Friday, November 8, 2013

Soma magazeti ya leo Alhamis ya tarehe 7/11/2013 Hapa.......



BAADA YA KUTOKA LUPANGO, MASOGANGE APIGA ZA UTUPU

Na Gladness Mallya

SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi…
Na Gladness Mallya
SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.
Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.

NDOA YA BOB JUNIOR CHALI


Na Waandishi Wetu

MIEZI michache baada ya kufunga ndoa na kupata mtoto, Prodyuza na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ na mkewe Halima Ally wameachana, Amani linakuhabarisha.

Habari kutoka katika chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu na Bob Junior zinasema kwamba, ndoa hiyo ilivunjika muda mrefu lakini wahusika walikuwa wakifanya siri lakini Amani limeinasa.
Siku ya ndoa.
BOB JUNIOR TATIZO

Kwa mujibu wa jamaa huyo ambaye hakutaka…

Na Waandishi Wetu
MIEZI michache baada ya kufunga ndoa na kupata mtoto, Prodyuza na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ na mkewe Halima Ally wameachana, Amani linakuhabarisha.
Habari kutoka katika chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu na Bob Junior zinasema kwamba, ndoa hiyo ilivunjika muda mrefu lakini wahusika walikuwa wakifanya siri lakini Amani limeinasa.
Siku ya ndoa.
BOB JUNIOR TATIZO
Kwa mujibu wa jamaa huyo ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema chanzo cha kuparaganyika kwa ndoa hiyo ni Bob Junior mwenyewe kutokana na kutuhumiwa na mkewe kumsaliti.
“Mke wake alikuwa anamtuhumu Bob kutoka kimapenzi na mwanamke mmoja wa Kikenya na pia inasemekana anatembea na Vanessa Mdee (mwanamuziki). Maneno yalivyokuwa mengi, mkewe akaamua kuondoka, hivi ninavyoongea na wewe, yupo kwao,” alisema.
Siku walipopata mtoto.
BOB JUNIOR AKIRI
Mashitaka yote yalifikishwa kwa Bob Junior kama yalivyo ambapo bila kumung’unya maneno, msanii huyo mwenye mauno sana awapo jukwaani alikubali kutengana na mkewe lakini akachomoa suala la Mkenya na
Vanessa.
“Ni kweli nimeachana na mke wangu kama mwezi mmoja uliopita na ameondoka na mtoto, hayo maneno kwamba nina mwanamke wa Kikenya siyo ya kweli. Vanessa ni msanii mwenzangu, nafanya naye kazi tu, hakuna cha zaidi,” alisema.
YUKO NA NANI SASA?
Alipoulizwa kama ameshafungua ukurasa mwingine wa kimapenzi alisema: “Nimeshasema nimeachana na mke wangu, kwa sasa niko singo, sina mpenzi wala mchumba, niko singo tu.”
Bob Junior alipoulizwa kama atarudiana na mkewe alisema hana uhakika ila kama Mungu ndiye aliyepanga watarudiana lakini kama siyo hawatarudiana.
VANESSA NAYE
Vanessa alipopatikana kwa njia simu na kuelezwa kila kitu, alisema: “Siwezi kuzungumzia suala hilo maana kila jambo huwa lina mipaka yake.”
Imeandikwa na Musa Mateja na Gladness Mallya.

Khamis Mkundo Kijana aliyejinyonga.
Na Francis Godwin, Iringa

MADENTI wa Shule ya Sekondari Sabasaba na Kituo cha Krelluu mjini hapa wamemlilia mwenzao, Khamis Mkundo aliyejinyonga kwa hofu ya kufeli mtihani wa taifa (Necta) wa kidato cha nne, mwaka huu.
Hii ndo barua ya  Khamis Mkundo aliyoiacha kabla ya kujinyonga.
Denti huyo, mkazi wa Mwangata C mjini hapa aliwaliza wenzake aliokuwa akisoma nao Sabasaba na…
Khamis Mkundo Kijana aliyejinyonga.
Na Francis Godwin, Iringa
MADENTI wa Shule ya Sekondari Sabasaba na Kituo cha Krelluu mjini hapa wamemlilia mwenzao, Khamis Mkundo aliyejinyonga kwa hofu ya kufeli mtihani wa taifa (Necta) wa kidato cha nne, mwaka huu.
Hii ndo barua ya  Khamis Mkundo aliyoiacha kabla ya kujinyonga.
Denti huyo, mkazi wa Mwangata C mjini hapa aliwaliza wenzake aliokuwa akisoma nao Sabasaba na baadaye kwenye kituo hicho ambapo alikuwa ‘akiristi’ baada ya kufeli mtihani huo zaidi ya mara moja.
Wana usalama wakisoma barua aliyoiacha denti huyo.
“Inauma sana, marehemu alikuwa akijitahidi sana kusoma, tuliweka mikakati ya pamoja ili tuweze kufanya vizuri mwaka huu lakini ghafla tukasikia amejiua,” alisema mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Jamaa huyo alijiua Jumapili iliyopita kwa kujinyonga kwa kamba na kuacha barua ndefu iliyosomeka kuwa amefanya hivyo si kwa kupenda, ila alichukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara akajiua ili kuepuka aibu hiyo.

ARSENAL, CHELSEA, BARCELONA ZAUA

Wachezaji wa Arsenal Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao lao la pekee dhidi ya Dortmund. Bao hilo limefungwa na Ramsey dakika ya 62.
Mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o akishangilia na kocha wake Jose Mourinho baada ya kuifungia timu yake bao.…
Wachezaji wa Arsenal Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao lao la pekee dhidi ya Dortmund. Bao hilo limefungwa na Ramsey dakika ya 62.
Mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o akishangilia na kocha wake Jose Mourinho baada ya kuifungia timu yake bao.
Lionel Messi (kushoto) akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake ya Barcelona na Cesc Fabregas.
Arsenal, Chelsea na Barcelona zimeibuka na ushindi katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizopigwa usiku huu. Arsenal wameilaza Borussia Dortmund bao 1-0, Chelsea wakiizamisha 3-0 timu ya Schalke 04 wakati Barcelona wakiichachafya AC Milan bao 3-1. Bao la Arsenal limefungwa na Aaron Ramsey ya Chelsea yakiwekwa kimiani na Samuel Eto'o aliyefunga mawili na Demba Ba wakati ya Barcelona yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili na Sergio Busquets na lile la AC Milan Gerard Pique aliyejifunga.

No comments:

Post a Comment