Saturday, November 9, 2013

Mwendesha Mashtaka auawa Libya

Moja ya matukio ya milipuko ya mabomu yaliyotegwa kwenye gari nchini Libya
Mwendesha Mashtaka Mohammed al Naass ameuawa kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa bandari wa Darna mashariki mwa Libya.
Wakati huo huo polisi wawili wamepigwa risasi katika mji wa Benghazi ambapo ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linasema karibu watu hamsini wameuawa tangu mwaka 2012 katika matukio yanayohusiana na mgogoro wa kisisiasa katika miji miwili iliyopo mashariki.
Pia kumekuwa na hali machafuko katika mji kuu wa Tripoli tangu mwishoni mwa wiki wakati makundi mawili ya wapiganaji yalipopambana kwa kutumia bunduki na silaha nzito nzito na kufanya milio ya makombora kusikika katika baadhi ya maeneo ya mji huo.
Karibu watu kumi wameripotiwa kujeruhiwa katika ghasia hizo.


Taarifa na BBC Swahili

No comments:

Post a Comment