Friday, November 8, 2013

Magazeti ya leo tarehe 7/11/2013 Alhamisi ni raha tupu soma hapa hapa.......

DIAMOND ‘AHENYESHWA’ NA MISIBA YA WAKWE ZAKE

Na Musa Mateja

RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameendelea ‘kuhenyeshwa’ na misiba ya wakwe zake kufuatia mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kufiwa na baba yake mdogo, Boniface Mungilwa.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ (katikati) akishiriki mazishi ya baba mzazi wa Wema, Balozi Sepetu Visiwani Zanzibar.
Msiba wa marehemu huyo ulikuwa Magomeni jijini Dar na alizikwa Jumatatu iliyopita. Diamond alifika msibani hapo na kujumuika na waombolezaji wengine.
Hivi karibuni, Diamond alifiwa na ‘baba mkwe’ wake mwingine, mzee Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba mzazi wa mpenzi wake, Wema Sepetu mazishi…
Na Musa Mateja
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameendelea ‘kuhenyeshwa’ na misiba ya wakwe zake kufuatia mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kufiwa na baba yake mdogo, Boniface Mungilwa.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ (katikati) akishiriki mazishi ya baba mzazi wa Wema, Balozi Sepetu Visiwani Zanzibar.
Msiba wa marehemu huyo ulikuwa Magomeni jijini Dar na alizikwa Jumatatu iliyopita. Diamond alifika msibani hapo na kujumuika na waombolezaji wengine.
Hivi karibuni, Diamond alifiwa na ‘baba mkwe’ wake mwingine, mzee Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba mzazi wa mpenzi wake, Wema Sepetu mazishi yalifanyika Zanzibar ambapo pia Diamond alihudhuria.

RAY AELEZA SABABU ZA KUIGIZA MUVI ZA MAPENZI

Na Gladness Mallya

STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua ya filamu husika kufungiwa.

“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu. Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam hawakunielewa mpaka baadaye. Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza filamu za mapenzi tu,” aliema…

NATASHA: SIKUJUA KAMA NDOA NI TAMU HIVI

Na Gladness Mallya
IMEPITA miezi minne tangu msanii mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ aingie kwenye ndoa, juzikati amefunguka kwamba amegundua ndoa ni tamu na anajiuliza kwa nini hakulijua hilo mapema.
Akistorisha na gazeti hili, Natasha alisema baada ya kuingia kwenye ndoa amejikuta akifurahia maisha tofauti na yale aliyokuwa akiishi wakati wa ubachela.
“Nafurahia ndoa kwa sababu tuko wawili, nikisikitishwa na jambo napata faraja kutoka kwake. Nikitaka kwenda mbali naomba ruhusa kwa mume wangu, hilo pia linanipa furaha,” alisema Natasha.

No comments:

Post a Comment