Saturday, November 9, 2013

SIRI ZA KUDUMISHA PENZI LAKO LISITETEREKE! kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi.


Posted by Mayness on November 8, 2013 at 9:17am 0 Comments 0 Likes
NAKUKARIBISHA kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi. Ni imani yangu, umekuwa ukipata maarifa mapya kila siku kupitia hapa. Kaa tayari uvune kitu kipya leo.

Kwanza kabisa, napenda kuchukua  nafasi hii kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia ya simu na kunipongeza, kunikosoa na kuuliza maswali kuhusu mambo mbalimbali yanayowakabili katika uhusiano.
Kufanya kwenu hivyo kunanipa moyo kwamba, ujumbe unawafikia vilivyo. Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Nazungumzia juu ya mambo ya kuzingatia kama unahitaji kudumu katika uhusiano

ulionao.
Hapa naomba nizungumze na wanawake zaidi. Hii haina maana kwamba, wanaume hawahusiki katika mada hii.    Ni ukweli kwamba…
NAKUKARIBISHA kwa moyo mkunjufu katika safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi. Ni imani yangu, umekuwa ukipata maarifa mapya kila siku kupitia hapa. Kaa tayari uvune kitu kipya leo.

Kwanza kabisa, napenda kuchukua  nafasi hii kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia ya simu na kunipongeza, kunikosoa na kuuliza maswali kuhusu mambo mbalimbali yanayowakabili katika uhusiano.
Kufanya kwenu hivyo kunanipa moyo kwamba, ujumbe unawafikia vilivyo. Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Nazungumzia juu ya mambo ya kuzingatia kama unahitaji kudumu katika uhusiano
ulionao.
Hapa naomba nizungumze na wanawake zaidi. Hii haina maana kwamba, wanaume hawahusiki katika mada hii.    Ni ukweli kwamba wanawake ndiyo wanaokumbana zaidi na matatizoya kuachwa na wapenzi wao kuliko wanaume kuachwa solemba na wenzi wao. Ni sahihi kusema, wanawake ndiyo huumizwa zaidi katika mapenzi kuliko wanaume.

Hii ni kutokana na sababu kubwa mbili; kwa kawaida wao ndiyo hufuatwa na kutongozwa na wanaume, lakini lingine ni kwamba, mara nyingi wanaume ndiyo hutoa uamuzi wa kuacha au kuachana. Kwa sababu hizo, hakuna ubishi kuwa wanawake ndiyo walengwa wakubwa wa mada hii. Rafiki zangu, kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kusababisha uhusiano kuwa butu na baadaye  kuishia njiani. Hapa katika Let’s Talk About Love nitakupa dondoo za kuzingatia ili usiingie kwenye matatizo niliyoeleza hapo juu. Jambo kubwa kabisa ambalo unatakiwa kulifahamu mpenzi msomaji wangu ni kuwa, mwanaume anahitaji kuwa na mwanamke wake ambaye atakuwa kila kitu kwake. Hebu sasa twende tukaone vipengele vyenyewe.

UTAMBUZI WA THAMANI
Ili uweze kuwa bora ni lazima uanzie kwako, ujitambue kama mwa n a - mke na thamani yako kwa mwanaume wako.
Ukiijua thamani yako, lazima utakuwa makini na kila kitu. Rafiki yangu, ninaposema thamani ninamaanisha kwanza kujiamini na kujipa nafasi ya kwanza.
Uamini kwamba wewe ni mwanamke mrembo na unayevutia. Imani hiyo ikishaingia, tayari utakuwa unajali mambo
mengi ya msingi, ikiwemo usafi wako binafsi. Waswahili wanasema, mwanamke ni pambo la nyumba. Pambo haina maana  ya ua, inamaanisha ule usafi wa kila kitu.

Kwamba nyumba bila mwanamke haiwezi kukamilika, wewe kama mwanamke unatakiwa kufahamu wewe ni kila  kitu ndani ya nyumba. Umakini wako na kujitambua ndiyo vitu vitakavyokuweka katika nafasi nzuri ya kudumu katika uhusiano wako na baadaye kuingia katika ndoa.

TAMBUA THAMANI YAKE
Ukiijua thamani ya mwanaume kutoka ndani ya moyo wako ni wazi kwamba hata vipengele vifuatavyo hapa chini havitakuwa vigumu kwako kutekelezeka. Inakupasa ujue thamani ya mwanaume wako.
Hilo si tu kwa maneno, bali ni jambo ambalo litatakiwa kufanyika kwa ridhaa ya moyo wako. Ni rahisi zaidi jambo hili kufanyika ikiwa utakuwa na mapenzi ya dhati. Mpende kwa moyo wako wote na ujue kuwa maisha yako yanakamilishwa  na uwepo wake. Ndiyo! Yanakamilishwa na uwepo wake, maana una mategemeo ya kuingia katika ndoa naye. Hapo mtakuwa mwili mmoja na maisha ya kila mmoja yatamtegemea mwenzake. Bado kuna vitu vya kujifunza zaidi. Wiki ijayo tutaendelea. Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vitatu; True Love, Let’s, Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

No comments:

Post a Comment