- Tanzania ilitwaa medali 72 kwenye mashindano hayo 22 dhahabu, 25 za fedha, 25 za shaba, huku muogeleaji Hilal
Tanzania ilitwaa medali 72 kwenye mashindano hayo 22 dhahabu, 25 za fedha, 25 za shaba, huku muogeleaji Hilal
Hilal akivunja rekodi kwa kupata medali 15 katika
mtindo wa free style mita 50, 100, 200, 400 na 800, butterfly mita 50 na
100, breaststroke mita 50 na 200, backstroke mita 50,100,
Individual Medley mita 100 na 200 na kwenye relay mita 200 freestyle, backstroke na Medley.
Akizungumza katika hafla ya kuipongeza timu hiyo
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Michezo nchini, Juliana Yasoda alisema ushindi huo ni
faraja kubwa kwa taifa.
Yasoda alisema timu hiyo imeonyesha ukakamavu wa
hali ya juu kwenye mashindano hayo na kuitaka kuendeleza rekodi hiyo
kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwakani na ile ya Cana ya kanda
ya nne na ya tano.
“Hatua mliyofika kwenye mashindano ya Afrika
Mashariki ni kubwa si tu kwenu nyinyi bali taifa zima la Tanzania,
mmetuwakilisha vyema na sisi tunaahidi kuwa bega kwa bega na nyinyi,”
alisema Yasoda.
Kwa mujibu wa Katibu msaidizi wa Chama cha
Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka, kikosi cha Tanzania Swim
Squad kilikuwa na wachezaji 42 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es
Salaam.
Namkoveka alisema katika mbizi hizo Tanzania Swim
Squad ilitwaa medali katika mitindo ya Backstroke, Breaststroke,
butterfly, Free Style na Individual Medly ambayo ilishindanishwa kwenye
mashindano hayo.
“Huo ni mwanzo mzuri kwa timu ya taifa ya
kuogelea, hasa baada ya chama kuamua kuweka viwango kwa wachezaji wa
timu ya taifa kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa na kwa
ushirikiano na wazazi tumefanikiwa hivyo mikakati hiyo itaendelezwa
kwenye kalenda yetu ya mwakani ambapo tutakuwa na mashindano mbalimbali
ya kimataifa,” alisema Namkoveka.
No comments:
Post a Comment