Waziri wa mambo ya nje wa Iran, amesema kuwa anaamini makubaliano kuhusu mpango wake wa Nuklia yataafikiwa mwishoni mwa Ijumaa.
Mohammad Zarif ameambia CNN kuwa Iran
haitasitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium kabisa lakini
inaweza kujizuia naa baadhi ya maswala yanayozungumziwa.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ambaye anazuru Mashariki ya Kati, anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo siku ya Ijumaa.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye msafara wa Bwana Kerry, anasema kuwa uamuzi wake kubadili mipango yake ya safari nchini Saudi Arabia na kwenda Geneva, ni dalili tosha kuwa mkataba huenda ukaafikiwa kati na Iran
Mnamo siku ya Alhamisi, Marekani ilithibitisha kuwa baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran vitalegezwa ikiwa Iran itachukua hatua muhimu na ambazo zinaweza kuthibitishwa katika mpango wake wa nuklia.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema kuwa ikiwa mkataba utafikiwa litakuwa kosa la kihistoria na kuituhumu Iran kwa kutokuwa mkweli.
Wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ujerumani , walikutana kwa mazungumzo kuhusu Iran siku ya Alhamisi mjini Geneva.
Nchi za Magharibi zinashuku kuwa mpango wa Iran wa kurutubisha madini ya Uranium ni hatua ya kutaka kujenga zana za nuklia.
Na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment