Saturday, November 9, 2013

MWANAMKE, MWANAUME WAFA WAKIWA WAMEKUMBATIANA!

NA MWANDISHI WETU,GEITA

Watu w a w i l i a m b a o hawakufahamika majina yao, wamefariki dunia papohapo wilayani Bukombe mkoani Geita baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga kisha kugongwa na gari aina ya Noah. Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, ilitokea hivi karibuni ambapo dereva wa bodaboda hiyo alikuwa amembeba mwanamke pamoja na mizigo mingi.
Shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini akisimulia zaidi alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo kilitokana na dereva wa bodaboda aliyekuwa akiendesha kwa kasi kushindwa kuimudu pikipiki yake iliyoteleza kwenye mchanga. “Wakati akipishana na gari pikipiki yake iliteleza kwenye mchanga na kuanguka katikati ya barabara ndipo gari aina ya Noah ambayo namba zake…
NA MWANDISHI WETU,GEITA
Watu w a w i l i a m b a o hawakufahamika majina yao, wamefariki dunia papohapo wilayani Bukombe mkoani Geita baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga kisha kugongwa na gari aina ya Noah. Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, ilitokea hivi karibuni ambapo dereva wa bodaboda hiyo alikuwa amembeba mwanamke pamoja na mizigo mingi.
Shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini akisimulia zaidi alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo kilitokana na dereva wa bodaboda aliyekuwa akiendesha kwa kasi kushindwa kuimudu pikipiki yake iliyoteleza kwenye mchanga. “Wakati akipishana na gari pikipiki yake iliteleza kwenye mchanga na kuanguka katikati ya barabara ndipo gari aina ya Noah ambayo namba zake hazikunaswa aliyokuwa akipishana nayo ikawapitia vichwani na kufa papohapo wakiwa wamekumbatiana,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:“Ni ajali mbaya sana kwani wote wawili wamekufa palepale, mbaya zaidi hawajafahamika ni wakazi wa eneo gani,” alisema shuhuda huyo.

No comments:

Post a Comment