefu na mwisho ni kutapika.
Ukiachana na sababu hizo, bado pia wagonjwa wa kidole tumbo yaani ‘appendix/appendiatis’ au hata wanaougua magonjwa ya mchafuko wa tumbo kama kuharisha na kipindupindu pia hupatwa na kichefuchefu na hutapika sana wanapokosa msaada wa tiba.
Kwa maradhi haya, kitu cha haraka kukifanya ni kunywa maji mengi huku ukijikongoja umwone daktari haraka kwa kuwa aina nyingi za maradhi haya huua haraka sana kwa kukosa maji na madini muhimu mwilini kwa kutapika. Ila, ulimwengu wa kisasa umetuletea teknolojia sahihi zinazokubalika duniani kote kwa kutengeneza vyakula lishe ambavyo ni mkandamizo wa vitamini, madini na tindikali muhimu kwa afya. Vyakula hivi vyenye kanuni ya vidongelishe na ungalishe vipo vya aina nyingi tu madukani na vinasaidia watu kupona maradhi mbalimbali bila kwenda hospitali.
Kama hujatumia tangawizi kwa muda mrefu na unajihisi kuwa na kichefuchefu mara kwa mara basi unaweza kuanza kutumia mara moja japo hutaona matokeo haraka ila ukitumia dawalishe ya B6 basi utapata nafuu haraka sana.
Akina mama wajawazito wao wanashauriwa kutumia dawalishe yao maalum iitwayo ‘Pregnancy Shake’ na MOM2B ya vidonge ambayo pamoja na vitamins nyingi zilizomo humo pia kuna vitamin B6 ambayo itamfanya ajisikie mwenye afya njema siku zote atakazobeba mimba yake huku akijihakikishia kujifungua salama.
Kama wewe huna maradhi yoyote ila ungependa kujiwekea kinga ya kutosha kwa maradhi basi unashauriwa utumie Dawalishe za B6 au uanze mara moja kuihusisha tangawizi katika milo yako yote ya kutwa nzima na hakika utaonekana ukitabasamu muda wote kwa kuwa utakuwa na kinga ya maradhi, hutaumwa viungo na hutasikia kichefuchefu tena katika maisha yako.
Ukiona mtu anatapika, basi chemsha maji yenye tangawizi yapooze na umpe anywe na kutapika kutaisha huku ukimuwahisha kwa daktari kwa msaada zaidi.
Kwa maoni na ushauri usisite kuwasiliana nasi.

BABU SEYA, PAPII KOCHA... KAZI IMEKWISHA

Na Mwandishi Wetu
MABERE Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya ameimaliza, sasa anasubiri majaji waliosikiliza alichokisema ili watoe uamuzi wa mwisho lakini pia anamtegemea Mungu.
“Mimi kazi nimemaliza sasa nawasubiri hao wakubwa (majaji) ili wapime nilichowaambia kwa mujibu wa sheria na kisha watoe uamuzi, lakini pia namtegemea Mungu,” alisema Marando.
Alisema ameiomba Mahakama ya Rufaa…

Alisema ameiomba Mahakama ya Rufaa Tanzania ifanye marejeo kuhusu hukumu iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani wateja wake hao na adhabu ya kifungo cha maisha jela wanayoitumikia kwa sasa.
Alipoulizwa alitumia muda gani kuwasilisha hoja zake hizo, Marando alisema takriban dakika 120 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Salum Massati.
Akiwa mahakamani hapo, Marando alidai kuwa mahakama iliteleza katika kutoa uamuzi uliowatia hatiani na kuwafunga maisha wateja wake na kwamba kuteleza huko kunaonekana waziwazi.
Alifafanua kuwa wakati wakifanya majumuisho ya kesi hiyo, mahakama ilijiridhisha kwamba kulikuwa na makosa katika kupokea ushahidi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuata taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa watoto.
Alieleza kuwa mtoto anayesoma shule kuanzia ya msingi anapotoa ushahidi licha ya tahadhari, ana uwezo wa kutambua zuri na baya na kwamba lazima ushahidi wake uwekwe kwenye kumbukumbu ya maandishi na kwamba usipoonekana ushahidi wote ni batili na unaondolewa.
Katika shauri hilo upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka uliwakilishwa na Mawakili Jackson Mlaki, Angaza Mwaipopo, Emakulata Banzi, Joseph Pande na Apimack Mbarouk ambao waliyapinga maombi hayo kuhusu marejeo kwa madai kuwa yamepelekwa mahakamani bila usahihi.
Mahakama hiyo imesema itatoa uamuzi wake siku itakayotangaza.
Babu Seya na Papii Kocha wako jela kwa makosa 10 ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo.
Walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Aprili na Oktoba 2003 eneo la Sinza Kwaremy jijini Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, Mwalimu wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye alishitakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa hayo kwa kuwaruhusu baadhi ya wanafunzi hao kutoka madarasani, aliachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.

MWINGIRA AMEZAA NA MKE WANGU - MUME

Stori: Na Waandishi Wetu

TUHUMA nzito dhidi ya kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, zimefunguliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kibaha, Pwani.
Dk. William T. Morris ambaye ni daktari anayetambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), ndiye aliyeshusha tuhuma hizo, akidai kwamba Mwingira amezaa na mke wake, Dk. Philis Nyimbi.
Morris ambaye wasifu wake unaeleza namna sifa zake zinavyojipambanua ndani ya Shirika la Afya Duniani (WHO), aliwasilisha madai hayo mwaka 2011, akitaka jeshi la polisi limsaidie kupata haki zake.
UWAZI LANASA JALADA LA UCHUNGUZI

Mtandao mpana wa mitego ya habari katika Gazeti la Uwazi, uliwezesha kunasa uwepo wa jalada la uchunguzi, likiwa na nambari KBA/ PE/23/2011 ambalo mhusika wake ni…

Stori: Na Waandishi Wetu
TUHUMA nzito dhidi ya kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, zimefunguliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kibaha, Pwani.
Dk. William T. Morris ambaye ni daktari anayetambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), ndiye aliyeshusha tuhuma hizo, akidai kwamba Mwingira amezaa na mke wake, Dk. Philis Nyimbi.
Morris ambaye wasifu wake unaeleza namna sifa zake zinavyojipambanua ndani ya Shirika la Afya Duniani (WHO), aliwasilisha madai hayo mwaka 2011, akitaka jeshi la polisi limsaidie kupata haki zake.
UWAZI LANASA JALADA LA UCHUNGUZI
Mtandao mpana wa mitego ya habari katika Gazeti la Uwazi, uliwezesha kunasa uwepo wa jalada la uchunguzi, likiwa na nambari KBA/ PE/23/2011 ambalo mhusika wake ni Mwingira.
Shauri hilo linasomeka kwenye kumbukumbu za jeshi la polisi KBA/ PE/23/2011 JALADA LA UCHUNGUZI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ACP Unrich Matei, alilithibitishia gazeti hili kwamba kweli jalada hilo lilifunguliwa na tuhuma zake ni hizo za Morris kudai Mwingira amezaa na mkewe.
UTHIBITISHO WA BARUA YA POLISI
Habari zinasema kuwa Morris alipofungua shauri hilo, haikuchukua muda mrefu alirudishiwa majibu kwamba tuhuma zake azipeleke mahakamani kwa sababu hazina mashiko katika jinai.
Awali, tuhuma zake zilijipambanua kwamba Mwingira amekuwa na uhusiano usiofaa na mkewe (Philis) mpaka kumpa ujauzito na hatimaye mtoto akazaliwa.
Katika barua hiyo, iliyosainiwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (RCO), Mkoa wa Pwani, SSP E.H. Mwijage, ilimwelekeza Morris kutafuta haki katika mkondo mwingine wa sheria, hususan mahakamani.
Barua hiyo ilikuwa na kichwa; YAH: KBA/PE/23/2011, KOSA: JALADA LA UCHUNGUZI, MTUHUMIWA: JOSEPHAT MWINGIRA.
Vilevile barua hiyo, ilikuwa na kumbukumbu nambari PWA/CID/130/VOL XXV11/211 na ilikuwa ni majibu ya ile ambayo Morris alimwandikia RCO, Desemba Mosi, 2011.
Barua hiyo ya RCO, iliandikwa Januari 25, 2012 ikiwa na maelezo yafuatayo;
“Baada ya uchunguzi makini juu ya malalamiko yako, uchunguzi umebaini kuwa kosa lililofanyika ni adultery (kuzini) au defamation (udhalilishaji) ambapo katika sheria za makosa ya jinai, makosa hayo hayapo.
“Kutokana na sababu hizo hapo juu, tunakushauri uchukue hatua nyingine za kupata haki yao au ufungue kesi ya madai mahakamani dhidi ya mtuhumiwa.”
MORRIS ANASEMAJE?
Morris alitafutwa na waandishi wetu na alipopatikana, alikiri kila kitu lakini alidai kwamba amekuwa akipata shida kufungua kesi ya madai mahakamani kutokana na misukosuko mbalimbali anayopewa.
Alisema, yeye siyo Mtanzania na kutokana na hilo, amekuwa akisumbuliwa na hata kutishiwa kurudishwa kwao.
Aliongeza kwamba ameendelea kushughulikia hili suala lake kwa utulivu bila papara ili asipoteze haki zake za msingi.
UMOJA WA MATAIFA
Kwa upande mwingine, zipo nyaraka ambazo Morris inadaiwa alizituma Umoja wa Mataifa kwa barua pepe (tunayo nakala yake) aliyoielekeza kwa katibu mkuu wa shirika hilo, Ban Ki Moon, Januari 11, 2011.
Hata hivyo, ndani ya barua hiyo, Morris ameeleza tuhuma nyingine mbalimbali kuhusu Mwingira lakini zinahifadhiwa kwa sasa.
Katika barua hiyo, Morris aliomba ulinzi kwa sababu tayari Ubalozi wa Marekani nchini, Umoja wa Ulaya, Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Amnesty International), Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na taasisi ya haki za binadamu nchini, ameshazipa taarifa.
Aidha, Morris alimsisitizia Ki Moon ombi lake la kusaidiwa kupata haki zake na mkewe pamoja na madai mengine aliyoyaandika katika waraka huo.
CHETI CHA NDOA
Kwa mujibu wa Morris, Philis ni mke wake halali, aliyefunga naye ndoa takatifu katika Kanisa la St. Alban jijini Dar es Salaam, Desemba 23, 2001, akiwa na umri wa miaka 39 na mkewe wakati huo alikuwa na miaka 30 na kupewa cheti cha ndoa namba B. 0638572 na ilifungishwa na Padri Canon William Kambanga.
Uwazi linayo nakala ya cheti hicho cha ndoa.
MKE NAYE AZUNGUMZA
Kuhusu tuhuma hizo, Philis alisema kuwa Mwingira hahusiki kwenye matatizo yao.
“Yule alinitelekeza, siyo mume wangu,” alisema Philis na kuongeza: “Angekuwa mume kweli asingenitelekeza na kunisaliti mpaka kwa mtoto wa kike ambaye tunaweza kumzaa.”
Aliongeza kuwa alimvumilia Morris kwa mambo mengi na hawezi kumsamehe kwa sababu alimuumiza sana.
MWANDISHI: Kwa maana hiyo unakiri kwamba ulizaa na mwanaume mwingine?
PHILIS: Ni kweli, nilifanya hivyo baada ya yeye kunitelekeza na hakuwa na uwezo wa kunizalisha.
MWANDISHI: Huyo mwanaume ni nani? Ni Mwingira?
PHILIS: Hilo swali siwezi kujibu, iwe Mwingira au mwanaume mwingine yeyote, labda kwa wakili wangu au mahakamani.
MWANDISHI: Unafahamiana na Mwingira kwa ukaribu?
PHILIS: Ndiyo nafahamiana naye, ni ndugu yangu.
MWANDISHI: Ndugu yako kivipi? Labda kaka, mjomba au?
PHILIS: Wewe elewa ni ndugu yangu, ila kuhusu ndugu yangu kivipi, hilo swali siwezi kukujibu.
MWANDISHI: Umewahi kuwa muumini wa Mwingira?
PHILIS: Iwe nasali RC, KKKT au vyovyote vile, wewe inakuhusu nini?
MWANDISHI: Kama utasuluhishwa na Morris, unaweza kuishi naye tena?
PHILIS: Wewe kaka, hivi unajua jinsi yule mwanaume alivyoniumiza? Siwezi kabisa.
KUMPATA MWINGIRA SHUGHULI
Waandishi wetu walifanya jitihada za kuzungumza na Mwingira mara tatu bila mafanikio.
Mara ya kwanza, waandishi wetu walikutana na walinzi ambao walisema, hawataonana na Mwingira, isipokuwa wakutane na msaidizi wake ambaye anaitwa Mchungaji Urasa.
Mara ya pili, waandishi wetu walikutana na Urasa ambaye alisema ili kumuona Mwingira inabidi kuandika nambari ya simu, jina na mahali ambako wanatoka.
Mmoja wa waandishi wetu aliacha jina, nambari ya simu na maelezo mengine yaliyohitajika lakini hakupata majibu yoyote.
Jumapili iliyopita, waandishi wetu walirudi kanisani Efatha kwa mara ya tatu na kukutana na mtu anayeitwa Samuel Peter ambaye alijitambulisha kama mtumishi.
Waandishi wetu walipomuomba Samuel awape muongozo wa kuonana na Mwingira, alijibu: “Siyo rahisi kumuona nabii.”
Hata waandishi wetu walipoomba nafasi ya kuonana na Urasa ili kukumbusha ahadi ya mwanzo, Samuel alijibu: “Hata Urasa hamuwezi kumuona, mbona huwa hamji kuripoti habari za ukombozi kama misukule? Hamuwezi kuwaona wote hao.”
KAMANDA WA POLISI
Jumapili iliyopita, Kamanda Matei, alipoulizwa kuhusu maendeleo ya kesi hiyo ya Morris na Mwingira, alisema anahitaji mlalamikaji aende ofisini kwake.
“Ni kweli tukio hilo lipo kituoni lakini jalada lake likafungwa. Naona mazingira ya kulifunga lile jalada hayakuwa sahihi, nahitaji aje ofisini kwangu tuone nini hasa kilisababisha lile jalada la uchunguzi likafungwa,” alisema Matei.
Alifafanua kuwa kesi hiyo ilifunguliwa wakati Pwani ikiwa na kamanda mwingine, kwa hiyo yeye amelikuta shauri hilo.
“Unajua yale ni madai tu, inabidi mlalamikaji aje atupe ushirikiano, mtoto apimwe damu kwa ajili ya DNA, vile vinasaba ndivyo vitatoa jibu yule mtoto ni wa nani,” alisema Kamanda Matei.

KISA ULEMAVU, MAMA AMTUPA MTOTO

Stori: IGENGA MTATIRO, TARIME.
MTOTO wa kiume mwenye umri wa siku tatu ametupwa na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Bhoke Masero katika Kijiji cha Nyasaricho, kwa kile kilichodaiwa kuwa ulemavu wa mdomo aliozaliwa nao.
Kwa mujibu wa wazazi wa kijana Chacha Sylvester aliyedaiwa kumpatia ujauzito binti huyo, Scholastica na Sylevester Chacha, mama wa mtoto huyo alimtupa na kumtelekeza mtoto huyo majira ya saa 12.00 jioni nyumbani kwao wiki iliyopita.
Walidai kuwa binti huyo aliyetupa mtoto alifika nyumbani hapo akiwa ameongozana na wazazi wake waliowataja kwa majina ya Kambi Siruri na Paulina Kambi wakiwa na mama mdogo wake ambapo walikiweka kichanga hicho mezani na kutoweka.
Kufuatia tukio hilo, wazazi hao walilazimika kupiga simu kituo cha Polisi…

Stori: IGENGA MTATIRO, TARIME.
MTOTO wa kiume mwenye umri wa siku tatu ametupwa na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Bhoke Masero katika Kijiji cha Nyasaricho, kwa kile kilichodaiwa kuwa ulemavu wa mdomo aliozaliwa nao.
Kwa mujibu wa wazazi wa kijana Chacha Sylvester aliyedaiwa kumpatia ujauzito binti huyo, Scholastica na Sylevester Chacha, mama wa mtoto huyo alimtupa na kumtelekeza mtoto huyo majira ya saa 12.00 jioni nyumbani kwao wiki iliyopita.
Walidai kuwa binti huyo aliyetupa mtoto alifika nyumbani hapo akiwa ameongozana na wazazi wake waliowataja kwa majina ya Kambi Siruri na Paulina Kambi wakiwa na mama mdogo wake ambapo walikiweka kichanga hicho mezani na kutoweka.
Kufuatia tukio hilo, wazazi hao walilazimika kupiga simu kituo cha Polisi Bomani kwani mtoto huyo anapata taabu kunyonya au kunyweshwa chochote kutokana na ulemavu wake wa mdomo. Polisi hao waliwataka kwenda kituoni kuandikisha maelezo.
Walisema walijaribu kuwasihi wazazi hao kutofanya kitendo hicho wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasaricho lakini bila mafanikio.
Ilielezwa kuwa mama mzazi wa mtoto huyo aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya mtu aliyedai kumpa ujauzito huo, Sylvester kuukana baada ya kujulishwa.
Gazeti hili lilifanikiwa kufika kwenye tukio, kituo cha Polisi Bomani na Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ambako mtoto huyo aliyelazwa katika wodi namba tano anaendelea vizuri.
Afisa Ustawi wa Jamii wa hospitalini hiyo Abeil Gichaine, alisema mama mzazi wa mtoto huyo anaendelea kutafutwa na polisi pamoja na mambo mengine, aweze kumnyonyesha.
‘’Kwa vile mama mzazi yupo, tunamtafuta ili aweze kumnyonyesha mwanaye,” alisema.

MWANAMKE AMWAGIWA MAJI YA MOTO

Stori: Mwandishi Wetu, Musoma

Msichana mmoja, Mariam Chacha, mkazi wa Mtaa wa Nyasho A, mjini hapa amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa mwili, hali iliyofanywa alazwe katika hospitali ya mkoa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa mbili usiku ambapo inadaiwa aliyefanya kitendo hicho ni Pendo Wambura ambaye amekamatwa na polisi.
Habari kutoka ndani ya kituo cha polisi mjini hapa zinadai kuwa mara baada ya Mariam kumwagiwa maji ya moto mwenzake na kuungua sehemu za kitovu mpaka usoni, matiti na mikono na akiwa hajitambui mpaka sasa,wasamaria wema walimpeleka polisi ili kupata hati ya matibabu (PF 3) na akaenda kutibiwa katika Hospitali ya Serikali ya Musoma alikolazwa wodi namba nne.
“Polisi tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia…

“Polisi tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa kuwa majeruhi hali yake ni mbaya, kalazwa, na tayari amefunguliwa jalada namba MUS/IR/5009/013,” alisema afisa mmoja wa polisi kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Shuhuda mmoja aliliambia gazeti hili kwamba Mariam alikwenda kuwasalimia ndugu zake pamoja na mama yake ambaye ni mgonjwa wanaokaa nyumba moja na mtuhumiwa.
“Mariam alipoona hali ya mama yake alianza kulia ndipo Pendo alipokwenda kuchukua maji yaliyokuwa yakichemka ili yapikiwe ugali wa mama mwenye nyumba na akamwagia mwenzake akidai eti anachukizwa na kitendo chake cha kumlilia mgonjwa wake,” kilisema chanzo.

No comments:

Post a Comment