Miili
ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya
kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala
ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
Baadhi
ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma walikufa kutokana
na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori
hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani
hapo.
Baadhi
ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada
katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara
CBE Dodoma.
Asikari
wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu
ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.
Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara wamepoteza CBE wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya
kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya
kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa
wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji
cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika
barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa
zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza
utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha
pikipiki hiyo yenye namba za usajili T
420 CCN waliokuwa wakukitokea barabara
ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala
wanafunzi wa CBE na kwamba uzembe wa
Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838
AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala kuweka alama yoyote huku
matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika
vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo
na ubongo kusambaa katika eneo hilo
imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.
No comments:
Post a Comment